Trump kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani

Natalia

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
4,324
1,892
From Syria,Iraq ,Iran ,Libya,Somali ,Sudan ,Yemen .He will use George bush bill to build the wall in Mexico .Nchi 9 za Africa hazitopata msaada mpaka waonyeshe maendeleo .

=====

1.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini sheria kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Taarifa kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani leo Jumatano.

Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi

Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi.

Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Chanzo: BBC
 
Ngoja Africa sasa tuisome namba na pia akili na utashi wa kutumia vizuri rasilimali tulizonazo ndipo utakaa vizuri kwa sasa.

Pia, siasa uchwara zote ni lazima zifike kikomo ili sasa iwe ni uzalendo , utaifa kwanza na maslahi ya nchi.

Safi sana Trump!!
 
1.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini sheria kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Taarifa kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani leo Jumatano.

Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi

Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi.

Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Chanzo: BBC
 
Trump yuko sahihi kabisa dhidi ya wahamiaji na hasa kutoa North Africa na Middle East. Kazi namba moja ya Serikali yoyote duniani ni ulinzi wa raia wake na mali zao. Haikubaliki mijitu inatoka sijui wapi huko kwenda kuua raia wasio na hatia kwa kisingizio chochote kile.
 
_93792383_trump.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini amri kuu kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Taarifa kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani baadaye Jumatano.

Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi.

Miongoni mwa nchi zitakazoathiriwa na agizo la Trump ni Syria, Yemen, na Iraq.

Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.

Mwandishi wa BBC David Willis kutoka Washington anasema hatua hiyo huenda ikayaudhi mashirika ya kibinadamu na yale ya kutoa misaada ikizingatiwa mzozo unaoendelea kwa sasa kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria.
Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi. Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

_93798285_trumpwall.jpg

Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Chanzo: BBC
 
Safiiiiiiiiiii, Mimi ningekuwa triumph hats bidhaaa kutoka huko nisingezihitaji kabisaaass
Sasa USA ita survive vipi bila bidhaa kutoka huko

Au hujui bidhaa kutoka huko ndio inayoifanya dollar iwe juu na USA iizidi kete urusi

Bila bidhaa kutoka huko USA hamna kitu

unahitaji elimu ndugu
 
Japo sikubaliani na kila kitu ambacho huyu bwana anafanya ila inabidi kumpa credit kwa kusimamia kile anachokiamini.

Kwanza he went thru a rough terrain kufika hapo alipo. He did whatever it takes kuwa hapo. Sasa yupo hapo anafanya kile kile alichokihubiri siku zote bila kupepesa macho. Anaweza kuwa hayupo sawa ila kwake anajiona sawa na ndiyo anachokifanya.

Wengi hubadilika ili kuendana na mtazamo wa society si Trump.
 
Anachokifanya Trump ndicho anachotakiwa kukifanya kiongozi yeyote yule kwa taifa lake.......

Kwa hali ilivyo sasa hivi nchini Marekani.....hasa ukizingatia hali ya usalama.....ni lazima kiongozi anayejua maana ya uzalendo afanye hayo kwa manufaa ya taifa lake......

Trump hapambani na uislam bali anapambana na watu wanaoutumia uislam kama kichaka chao cha kufanyia mauaji ya watu wasio na hatia......na watu hao ni rahisi kuwajua kwa kuwa kwao msamiati wa Amani haupo vichwani mwao bali vurugu.......

Wahamiaji wanaoingia nchi yoyote kwa njia zisizo halali na bila mpango maalumu.....ni rahisi sana kuangukia kwenye uharifu.....hivyo kutishia usalama wa eneo au nchi husika......
 
Back
Top Bottom