Trucking business | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trucking business

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Enny, Jan 15, 2010.

 1. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Habari wana jamii forum. Kuna mzee mmoja nafahamiana naye siku nyingi anataka kuingia kwenye biashara ya usafirishaji (malori). Kwa vile sina ajira kwa sasa ameniomba nimsaidie kusimamia biashara yake hiyo lakini mimi sina uzoefu kwenye hiyo biashara, ingawa nimesomea masomo ya biashara.

  Kama kuna mtu anaweza kunipa ideas jinsi ya kuendesha biashara ya malori na market yake kubwa ipo wapi? naomba mnisaidie, ili ajira yangu iweze kusimama vizuri ndugu zangu.

  Asante
   
 2. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Biashara ya malori kwa sasa transit goods zinalipa sana especially kuelekea Congo (Lubumbashi),Zambia,Rwanda,Burundi na Malawi.

  Unahitajika kujenga uhusiano mzuri na clearing agents, unaweza kupata contacts zao kutoka kwenye website ya TRA. Fanya mawasiliano nao either by visiting them and make your company known to them.

  Fanya research ya kutosha kuhusu yafuatayo
  .Bei za kusafirishia mizigo kwenda destination mbalimbali
  .Bai na suppliers wa inputs kama matairi na vipuri
  .Madereva wazuri na waaminifu na uwalipe vizuri
  .Gari gani zinahitajika sana,box body au za kubeba container?
  .Angalia washindani wako wakubwa katika biashara na athari zao kwa biashara yako.
  .Mafundi ambao ni full time kwa ajili ya magari yako  Faida ya biashara hii ni kubwa lakini inahitaji involvement ya hali ya juu. Unatakiwa ufuatilie kila details kwa sababu unaweza ukajikuta unawafanyia biashara madereva wako,especially mafuta wanauza sana njiani.

  Ikiwezekana safiri na magari yako angalau kila route mara moja ili ujue ni kiasi hali halisi ya barabarani kwa sababu umesema hujawahi kuwa katika biashara hii.  KILA LAHERI MKUU
   
 3. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Asante sana kwa maelezo yako mazuri angalau umenipa mwanga wapi pa kuanzia.
   
Loading...