UZINDUZI wa safari za treni ya abiria jijini la Dar es Salaam, nusura uingie dosari jana wakati kibaka aliyetambuliwa kwa jina la Vincent Michael alipoamua kuiba vyuma vya breki katika moja ya mabehewa yaliyoegeshwa katika kituo cha Yombo.
Tukio hilo lilifanyika muda mfupi kabla ya treni iliyombeba Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe haijafika katika kituo hicho.
Msafara wa Dk. Mwakyembe aliyeambatana na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Sumatra na wale wa Shirika la usafirishaji la Tanzania na Zambia (TAZARA), ulikuwa unarejea stesheni ya Dar es Salaam, ukitokea katika kituo cha Mwakanga nje ya jiji.
Safari hiyo ilikuwa ni baada ya Waziri Mwakyembe kuzindua usafiri wa aina hiyo kwa treni ya Shirikla la Reli nchini (TRL), uliofanyika eneo la Ubungo Maziwa.
Mmoja wa maofisa wanaolinda katika eneo hilo la Yombo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa kuwa si msemaji, alisema kuwa walimkamata kibaka huyo wakati akitekeleza uhalifu wake pasipo kuhofia athari zitakazojitokeza endapo behewa hilo lingeanza kufanya safari zake.
Kufuatia tukio hilo kibaka huyo alibebwa katika moja ya mabehewa yaliyombeba Waziri Mwakyembe na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Tazara kwa hatua zaidi.