Trump: Biden ana matatizo ya akili

Trump: Biden ana matatizo ya akili

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Trump azungumza kwa mara ya kwanza ya vyombo vya habari baada ya kuondoka White House, asema Biden ana matatizo ya kiakili


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amevishambulia vikali vyombo vya habari katika mazungumzo yake ya kwanza na vyombo vya habari baada ya kuondoka White House akimtuhumu rais wa sasa wa nchi hiyo, Joe Biden kuwa ana matatizo ya kiakili.

Donald Trump ambaye alikuwa akizungumza na televisheni za Fox news Newsmax na OAN zinazompigia debe na kumuunga mkono, amekariri tena madai yake kuwa kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwaka jana.

Vilevile ameutaja mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa unachosha baada ya kuzuiwa kutumia mtandao huo kufuatia hujuma iliyofanywa na wafuasi wake dhidi ya majengo ya Kongresi ya Marekani mwezi uliopita ambapo watu wasiopungua 5 waliuawa katika shambulizi hilo.

Trump amesisitiza kuwa: "Biden ana matatizo ya kiakili na bado naamini kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yalichakachuliwa." Madai hayo ya Trump ya kuibiwa kura katika uchaguzi uliopita ndiyo yaliyowachochea wafuasi wake kuvamia majengo ya Kongresi ya Marekani.

Joe Biden alishinda uchaguzi wa rais wa Marekani kwa kupata kura 306 za wajumbe wa jopo maalumu Electoral College dhidi ya Trump aliyepata kura 232.
 

Wamwache mzee alale tu, anasinzia kama mugabe

Anyway kihusu tatizo la akili hili lipo wazi mbona

Anaebisha atuambie tatizo la joe Biden la kiafya ambalo ni "DIMENTIA" Je hili sio tatizo la Akili?????

Usiweke moyo kabla hujatoa jibu kwa hisia, Fikiria kwa akili, Je dimentia ni Tatizo la nini???
 
nashauri reference ya mabishano haya iwe ile mijadala yao miwili waliyoifanya wakati wa kampeni za uraisi.......wanakutanishwa mara mbili kama sikosei. je, ilikuaje? kulikuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa wa akili? km ndiyo, ilikuaje tena akaendelea kushinda?

nyongeza: kwakuwa focus ni biden basi tujikumbushe pia mijadala aliyowahi kuifanya wakati wa kutafutwa kupitishwa na chama chake.

ahsanteni
 
Kama Baideni ana matatizo ya akili basi tirampu atakuwa chizi wa kuokota makopo.
 
Yule mzima sana tu..na uzuri wake yeye sio mnafiki kama hawa akina Biden.
Yule Mzee ni mjinga sana, anapenda maashindano ya kitoto, hii hoja mbona alishaitoa WAKATI WA KAMPENI NA ILIBACKFIRE!!!!
Yeye ni ex President atulie sindano zimuingie sawasawa, One term President.
 
naona watu wengi wanachangia huu uzi bila kujiuliza kwanini trump alisema biden either ni mwongo au ana matatizo ya akili.....


majuzi akiwa town hall na cnn, biden alikaririwa akisema 'alipochukua madaraka i.e jan 20, hakukua na covid vaccine',..... cha ajabu cnn hawakumtaka afafanue na vyombo vingi vya habari vimeipotezea hii comment ya Joe!


sasa, Fox na hao wengine waliongea na Trump kwa njia ya simu, na wakataka neno lake kutokana na hiyo comment ya Biden kuhusu covid Vaccine.........!!


ndipo trump akasema huyu mtu either mwongo au ni mgonjwa wa akili, maana yeye binafsi (biden) alipokea chanjo ya covid disemba, sasa atasemaje alipoingia madarakani hakukua na chanjo?.... he is obviously mentally gone!....


mashabiki wa biden mtu mnaemtetea ni mgonjwa, achaneni na hizo blah blah
 
Sasa km raisi Ana matatizo, nchi iko salama kweli

..Marekani wana MIFUMO imara inayoweza kumsaidia Raisi wao.

..Binafsi siamini kama Marekani itaathirika kutokana na kumchagua Raisi mwenye changamoto za uzee.
 
Back
Top Bottom