Trump azidi kukataliwa

Trump azidi kukataliwa

wambeke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
2,655
Reaction score
2,650
Wakuu wa Republican wataka chama kikate udhamini kwa Trump

_90763270_735f0b6f-a0b4-4bac-8ffb-13e80a3b173f.jpg

Donald Trump anasema hajali kwamba chama cha Republican kitakata udhamini wa kampeni zake.
Zaidi ya wakuu 70 wa chama cha Republican wamesaini barua na kuituma kwa mkuu wa kamati ya kitaifa ya chama hicho wakimtaka aache kusaidia kampeni za Donald Trump.Wamesema "ubaguzi " na " uwezo mdogo" unakiweka chama katika hatari kushindwa katika uchaguzi wa Novemba.

Barua ilisema kwamba badala yake chama kinapaswa kuelekeza juhudi zake katika kuwalinda wagombea katika uchaguzi wa seneti na baraza la wawakilishi.

Wajumbe wa zamani wa baraza la Congress ni miongoni mwa wale waliosaini barua hiyo.

''Tunaamini kwamba kauli za kugawanya watu, uropokaji, ukosefu wa uwezo na kuvunja rekodi ya mgombea asiye maarufu vinaweza kuitia demokrasia hatarini ," ilieleza barua hiyo.

Akijibu kuhusu hatua ya barua hiyo , Bw Trump amesema kuwa hajali kwamba chama kinaweza kukata msaada kwake .

"kile ninachoweza kufanya ni kusitisha udhamini wangu kwa chama cha Republican " alisema bilionea huyo.

Lakini je ni yapi matumaini kwa wasiompenda Trump katika Republican?
  • Tumaini la kujiuzulu: Iwapo Trump ataamua kujiondoa mwenyewe itakua njia rahisi ya kupata mtu atakaechukua nafasi yake kama mgombea, lakini si rahisi achukue uamuzi huo .
  • Uwezekano mwingine ni kumtafuta mgombea mwingine: Bila Bw Trump kuondoka kwenye kinyang'anyiro hicho, kumuweka mtu mwingine haiwezekani chini ya sheria za chama.Baadhi wanafikiria kumuidhinisha mgomea mwenye msimamo huru Gary Johnson, lakini hili linaweza kuleta mgawanyiko wa kura za chama.
  • Suala jingine ni kumlazimisha aondoke kwa kutumia sheria ya siri: baadhi wanafikiria kumtangaza Bwa Trump "kama mtu mwenye matatizo ya kiakili ", chini ya kanuni ya kamati ya kitaifa ya Republican ambayo haijawahi kutumiwa.Lakini hii itakua hatua ngumu kwasababu huwezi kumuita mtu aliechaguliwa na watu zaidi ya milioni 10 asiye na uwezo wa kiakili.
  • Kukaa na kusubiri: Baadhi ya wanachama wa Republican ambao hawajaathiriwa wanadhani njia bora tu ni kumpinga Bw Trump na kusubiri watakapopata mgombea bora.
 
Japo simsupport Trump kunafigisufigisu nyingine either zimeongezewa chumvi ama Baadhi ya Republicans wamekosa busara..
At this stage,kumtoa Trump haitasaidia hata kidogo.Bado wako kwenye lose-lose situation tu.
 
Hawakuanza Leo kumkataa, walishayafanya yote hayo usiku huku mchana wakijidai wapo Neutral, sasa wameanza kuyafanya mchana, wamejichoresha na kila mtu anawajua.
Ni kama vile wanazidi kumnadi tu.
 
Japo simsupport Trump kunavigisuvigisu nyingine either zimeongezewa chumvi ama Baadhi ya Republicans wamekosa busara..
At this stage,kumtoa Trump haitasaidia hata kidogo.Bado wako kwenye lose-lose situation tu.
Naona wako kwenye totally lose! ....hakuna njia ya kutokea
 
Kama ameweza kusema kuwa Barack Obama na Bi Clinton ndyo founder wa Islamic state atakuwa mzima kweli.
Huo ndiyo ukweli, unadhani John McCain alikua aki engineer hilo suala kwa msaada kutoka wapi?
 
Huo ndiyo ukweli, unadhani John McCain alikua aki engineer hilo suala kwa msaada kutoka wapi?
sasa mbona anaipinga kauli yeke mwenyewe anasema ulikuwa ni mzaha na kuilaumu CNN, Mbona amekuwa mtu ambaye hana msimamo yaani anabadilikabadlika
 
Kama ameweza kusema kuwa Barack Obama na Bi Clinton ndyo founder wa Islamic state atakuwa mzima kweli.
kwani unafikiri ni uwongo , huo ni ukweli mtupu, nilikuwa simpendi trump, lakini sasahivi nampenda baada ya kumuelewa, issue ambayo sio sawa ni ile ya kutaka kuwazuia waislam ambayo sasivi amelegeza msimamo
 
sasa mbona anaipinga kauli yeke mwenyewe anasema ulikuwa ni mzaha na kuilaumu CNN, Mbona amekuwa mtu ambaye hana msimamo yaani anabadilikabadlika
Hapo ametetea USA interest tu,lakini ukweli ndio huo
 
Japo simsupport Trump kunafigisufigisu nyingine either zimeongezewa chumvi ama Baadhi ya Republicans wamekosa busara..
At this stage,kumtoa Trump haitasaidia hata kidogo.Bado wako kwenye lose-lose situation tu.
Trust me hakuna chumvi. Jamaa ni tapeli, incompetent, a liar and a loud know-nothing. Many of us have pointed this out since last year.
 
Mie Siipendi America ndio sababu tangu awali nampenda Trump
I am not too sure huipendi Marekani halafu unampenda Trump kwa sababu gani. I suspect it has to do with one story. You liked one story about Trump.You are completely oblivious of everything else that is so despicable about Trump.
 
Kama ameweza kusema kuwa Barack Obama na Bi Clinton ndyo founder wa Islamic state atakuwa mzima kweli.
Kasema ukweli, sasa cha ajabu hapo ni nini?. Siku zote msema kweli huchukua na watu wengi hass wale wenye maslai na ule ukweli!
 
Back
Top Bottom