Kuna njia nyingi za kuondoa ushahidi baada ya kufanya mauaji. Unaweza kujaribu kuchoma mwili kama Angela Simpson, kuutupa au kuuficha kama Ted Bundy alivyofanya.
Dayna Jennings aliamua kuupgrade alichofanya Ted Bundy: kuuficha mwili ila ndani ya nyumba hiyo hiyo anayoishi.
Mwili ulikuwa wa William Mussack, baba wa Dayna, waliishi wote Federal Heights, Colorado, Marekani.
Dayna Jennings
Desemba 7, 2017, William alimtumia ujumbe mwanawe Brian. Alimweleza kuwa alikuwa na wasiwasi kwamba Dayna alikuwa amempa dawa za kumlewesha. Alisema baada ya kutafuna hamburger aliyopewa na binti yake, alijikuta amelala kwa takribani saa 15. Alipoamka, hamburger ile ilikuwa bado pale pale, ikiwa na alama ya kutafunwa mara moja tu.
William 'Bill' Mussack na binti yake
Mwishoni mwa Novemba 2017, Dayna alikuwa anatafuta taarifa kuhusu dawa iitwayo Acepromazine. Dawa maalumu ya kuwapa usingizi mifugo haswa farasi. Aliporidhishwa na taarifa alizopata akaiagiza dawa hiyo kupitia eBay.
Desemba 9, mwaka huo huo, aliingia Google akawa anauliza ni muda gani mwili wa binadamu huoza baada ya kufariki.
Ujumbe ambao Bill alimtumia Brian, haukumshtua sana Brian kwakua hata hakufikiria kwamba huo ungekuwa ujumbe wa mwisho kuuona kutoka kwa baba yake.
Baada ya huo ujumbe, Bill hakuwasiliana tena na ndugu wala marafiki. Familia ilianza kuwa na wasiwasi. Desemba 28, 2017, taarifa ya kupotea kwake ikafikishwa polisi.
Lakini Dayna alikuwa na maelezo yake. Aliwaambia watu kwamba baba yake alikuwa ameenda kutembea milimani na mpenzi wake Martha.
Martha akasema hajamuona Bill kwa muda mkubwa sana.
Dayna akasema anachat na baba yake na alimuambia hivyo.
Askari walivyotrace minara wakakuta simu ya Bill haijawahi kutoka hata nje ya mlango tangu mwezi uanze.
Zaidi ya Dayna hakuna mtu mwingine aliyekuwa amemwona William tangu mwanzoni mwa mwezi huo.
Polisi wakaanza kufuatilia, wakakuta Dayna alikuwa ameagiza makontena mawili ya kutupia taka. Alikuwa amenunua mifuko ya simenti, huku sakafu na zulia la sehemu ya chini ya nyumba vikiondolewa na kutupwa.
Na kuna jambo lingine, muda wote wanahangaika kumtafuta Bill akaunti yake ya benki ilikuwa inaendelea kutumika, lakini miamala mingi ilikuwa ikihusishwa na Dayna kwakua sahihi zilikua tofauti na za Bill.
Walipofika nyumbani kwa Dayna walikumbana na harufu kali na Dayna akasema choo kilikua kimeziba ndiyo sababu harufu ilikua kali.
Askari wakawa wana hii harufu kali pale nyumbani, miamala ya benki isiyo na sahihi za mhusika na binti mwenye stori mbalimbali juu ya alipo baba yake.
Januari 10, 2018, polisi wakapambania kibali cha kupekua nyumba. Walipoingia, wakakutana na harufu ileile uchunguzi uliwaelekeza kwenye sehemu ya chini ya nyumba, kwenye eneo la crawl space. Hapo wakakutana na zege lilionesha kua ni jipya na hata kukandamizwa kwake ni kama ulitumika mguu zaidi.
Walipoanza kulivunja, cha kwanza kukutana nacho ulikua mkono wa binadamu.
Wakaufukua mwili wa Bill ukaenda kufanyiwa uchunguzi.
Majibu yakaonyesha alikuwa amemeza sumu ya acepromazine. Dawa hiyo hupunguza nguvu za mfumo wa fahamu na hupelekea mtu ashindwe kuhema.
Ule ujumbe aliomtumia Brian kuhusu kulala kwa saa 15 baada ya kula hamburger ukaanza kuonekana kwa namna tofauti sasa.
Walipokagu simu ya Dayna kwa kuingia Google, wakapata utafutaji wa mtandaoni wa zile searches za hovyo.
Dayna alikiri kwamba yeye ndiye aliyemimina zege kwenye sehemu ambayo waliukuta mwili wa baba yake. Mwaka 2019, akafikishwa mahakamani. Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa sumu, biashara yake kufa mpaka kuomba hifadhi nyumbani kwa baba yake, ununuzi wa simenti, makontena ya taka na taarifa zilizopatikana kwenye simu yake.
Pia walionyesha ujumbe aliomtumia rafiki yake siku 11 baada ya kifo cha baba yake, akisema: “Maisha yamebadilika, siku hizi nabonda na kunyonga.”
Julai 15, 2019, jury ilimpata na hatia ya mauaji na kuficha mwili wa marehemu. Agosti 19, akahukumiwa kifungo cha maisha pamoja na miaka sita kwa makosa mengine.
Lakini kesi hii haikuishia hapo.
Mwaka 2023, Mahakama ya Rufani ya Colorado ilibatilisha hukumu yake na kuamuru kesi irudi kwa ajili ya kusikilizwa upya. Sababu haikuwa kwamba mahakama ilitangaza Dayna hana hatia. Iligundua kuwa kibali cha kwanza cha polisi kupekua data za simu yake hakikusema wanapekua nini.
Hivyo kilikiuka masharti ya Katiba kuhusu upekuzi.
Kwa maana hiyo, ushahidi uliopatikana kupitia upekuzi huo ulikua kinyume na sheria, na kwakua ushahidi ulipatikana kinyume na sheria na ulitumika kumhukumu Dayna basi na hukumu haipo sahihi.
Hivyo hukumu ya 2019 ilibatilishwa na shauri likatakiwa kusikilizwa upya.
Now sijatafuta nini kimetokea kwenye hii ishu mpya na sina huo mpango but for now ishi humo.