Zekidon
JF-Expert Member
- May 29, 2013
- 1,903
- 569
Kichwa cha treni kilichokia kikienda karakana karibia na Karume jijini Dar es salaam, leo limezea kizaa zaa cha aina yake, yowe na vilio kwa abiria zaidi ya 70 waliokua ndani ya basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Mwenge na Mbagala, baada ya basi hilo kupaki katikati ya njia ya treni likisubiri foleni kama kawaida ya basi kufanya hivyo pindi kunapokua na foleni za magari maeneo ya mataa.
Kichwa hicho cha treni kilichokua kinakuja kwa mwendo wa kawaida kilikua kinaipigia honi gari hiyo iliyoshindwa kutoka katika barabara hiyo kutokana na kubanwa na magari mengine katika foleni, abiria ndani ya Basi hilo, bila kujali umri, jinsia wala utashi, iliwabidi kutumia mlango wa dharura (madirisha) ili kuokoa maisha yao, ilikua bahati kwa abiria hao, pale dereva wa treni alipofanikiwa kulisimamisha treni hilo mita chache toka lilipopaki basi hilo. Isingekua kwa mwendo wa taratibu wa treni hilo, leo vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali vya habari vingepambwa na habari nyingine mbaya.
Madereva mnapewa tahadhari ya kuacha kupaki magari katikati ya barabara za treni kuepusha majanga kama hayo.