Trump afurahishwa na hatua ya Korea Kaskazini na Kusini kukubaliana kuimarisha amani Rasi ya Korea

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Nchi za Korea kuifanya rasi ya Korea kuwa eneo la

Rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wawili wa Korea katika mkutano uliofanyika mjini Pyongyang.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alitangaza kuwa nchi yake itaacha mpango wake wa zana za kinuklia.Trump amesema mambo yalikuwa mazuri.
''Tumepiga hatua nzuri kuhusu Korea kaskazini. Awali kabla ya kuwa rais ilionekana kana kwamba tutaingia vitani na Korea Kaskazini na sasa tumepiga hatua sana.
Tumerejeshewa wafungwa wetu, tunarejeshewa mabaki ya wapiganaji wetu,lakini la muhimu hakuna tena majaribio ya makombora, majaribio ya silaha za nuklia. Sasa wanataka kuomba kuhodhi mashindano ya olimpiki, sasa tuna mambo mengi mazuri yanayoendelea,'' alieleza.

Trump amerejelea kauli yake kuwa utawala wake umekuwa chachu ya kuleta mazingira tulivu yanayoonekana sasa.
''Kumbuka hili, kabla ya kuwa rais watu wengi walifikiri kuwa tunakwenda vitani lakini sasa mahusiano mazuri yamejengwa, nawaambia kwa mawazo yangu, mahusiano ni mazuri, hali imekuwa ya utulivu, kwa sasa tunapoongea hali imetulia, amekuwa mtulivu, nimekuwa mtulivu hivyo tutaona mambo yatakavyokuwa''
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesema makubaliano hayo yanalenga kumaliza historia ya matukio ya makabiliano na kuifanya rasi ya Korea kuwa ardhi ya amani bila kuwepo kwa vitisho wala silaha silaha za nyuklia.

Bbc swahili
_103504576_korea.jpg
 
Kila la kheri, makubaliano hayo yawe ya kweli na yenye faida kwa watu wa nchi mbili hizo
 
Kim kanyooka maaaamae! Jeuri na ufedhuli mwiiingi bila akili!
 
Back
Top Bottom