TRL yaanzisha treni ya stesheni hadi Pugu

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,450
5,792
Gazeti la nipashe linaripoti kuwa TRL wameanzisha treni ya Stesheni hapi pungu..Nadhani hii itasaidia kupunguza shida kwa wasafiri wa Dar Es Salaam

=======

TRL yaanzisha treni Stesheni hadi Pugu

KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL), imeanzisha treni ya pili ya usafiri jijini Dar es Salaam maarufu kama 'treni ya Mwakyembe' itakayoanza kazi keshokutwa(Agosti Mosi mwaka huu), ambayo itafanya safari zake kuanzia kituo kikuu cha Stesheni hadi Pugu .

TRL.JPG

Treni hiyo itakuwa ikipita katika vituo 10 ikiwamo Kamata, Mwisho wa Lami, Vingunguti, Gongo la Mboto, FFU Mombasa, Banana pamoja na Karakata.

Aidha kuongezwa kwa usafiri huo, kumesababisha mabadiliko ya ratiba ya treni kutoka Dar es Salaam kwenda bara, kuanzia Agosti 2 mwaka huu kwani itaanza safari zake kuanzia saa 9 alasiri badala ya saa 11 jioni kama ilivyokuwa awali.

Ofisa Uhusiano wa TRL, Masanja Kadogosa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kwamba treni hiyo ya pili imeongezwa ili kuboresha huduma ya usafiri kwa wakazi jijini.

"Ujio wa treni ya pili (treni ya Mwakyembe) itakayoanza Agosti Mosi mwaka huu umeleta mabadiliko ya treni iendayo bara, kutoka hapa Dar kwenda Kigoma au Mwanza, itakuwa inaanza safari jijini Dar es Salaam saa 9 alasiri tofauti na awali ilikuwa ikitoka saa 11 jioni," alisema Kadogosa.

Alisema treni hiyo ya Mwakyembe, itasafiri umbali wa kilomita 20 kwa dakika 32, kutoka Stesheni hadi Pugu na itatoza nauli ya Sh. 600 kwa kila abiria na kwamba kwa sasa itaanza na mabehewa saba na iwapo mahitaji yataongezeka mabehewa yataongezwa na kufikia 10.

Chanzo: Nipashe
 
Itapunguza foleni ya treni ya awali manake ilikua inajaza balaaa!
 
Safi sana.naomba nimpongeze kadogosa kwa kuwa creative.hatua hii ni ya kuunga mkono kwa wote wanaopenda maendeleo.tuaomba aanzishe pia express tren kwenda mwanza angalau masaa 24 kila siku ili tuachane na mabasi yanayosababisha ajali.thanks and keep it up
 
Naomba kujua ratiba ya treni kwenda mwanza.inaondoka siku gani na muda gani.inachukua muda gani.nauli ikoje.kuna mipango gani ya maboresho baada ya kupata co mpya ambae anaonekana very creative and innovative.let give him support
 
jana nimekutana nayo pale goms ikipakia abiria bure tu kwenda pugu na kurudi.
 
Back
Top Bottom