Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,361
- 4,816
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Marekani Donald Trump wamesema wanatafakari namna ya kuendeleza uhusiano wao wa karibu na kukubaliana kwa kile walichokiita "makubaliano makubwa ya biashara huria." Katika mawasiliano ya njia ya simu inaelezwa pia Trump alimpongeza Johnson kufuatia ushindi wa chama chake cha kihafidhina, katika matokeo ya uchaguzi wa Uingereza.
Maeneo ambayo yanazingatiwa kwa pande zote za Marekani na Uingereza ni pamoja na ulinzi na biashara. Aidha katika kufanikisha malengo ya viongozi hao mawaziri wa fedha wa Uingereza, Sajid Javid na mwenziwe wa Marekani Steve Mnuchin pia walipata nafasi ya kuzungumza.