True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

Asanteeee Jehovaaaaaaaa Aaaasaanteee Yehovaaaaaaa, Asante Jehovaaaaa, Asante Jehovaaaaaaaa, Asante Jehovaaaaaaaaaaaaaaaa Asante Jehovaaaa.
 
ASANTE KWA USHUHUDA UNA BAADHI WANAKUBEZA ILA SIKU ZOTE ANAYEJUA MAUMIVU YA KIDODO NI WEWE MWENYE KIDONDA HATA DAKTARI ANAYEKUTIBU HAJUI MAUMIVU UNAYOPITIA
 
ASANTE KWA USHUHUDA UNA BAADHI WANAKUBEZA ILA SIKU ZOTE ANAYEJUA MAUMIVU YA KIDODO NI WEWE MWENYE KIDONDA HATA DAKTARI ANAYEKUTIBU HAJUI MAUMIVU UNAYOPITIA
asante, sifa na utukufu kwa Mungu. hakika ninawaambieni, haya niliyoeleza yalitokea kwenye maisha yangu. wakati ule unapokuwa umetumia akili zako zote unazofiiri una uwezo, ukifika mwisho ndipo Mungu anapoanzia kufanya kazi. hakuna jambo linalomshinda Mungu, halijawahi kuwepo na halitakuja kuwepo milele. Mungu anaweza yote. Sara mke wa Ibrahim walipotembelewa na malaika, akiwa jikoni alisikia malaika (aliyetokea kwa mfano wa mwanadamu) akiwambia Ibrahim mwakani muda kama huu utakuwa na mtoto kupitia mkeo (ambaye ni kibibi), yeye akacheka. malaika alimwuliza, kuna jambo gani lililo gumu la kumshinda mungu?

"Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.'' ( Yohane 3:14-15 ) I love this song.....mtazame huyo (Yesu) aliyeangikwa juu (msalabani) hivi sasa upate ishi.

YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, KWA MUNGU YANAWEZEKANA

Hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo.

Zekaria 8:6, Bwana wa majeshi alimwambia Musa; “ingawa hili ni neon lililo gumu mbele za macho ya mabaki ya watu hawa, je, liwe neno gumu mbele za macho yangu? Hata kama jambo ni gumu na linaonekaka kama halitawezekana mbele za macho yetu sisi wanadamu, Mungu wa Ibrahim Isaack na Yakobo, yaani Mungu wa Israel, anaweza yote. hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wetu.


Mwanzo 18:14, Bwana alimwambia Sara mke wa Ibrahimu kuwa, Jambo gani lililo gumu linalomshinda Bwana? Mungu wetu anaweza yote. Mungu wetu ana nguvu, ni mkuu ni unique, na anaweza mambo yote. hafananishwi na chochote, hashindani na chochote wala yoyote, ni mkuu mno, nguvu zake hazichunguziki, mawazo yake hayachunguziki, na njia zake hazichunguziki.


Hesabu 11:23, Bwana Mungu wetu alimwambia Musa, Je, mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako au la. (Soma mpaka isaya 59:1, kuwa mkono wa bwana si mfupi hata usiweze kuokoa….sikio lake si zito lisiweze kusikia, ila maovu yetu ndo kikwazo…., pamoja na yote hayo, hapa, Mungu alitaka kumwonyesha Musa kuwa hakuna jambo lililo gumu kwake.


Ayubu 42:2, Neno la Bwana kwa kinywa cha Ayubu linasema”najua ya kwamba waweza kufanya mambo yote, na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuiliwa. Hakuna mtu wala kitu chochote kinachoweza kumzuia Mungu kufanya atakacho. Mungu akisema ndiyo hakuna mtu wa kusema hapana, na akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo.


Luka 1:37, Malaika alimwambia mariam kuwa, hakuna Neno lisilowezekana kwa Mungu. Kwa Mungu wa ibrahim isaka na Yakobo, Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi na vyote vijazavyo, anaweza yote.


Yeremia 32:17, Neno la Bwan alinasema “Aa! Bwana Mungu tazama wewe umeziumba mbingu na nchi kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa, hapana neno gumu usiloliweza.


Efeso 3 :20, Neno la Mungu linasema, Basi, atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Mungu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko yale tuliyowahi kuyaona,kuyaomba au kuyawaza. Mungu aweza kufanya mambo makubwa sana na ya ajabu.


Mathayo 19 :26, Yesu akawakazi macho akawaambia « kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa Mungu yote yanawezekana. ». Yesu mwenyewe ndiye alitoa ahadi na ufafanuzi huu hapa kuwa, kwa Mungu yote yanawezekana. Hivyo, hakuna sababu ya kuwa na hofu tumwombapo Mungu, tunajua kuwa Mungu ano uwezo wa kufanya mambo yote hata yale ambayo sisi tunayaona kama magumu sana.


Marko 10 :27, Yesu akawakazi macho akasema, « kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo, maana yote yanawezekana kwa Mungu ». Hakuna jambo liwalo lote lile ambalo Mungu linamshinda. Hakuna.
 
Nikupe pole sana Azusa street, kila jambo lina ukomo na hakuna mapito yasio na mwisho, ni vyema sana Mungu amekutendea yale makuu, usiache kumshukuru kila leo, jivunie hivyo hivyo na Mungu ndipo atazidi kukuinua.... Mungu utenda miujiza zaidi kwa wale wanaoamini na kushukuru zaidi... Wenye macho basi waone miujiza ya Mungu...
 
Nikupe pole sana Azusa street, kila jambo lina ukomo na hakuna mapito yasio na mwisho, ni vyema sana Mungu amekutendea yale makuu, usiache kumshukuru kila leo, jivunie hivyo hivyo na Mungu ndipo atazidi kukuinua.... Mungu utenda miujiza zaidi kwa wale wanaoamini na kushukuru zaidi... Wenye macho basi waone miujiza ya Mungu...
 
Azusa Street mbona sasa kuna post huwa unatukana, au upako unakua umeyumba?
 
Nikupe pole sana Azusa street, kila jambo lina ukomo na hakuna mapito yasio na mwisho, ni vyema sana Mungu amekutendea yale makuu, usiache kumshukuru kila leo, jivunie hivyo hivyo na Mungu ndipo atazidi kukuinua.... Mungu utenda miujiza zaidi kwa wale wanaoamini na kushukuru zaidi... Wenye macho basi waone miujiza ya Mungu...
 
hamna kazi na mkeo akapata likizo!
nafikiri kwa faida yako nimefafanua. sidanganyi hii story, nisingepoteza muda kuandika yote haya. kuna mengi sijafafanua jinsi tulivyoishi, pasingetosha na wala msingeamini kama kweli tuliishi hivyo. ndani ya hayohayo matatizo, mke wangu alijiendeleza kielimu, na ujue mimi nilishakuwa na degree ndani ya matatizo hayo yote...still yalitokea hayo...kuna mengi sijaeleza..amni nilichokuambia.
 
Azusa Street mbona sasa kuna post huwa unatukana, au upako unakua umeyumba?
weka quote hata moja tu hapa niliyotukana kama ushahidi mkuu. pamoja na kwamba nakiri mimi ni mwanadamu mwenye madhaifu ninayehitaji bado msaada wa Mungu....lakini kwa hili hebu weka thread yeyote niliyotukana ili uwe ushahidi. thanks.
 
Nimepitia mengi sana, Mungu amenipitisha kwenye mambo mengi, ameniokoa na kunitoa kwenye vitu vingi. lakini kuna kitu kimojawapo kilichobadilisha kabisa mwelekeo wangu kimaisha, ni kitabu cha ISAYA 53. soma yote, ni mistari michache tu hata dakika kumi haziwezi kumalizika. ndani ya sura hiyo, kauli moja tu ambayo Mungu aliitamka nikaelewa kwamba kumbe bila Yesu Kristo, Mungu hatutambui na hataki hata kutuona? ili Mungu akubali kutuona, tunatakiwa kwenda kwa mgongo wa Yesu Kristo, hapo ndipo ameahidi atatusamehe dhambi zetu.

sio kwamba hataki kutuona kwasababu yeye anatuchukia sana, hapana! Mungu ni mtakatifu sanaaa, hakuna uchafu wowote ndani yake, utakatifu wake ni sawa na moto ulao unaozidi moto uyeyushao dhahabu na kutenganisha makapi na dhahabu halisi, hivyo uendapo kwa Mungu kama una dhambi akikusogelea unaweza kuteketea kabisa kwasababu yeye ni moto ulao. ndio maana hakuwashukia waisrael hadi alipowaambia wajitakase kwanza. wakaomba na kufunga, wakakaa mbali na wake zao (hii ni fundisho, hata wewe ukitaka kufanya maombi ya kufunga, kaa mbali na mkeo, nafikiri ukiwa unalala naye akili yako huwa kwake zaidi zaidi ya kuwa kwa Mungu, hivyo hautajimimina absolutely kwa Mungu)......

Isaya 53, kuna mstari ulinichoma anaposema "and for his sake, I will forgive their sins"...kumbe God forgives our sins just for the sake of his servant Jesus Christ?....na hii ndio siri kubwa ambayo wengi hata walipoambia hawakuiamini, kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu Yesu azaliwe na aishi maisha ya aina ile, ateswe na kumwaga damu namna ile, siku ya tatu afufuke namna ile, ......ukimwambia Mungu, ukimkumbusha Mungu kwamba, Mungu akumbuke jinsi Yesu alivyomwaga damu yake, aikumbuke ile damu ashuke kukusamehe, na uingie kwenye agano naye, agano la damu ya Yesu awe Mungu wako na wewe uwe mtoto wake, yeye ashughulike na mambo yako na wewe umtumikie, kwasababu Mungu ni Mungu wa maagano, na kwenye agano la Damu hasa ya Yesu huwa hakwepeshi.....utaona maisha yako yatakavyobadilika. HIVYO NDIVYO nilivyopata siri ya namna gani kusogea mbele za Mungu.

Kusogea mbele za Mungu sio kwa utani utani kama vile Mungu ni binamu yako....lazima uende kwa unyenyekevu wa hali ya juu, uende ukiwa na moyo uliopondeka, kamwe usijihesabie haki usogeapo mbele za Mungu, mwambie Mungu mimi ni mwenye dhambi tu na ninasogea kwako kwa kupitia Yesu Kristo tu (asingekuwa Yesu nisingesogea kabisa), tunafanya dhambi sana kwa mawazo, maneno, matendo kwa kujua hata kwa kutokujua....Yesu alitoa mfano wa msomi wa dini aliyesimama akasema "Mungu, angalia mimi natoa sadaka, nafanya haya na haya, sio kama yule....etc", mtoza ushuru mmoja (kama sikosei) akasimama, hata mbinguni hakutazama, akajipiga kifuani na kusema "Eee Mungu nisamehe mimi ni mwenye dhambi"....Yesu alisema huyo wa pili ambaye hakujihesabia haki ndiye aliyeenda nyumbani akiwa justified (amesamehewa dhambi kabisa). Mungu anataka twende kwa unyenyekevu mbele zake, na kila unachofanya, iwe kwenye kuimba, kufanya maombi, fanya kwa njia ya Yesu Kristo ukijua ya kwamba Mungu hawezi kukupokea kama hautaenda kwake kwa njia ya Yesu Kristo. mwenye masikio na asikie neno hili.
 
MUNGU MUNGU MUNGU MUNGU MUNGU..................
Kwenye kila mafanikio ya mtu nyuma yake yupo MUNGU.

Kazi ya shetani ni kulaghai nankudanganya watu so mkimbieni shetani.
 
imani yenye wokovu ni imani ya Kilokole tu, .

Huu ni uongo mtupu, imani yoyote inayotanguliza tu-miujiza-miujiza kama hiyo ya kwako siyo imani dhabiti na ni imani ya uongo. Ukisoma Mathayo 16:21-26 hata Yesu alikataa mambo ya kujitia ujinga kwamba ukiwa mfuasi wake basi huwezi kupatwa na taabu za hapa duniani. Inaonyesha wazi wewe shida yako ni faraja za kidunia kama watoto, mali n.k ndiyo maana umekuwa ukihama-hama madhehebu/makanisa. Yaani ni kama unamlazimisha Mungu ajibu hayo maombi yako na usipojibiwa unavyotaka imani yako kwa Mungu inapungua/inaisha!! Hii imani yako haina tofauti na wanaofanya ushirikina maana wao utafuta kwa kubadiri waganga mbalimbali mpaka wapate mganga atakayewapatia wanachotaka (mara nyingi mali, watoto au tiba yaani exactly kama yale uliyoyaandika kwenye hadithi yako). Hivyo, Imani ya kweli ni pale utakapo kubali ya kuwa katika hali yoyote ile iwe ya taabu na dhiki (umasikini, ugonjwa, n.k) au faraja (amani, ukwasi, n.k.) Mungu ataendelea kuwa Mungu na watu waambiwe ukweli ya kuwa hapa duniani kuna kupata na kupatwa hata kama ni mfuasi mwaminifu wa Mungu kupitia Yesu. Na siyo hayo majina mnayojibatiza ya ulokole na kuanza kuwadanganya watu eti wakijiunga na imani yenu basi shida zao zitaisha - dhubutu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…