Trump hatadumu hata awamu ya kwanza tu, ataondoka.

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,639
22,490
Kwa jinsi mambo yanavyojiri huko USA, sidhani kama Raisi mpya wa Marekani, Donald Trump, anaweza hata kumaliza miaka minne ya utawala wa awamu ya kwanza tu, achilia mbali kushinda awamu ya pili. La karibuni ni lile la kuvitibua sana vyombo vya usalama vya Marekani, kutia ndani CIA, ambao kimsingi ndio wanaohusika na usalama wake wa kila siku. Wahenga walisema usitukane wakunga na uzazi ungalipo, na yeye anaonyesha wazi kutukana wakunga.

Pili ni kwamba inaonyesha wazi kwamba ni rahisi sana kumtafutia jambo la kum-impeach na kumwondoa madarakani (trump-gate) kutokana na na jinsi anavyojiendesha eidha katika maisha yake binafsi, biashara zake au hata mambo ya siasa.

Suala lililopo ni lini hili litatokea! Watch this space.

Updates

Will US President Donald Trump get away with what Richard Nixon could not?
COLBERT I. KING

Last updated 06:04, May 14 2017

http://www.stuff.co.nz/world/americas/92555668/will-us-president-donald-trump-get-away-with-what-richard-nixon-could-not

'I think we're in Trump impeachment territory,' says former aide to Nixon and Clinton
DEREK HAWKINS

Last updated 05:33, May 18 2017

http://www.stuff.co.nz/world/americas/92710411/I-think-we-re-in-Trump-impeachment-territory-says-former-aide-to-Nixon-and-Clinton
 
Kwa jinsi mambo yanavyijiri huko USA, sidhani kama Raisi mpya wa Marekani, Donald Trump, anaweza hata kumaliza miaka minne ya utawala wa awamu ya kwanza tu, achilia mbali kushinda awamu ya pili. La karibuni ni lile la kuvitibua sana vyombo vya usalama vya Marekani, kutia ndani CIA, ambao kimsingi ndio wanaohusika na usalama wake wa kila siku. Wahenga walisema usitukane wakunga na uzazi ungalipo, na yeye anaonyesha wazi kutukana wakunga.

Pili ni kwamba inaonyesha wazi kwamba ni rahisi sana kumtafutia jambo la kum-empeach na kumwondoa madarakani (trump-gate) kutokana na na jinsi anavyojiendehsa eidha katika maisha yake binafsi, biashara zake au hata mambo ya siasa.

Suala lililopo ni lini hili litatokea! Watch this space.

USA civil war haiko mbali, kama Wayahudi na akina Obama wakimuondoa Trump kwa hila mwanzo wa mwisho wa USA utakuwa umekaribia, Trump ndo tegemeo la mwisho la Whiteman baada ya hapo Mzungu kwishnei so Wazungu hawawezi kukubali kuangamia kimya na kuikabidhi nchi yao kwa wapinga Kristo Obama na Wahamiaji masikini!
 
Hizi tabiri uchwara pelekeni uko Democrats...

Donald Trump hata fanya mambo makubwa na mazuri kuliko ndugu yetu mjaruo anaye toka.

hao CIA wanao piga kelele ni ant_trump wasie mtaka kaja...
 
teh! teh! naona mnahamisha tu magori, mlianza ooh hatapita mchujo wa chama! akatoboa. mkaja tena mkiwa mmeungana rais obama, democrats, republican, Papa, media, CIA, EU, nk ooh! hawezi shinda uchaguzi! lakin limdingi limewatoboa. mkaja tena na figisu za kurudia baadhi ya majimbo kuhesabu kura, mkatobolewa. teh! teh! naona bado hamjachoka, ila tambueni huyu mdingi hajawahi kushindwa.
 
Kwa jinsi mambo yanavyijiri huko USA, sidhani kama Raisi mpya wa Marekani, Donald Trump, anaweza hata kumaliza miaka minne ya utawala wa awamu ya kwanza tu, achilia mbali kushinda awamu ya pili. La karibuni ni lile la kuvitibua sana vyombo vya usalama vya Marekani, kutia ndani CIA, ambao kimsingi ndio wanaohusika na usalama wake wa kila siku. Wahenga walisema usitukane wakunga na uzazi ungalipo, na yeye anaonyesha wazi kutukana wakunga.

Pili ni kwamba inaonyesha wazi kwamba ni rahisi sana kumtafutia jambo la kum-empeach na kumwondoa madarakani (trump-gate) kutokana na na jinsi anavyojiendehsa eidha katika maisha yake binafsi, biashara zake au hata mambo ya siasa.

Suala lililopo ni lini hili litatokea! Watch this space.
iyo ni ndoto ya alinacha,,wamarekani kwa asili yao wanataka kiongozi shupavu na jasiri km Trump na co maneno mengi km Obama
 
Trump anaungwa mkono na wazungu(whites)....ila wanyoofu,walokole na kina Obama hawamtaki....hata yeye analijua hilo-kajipanga kukabiliana malo.
 
Ni vizuri tukaweka akiba ya maneno mimi nina wasiwasi wanaweza wakamKennedy kama kawaida yao jamaa anaonekana ana misimamo yake pekee yake
 
teh! teh! naona mnahamisha tu magori, mlianza ooh hatapita mchujo wa chama! akatoboa. mkaja tena mkiwa mmeungana rais obama, democrats, republican, Papa, media, CIA, EU, nk ooh! hawezi shinda uchaguzi! lakin limdingi limewatoboa. mkaja tena na figisu za kurudia baadhi ya majimbo kuhesabu kura, mkatobolewa. teh! teh! naona bado hamjachoka, ila tambueni huyu mdingi hajawahi kushindwa.

Teh teh teh....umewasahau na akina Jay Z, Beyonce, LeBron James na ma celebrity wengine kibao pamoja na mainstream media.

Nacheka sana tena kwa dharau nyingi.
 
Hakuna lisilowezekana japo, kama alivyotamka Michelle Obama hivi karibuni katika speech yake ya mwisho kama First Lady kwamba heshima kubwa kwake zaidi maishani ni kuwa kwake First Lady; vivyo hivyo, nionavyo, heshima kubwa zaidi kwa Trump ni kutangazwa kwake kuwa Rais wa US kuliko hata kukanyaga huko White House. Kumbuka alisema hata huo mshahara wa urais hana haja nao. Historia imeandikwa na hakuna wa kuibadili tena ever and ever.
 
Teh teh teh....umewasahau na akina Jay Z, Beyonce, LeBron James na ma celebrity wengine kibao pamoja na mainstream media.

Nacheka sana tena kwa dharau nyingi.
Unacheka sana kwa dharau nyingi wakati unakaa kwenye apartment za section 8!
Acha majivuno uchwara kijana. Ujuaji mwingi Kama bukta la Yericko.
 
Unacheka sana kwa dharau nyingi wakati unakaa kwenye apartment za section 8!
Acha majivuno uchwara kijana. Ujuaji mwingi Kama bukta la Yericko.
20161204_093253.jpg

Back
Top Bottom