Trump awachana maglobalist- "there is no such thing as global flag"!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,817
D.Trump amezidi kuwathibitishia ma-anti christ na ma-globalist kwamba yeye yuko kwa ajili ya USA na siyo Dunia yote, yeye siyo raisi wa Dunia bali ni raisi wa USA, hivyo hakuna tena kutuma Majeshi ya USA kuvamia nchi nyingine bila ya sababu kwa manufaa ya wachache, muda wa USA kuwa Askari wa Dunia umekwisha, alitoa maneno hayo kwenye Mkutano wa CPAC (The conservative Political Action Conference)!

,,There is no such thing as a global flag, a global anthem, or a global flag,” he said. I’m not representing the globe. I’m representing your country.
We have to, to turn things around. The era of empty talk is over, It’s over. Now is the time for action.” - D.Trump!

Wananchi wakimkatiza na kuimba USA, USA, USA!
 
Yuko sawa kabisa katika uamuzi wake huo. Amerika first.
Hope nasi waafrika tutaangalia MASLAHI ya nchi kwanza.!
 
Daesh na ISIS kwisha habari yao,
Sina uhakika na Israel maana hao atawalinda tu ila kwa dau kubwa sana.

Kuhusu Saudi mmmh kwa mafuta sidhani
 
D.Trump amezidi kuwathibitishia ma-anti christ na ma-globalist kwamba yeye yuko kwa ajili ya USA na siyo Dunia yote, yeye siyo raisi wa Dunia bali ni raisi wa USA, hivyo hakuna tena kutuma Majeshi ya USA kuvamia nchi nyingine bila ya sababu kwa manufaa ya wachache, muda wa USA kuwa Askari wa Dunia umekwisha, alitoa maneno hayo kwenye Mkutano wa CPAC (The conservative Political Action Conference)!

,,There is no such thing as a global flag, a global anthem, or a global flag,” he said. I’m not representing the globe. I’m representing your country.
We have to, to turn things around. The era of empty talk is over, It’s over. Now is the time for action.” - D.Trump!

Wananchi wakimkatiza na kuimba USA, USA, USA!

Ni vigumu sana kumwelewa Donald Trump ikiwa hutaenda ndani zaidi katika mawazo yao khasa ukizingatia kwamba Trump anawawakilisha wahafidhina wa Marekani yaani conservatives watu wenye msimamo wa mlengo wa kulia.

Ukiacha haya anayoyasema Donald Trump unatakiwa uwe unamsikiliza mkuu wa mikakati wa Ikulu ya Marekani bwana Stephen Bannon ambae ndiye alie nyuma ya mipango na sera za serikali ya raisi Donald Trump.

Stephen Bannon akiongea kabla ya raisi Trump kutoa hiyo hotuba alisema kwamba, wanaazimia kuunda upya utawala ya nchi, akimaanisha kwamba wanavunja mipango yote ya kijamii ukiwemo mpango wa "Obama Care ambao tayari umekwenda na maji pamoja na kurekebisha sera na sharia nyingi za serikali ambazo zilikuwa ama zinawafaidia watu wasio raia wa Marekani au wale wenye kufaidika na mfumo wa kifisadi ulokuwa ukiratibiwa na chama cha Democrats.

Lakini haya yote yanaambatana na uwepo wa nchi ya kipolisi ambayo inaendesha uchumi ambao unaamuru na kutoa maamuzi ambayo yana maslahi kwa Marekani pekee.

Pia pamoja na kuzuiwa na mahakama kujaribu kuwazuia raia wa kutoka nchi saba za kiarabu, raisi Trump ameapa kuendelea na mpango mpya wa kudhibiti wahamiaji wa kutoka katika nchi saba za kiislam.

Pia tunaona jinsi anavyotumia madaraka yake kujaribu kuwatafuta wahamiaji waso na hati za kuishi nchini huo ambao hapo awali waliruhusiwa na serikali ya Obama kuendelea na harakati za kuhalalisha hati zao za kuishi nchini humo kwa masharti kwamba hawana historia ya uhalifu.

Halikadhalika, umemsikia akisema jinsi alivyopania kuunda upya jeshi la nchi hiyo ambalo litakuwa imara kiasi cha kuweza kupambana na yoyote yule akiwalenga maadui wa ISIS ambao haya hivyo bado wanashughulikiwa hivi sasa huko Mosul nchini Irak.

Hivyo basi ukihitimisha kinachoendelea utaona kwamba Serikali ya raisi Donald Trump inazingatia utaifa kwanza, jambo ambalo si baya lakini nyuma yake kuna nia mbaya kabisa ya kuelekeza hasira ya wamarekani wenye msimamo mkali ambao wamedhamiria kuwaadhibu wafuasi wote wa ulokuwa utawala wa Obama na kuwasaka raia wote waso na hati halali za kuishi nchini humo, kisha kuwa tayari kuendeleza vita mahali popote pale duniani (zingatia maonyo kwa Iran na Korea Kaskazini) na kukandamiza haki za kimsingi za raia wa Marekani.

Na hiyo ni hatari sana kwa nchi kama Marekani.
 
Kwa wasiojua World History ndio wanaweza kushangilia misimamo kama hii ya kina Trump , nationalism siku zote inaishia kwenye majanga , someni world war 1 & 2 zilianzaje labda mtaelewa
 
Kwa wasiojua World History ndio wanaweza kushangilia misimamo kama hii ya kina Trump , nationalism siku zote inaishia kwenye majanga , someni world war 1 & 2 zilianzaje labda mtaelewa
Mkuu Koba pia usisahau kwamba Historia ya dunia inatufundisha kwamba huwezi kujenga taifa lolote imara bila kuwa na hisia za utaifa. (Nationalism). Hata Marekani, Uingereza, Uchina na Urusi yamejengwa juu ya misingi ya hisia za Utaifa (Nationalism)

Nikukumbushe jambo la mwisho ambalo najua litakuingia kichwani vizuri. Huku Afrika tuliweza kuutoa Ukoloni na kuwa mataifa huru kwasababu ya hisia za Utaifa (Nationalism) zilizojengwa kwa waasisi, wetu.
 
Ntamuelewa sana sana kama akikata misaada yote kwenda afrika ili viongozi waanze kufikiria nje ya box

Misaada ndio chanzo cha kudumaza akili
 
Back
Top Bottom