Trump alipa dola milioni 25 kumaliza kesi

Trump alipa dola milioni 25 kumaliza kesi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
ZAS.jpg
​

Wakili wa rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.

Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika chuo kikuu cha Trump,ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji

Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni ishirini na tano ili kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa.

Chanzo: BBC
 
Alituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake, jibu alilolitoa lilinifanya nimkubali zaidi, alisema yeye ni mjanja kuliko wakusanya kodi ndio maana hakulipa!

Huyo ndio rais wa Marekani, na amechaguliwa..hapo awali nilijua kulipa kodi ni ujanja, kumbe ni ujinga
Jpm atamtumbua huyo
 
Back
Top Bottom