Behewa 5 zimeharibika kufuatia TRL kufanya safari zake mara moja kwa wiki ambapo inasababishwa na abiria wengi kubeba mizigo mingi kupita kiasi. Inakadiliwa kuwa kufuatia safari na mabehewa kupunguzwa, kila abiria anabeba mara tano ya uzito unaotakiwa. Kwa kawaida kila abiria anaruhusiwa kubeba kati ya kilo 40 na 70 kufuatia daraja analosafiria. Abiria wanaofanya safari zao kati ya Dar na Kigoma wamaiomba serikali kuongeza mabehewa. Source ITV 2000 hrs news; 17/09/2010.
Katika hali kama hii, ahadi za Kikwete za kuanzisha reli mpya zinatekelezeka? Kama jibu ni ndiyo, kwanini reli ya kati isikarabatiwe ikawa bora na abiria wakasafiri kama binadamu badala ya kusafirishwa kama mizigo katika mabehewa mabovu? Karibu kuchangia.