TSIF – How willing are you to go above and beyond? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TSIF – How willing are you to go above and beyond?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Jun 5, 2009.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Thank Someone It’s Friday

  Mshikaji wangu mmoja (mbongo) ni software engeener (programmer??) huku kwa Obama. Basi juzi kati hapa wakati tunapiga stori, akazungumzia ishu ambayo nikamwona jamaa ni "mchapa kazi" kweli kweli. Eti, kuna “ki-parameter” kwenye program moja ya jobuni kwake ilikuwa inamsumbua sana kwa siku kadhaa. Basi kila akifanya manjonjo yake, ki-error bado kinamulika. Sasa siku moja mida ya naiti kali, akiwa anasaka usingizi kitandani, akagundua mbinu ya kumrekebisha yule mdudu-error. Basi mzee akakurupuka mida ile ile, akachoma motokaa mpaka job, na kuingia mitamboni. Bingo! ka-parameter kakasalenda …..program ikanyooka. Mchezo kwisha!

  Sasa mimi nikawa najiuliza….yaani mshikaji ametimka usiku wa manane kwenda job kurekebisha program? Kwa nini asingeandika kwenye karatasi alichogundua, halafu akaenda kukishughulikia kesho yake mida ya kazi??

  Duh basi nikajiona kweli mimi sio nguvu kazi. Yaani niutose usingizi, kwa shughuli ambayo inaweza kusubiri! Nyoooo…..Thubuutuuu!!!! Sijafikia (na ninaweza nisifike) huko kabisaaa! Kwanza huwa saa 11 kamili jioni ikigonga tu, mimi tayari niko mlangoni…nachumpa! Ndo imetoka hiyo... Na nikishachomoka tu, sifikirii wala sigusi makolokolo ya mzigoni ng’o…..mpaka kwenye saa 2 na ushehee kesho yake asubuhi!

  Hata hivyo, mshikaji kanifanya nijione choo kweli....

  Je unaweza kupima vipi dedication yako kwa kazi na/au mwajiri wako?
   
 2. B

  Babu Swahili Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe kijana uwezi kuandika kiswahili kilichonyooka? Vijana wa siku hizi mnajifanya wa mjini.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hiyo huwa inatokea, nyingine inakuja kwa "serendipity" tu. Unajua aliyegundua cherehani alifikiri sana bila kupata design, akaenda kulala akaiota cherehani nzima nzima pamoja na vikorombwezo vyake vyote, baada ya hapo akaamka mara moja na kuichora na kuifanyia kazi.

  Kuandika program ni sayansi iliyo kama sanaa, ni kama kuandika wimbo au hadithi, au kucheza mpira kuna wakati unakuwa kwenye mood/ form na wakati mwingine unakuwa huna.Kwa hiyo huyu jamaa akaona bora aifanyie kazi hiyo inspiration/ burst of insight kabla haijamtoka.

  Programming is not for the faint of heart, ina torture saa nyingine, kuna watu wana enjoy hiyo challenge.
   
Loading...