Trump: Mayahudi wa Marekani hawaipendi tena Israel amlaani Netanyahu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Trump: Mayahudi wa Marekani hawaipendi tena Israel

Dec 19, 2021 08:18 UTC

[https://media]Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Mayahudi wa Marekani hawaipendi tena Israel

Donald Trump aliyekuwa akizungumza na mwandishi habari wa mtandao wa Kizayuni wa Valla, Barack Ravid, ameeleza mitazamo yake kuhusu Wayahidi wa Marekani. Ameashira kuwa gazeti la New York Times linaendeshwa na Mayahudi na kusema: Wayahudi wanaoishi Marekani hawaipendi tena Israel.

Trump ameeleza kuwa "Hapo zamani, Israel ilikuwa na mamlaka kamili juu ya Bunge la Marekani (Kongresi) na leo hali imekuwa kinyume kabisa na kuongoza kwamba, Wakristo wa Kiinjilisti nchini Marekani wanaipenda zaidi Israel kuliko Wayahudi.

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo iliyotangazwa Ijumaa ya wiki iliyopita, rais huyo wa zamani wa Marekani alisema kwamba, hakuna kiongozi wa Marekani aliyemfanyia kazi kumhudumia Netanyahu na Israel kama yeye. Amesema mpango wa "Muamala wa Karne" ulikuwa jambo kubwa na kwamba alifanikisha mpango huo kabla ya uchaguzi wa Israel na kumsaidia sana Benjamin Netanyahu.

Trump ameendelea kumshambulia waziri mkuu wa zamani wa Israel akisema: "Netanyahu alikuwa mtu wa kwanza kumpongeza Joe Biden na kwamba alifanya hivyo kwa njia ya video."

[https://media]Trump: Sitamsamehe Netanyahu, laana zimshukie!

"Lilikuwa kosa kubwa", amesisitiza rais huyo wa zamani wa Marekani na kuongeza: "Tangu wakati huo sijazungumza na Netanyahu. Laana zimshukie! Sitamsamehe."

Katika sehemu nyingine ya mahojiano yake Trump amesema: "Kama nisingekuwa rais wa Marekani, nadhani Israel ingetokomezwa."

4by87568f312671zrq6_800C450.jpg
 
Unatia huruma sana. Hapo ulipo umejaa chuki juu ya Marekani na Israel.
Hapo ulipo unatumia dawa za Marekani na unaangalia movie kutoka Hollywood. Ndugu zako wanachojua ni kwenda kuswali, kula tende na kutengeneza bunduki za kuana tu.
Iran ikitoa msaada ni kujenga msikiti tu.
Badilika, chuki zako hazikusaidii chochote. Hapo ukipewa visa ya Iran na Marekani utaenda Marekani.
 
Unatia huruma sana. Hapo ulipo umejaa chuki juu ya Marekani na Israel.
Hapo ulipo unatumia dawa za Marekani na unaangalia movie kutoka Hollywood. Ndugu zako wanachojua ni kwenda kuswali, kula tende na kutengeneza bunduki za kuana tu.
Iran ikitoa msaada ni kujenga msikiti tu.
Badilika, chuki zako hazikusaidii chochote. Hapo ukipewa visa ya Iran na Marekani utaenda Marekani.
unateseka sana kijana kunywa maji mengi utakufa kwa pressure

Sent from my SM-J5108 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom