john agrey
JF-Expert Member
- Jan 24, 2015
- 1,280
- 2,080
Leo naomba niwape kiufupi stori ya kweli iliyonikuta kwa takribani miaka minne hivi.
Nilipokuwa kidato cha sita mwaka 2012 nilitokea kukutana na binti mmoja anaitwa Sophia. (Si jina lake ila nimeona nitumie hili). Baada ya kukutana tulikuwa na mazoea mengi sana maana alikuwa anaishi dar na mimi naishi dar, Sophia alikuwa ni mtoto wa mke mdogo kwa baba yake so mara nyingi aliishi na mama yake. Baada ya kuingia kidato cha sita yeye alianza kidato cha tano shule moja ipo Moshi, tuliendelea kuwasiliana na baadae niliamua kuanzisha nae mahusiano kwa maana ya mapenzi.
Sophia hakukataa maana hadi hapo tulikuwa kama na mwaka hivi na zaidi hivyo kidogo alinifahamu mimi ni mtu wa namna gani, tulipokuwa likizo tulikuwa tunatembeleana na mimi kaka yangu alifahamu kuwa nina mahusiano nae. Baada ya mda mama mama ake sophia aligundua kuwa mwanae anamahusiano na mwanaume alichokifanya alimuita na kumuuliza, Sophia alikubali kuwa ni kweli anamahusiano na Mimi, mama hakuonesha kama ni jambo baya licha ya kuwa tulikuwa dini tofauti, sophia alikuwa mtoto wa shekhe. Hapo kati mama alimpa taarifa baba ake Sophia, baba alikuwa mkali haswaaa maana alikataa binti ake kuwa na mahusiano na kafir, alimpiga sana binti yake, na akaanza kumlinda kila akirudi likizo, Sophia hakuruhusiwa kuwa na simu, wala kuondoka nyumbani kwao peke ake. Mambo yalikuwa magumu sana, tulionana kiwizi wizi tu baadae nikamnunulia simu tukawa tunawasiliana napo kwa kificho. Nilipomaliza kidato cha sita yeye ndio alikuwa anaingia, mimi niliendelea kuwasiliana nae akiwa shule licha ya kuwa hawakuruhusiwa kuwa na simu shuleni kwao.
Mwaka huo kwake ulikuwa mgumu sana wakati yupo likizo baba ake alikuwa bado anamsimamo ule ule, Sophia alikuwa anapigwa haswa na baba ake kisa Mimi, ikafika kipindi akagoma hadi kula, mama ake akawa anambembeleza aachane na mimi ila yeye hakutaka. Waliposhindwa kumshawishi binti yao wakaanza kunitafuta Mimi sasa, walinitishia sana hasa baba ake kuwa akiniona na mwanae ataniua, mi nikaona isiwe tabu nikaongea na mama ake sophia kwa kirefu na yeye hakuwa na shida.
Mda ulienda nikachaguliwa chuoni mkoa mmoja na anakosoma sophia, mapenzi yakazidi sana. Mara ya kwanza Sophia alikuja nilipokuwa nimepanga, na bahati mbaya tuliishia kufanya mapenzi na kumbe alikuwa bikra. Baada ya hapo alienda shule. Baba ake sophia alipata taarifa kuwa nasoma chuo kimoja na mwanae, alikuwa ananitishia mi nikawa nampuuza tu, baadae mwezi wa kumi na mbili nliona hali imekuwa mbaya maana baada ya baba ake kunitishia kunifunga na akawa ananitafuta kupitia uongozi wa chuo. Mimi nikaongea na mama ake Sophia kuwa asiwe na shaka mi nitaachana na mwanae. Ukweli tulikuwa tunapendana sana na sophia, nlitafuta namna nitakavomuambia nikatafuta njia nikutane nae likizo ya christmass nikakosa. Ilikuwa siku ya mkesha nikamwambia aombe ruhusa kwa mama ake (kumbuka yeye ni muislam hapo) mama akamkubalia wakaja na mdogo ake hadi kanisani. Wakati watu wakiendelea na nyimbo huko nikaamua nimwambie ukweli kuwa naomba uhusiano wetu uishie hapo, Sophia hakuweza kunijibu, kumbe alipoteza fahamu (alizimia).
Nilichanganyikiwa.................itaendelea