Treni Dar-Kigoma kama Ndege

Treni Dar-Kigoma kama Ndege

Kayoka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
2,384
Reaction score
2,208
View attachment 239834View attachment 239834


Dar es Salaam. Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.

Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.

Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.

Kwa mtazamo wa haraka, mabehewa hayo yanavutia yakilinganishwa na yale ya awali yaliyokuwa yamekithiri kwa uchakavu, yaliyokuwa yamejaa mende na yenye milango na madirisha mabovu.

Mabehewa hayo yana viti vya kutosha, huduma ya intaneti, swichi za umeme za kuchajia simu na kuunganisha kompyuta na safari zake zimeongezeka kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.

Akizungumza muda mfupi kabla uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema wamelazimika kupandisha viwango vya nauli kutokana na gharama zitakazokuwa zinatumika katika uendeshaji wa treni hiyo.

"Licha ya kuongeza kidogo kiwango cha nauli, dhamira yetu ni kuwapatia abiria huduma safi na ya raha... kila msafiri atasafiri akiwa ameketi kwenye kiti chake. Hakuna abiria atakayesafiri akiwa amesimama," alisema na kuongeza:

"Treni inayozinduliwa leo inatumia mabehewa mapya 22 yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na kichwa cha treni kiliundwa upya kwenye karakana ya TRL iliyopo Morogoro mabehewa mapya yamegharimu Serikali Sh28.6 bilioni."

Kuhusu vituo vya ambavyo treni hiyo alisema itasimama kwenye vituo vikubwa ambavyo vingi ni vile vya miji, wilaya na mikoa. Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka aliwataka abiria kuwa walinzi wa treni hiyo ili kuhakikisha usafiri huo unadumu.

"Kumekuwa na tabia ya watu kujiamulia kuharibu mali za umma, ninawaomba abiria mtakaopanda treni hii muwe walinzi wa wenzenu kwa sababu baadhi ya abiria wamekuwa na tabia ya kuchora kwenye viti," alisema Dk Mwinjaka.

Mmoja wa abiria, Saida Roman alisema Serikali inahitaji kupewa pongezi kwa hatua hiyo kwani hivi sasa abiria wanaotumia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma watasafiri kwa raha tofauti na ilivyokuwa zamani.
 
Cjawahi panda ndege wala tren unanihakikishia vit vya tren viko sawa na vya ndege
 
Tunapongeza sana. Pawepo na usimamizi name ulinzi madhubuti kwani wale waliokuwa wanafaidi kwa kukosekana hali nzuri ya mabehewa watafanya mbinu kuihujumu. Kwa upande wa treni ya mizigo ulinzi uwe madhubuti zaidi kwani wamiliki was malori na mafisadi hawataacha kuihujumu. Pongezi sana Makyembe
 
Kweli kama ndege, Dar mpaka Kigoma ni masaa 30 tu! Sijui mwaka gani huu, 1935 au?
 
Serikali ati ipewe pongezi kw sababu wLigoma watasafiri masaa 30 ndani ya nchi yao hio hio
 
Dar es Salaam. Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Daaaa kweli sisi tunajikongoja wenzetu wanakimbia,btw imepunguza ugumu na uchovu wa safari uliokithiri.one step ahead hahahaaa penda thana tz yangu bana
 
Tofauti ya maasaa 6,hiyo ndio ndege????.Hiyo ndege naipa mwezi mmoja tu alafu mleta uzi uje hapa utuambie itakuwa na hali gani.Pale TRL hasa DSM pamejaa rushwa,tena rushwa ya sh.1000 tu watu wanaingia kwenye treni bila tiketi,watuwanaingia na kuku,mbuzi na kila aina ya kolokolo.
 
Masaa 30 si bora nibebe mizigo yangu nitembee kwa miguu.
kwa treni ya umeme yangekuwa masaa saba au hata kumi. unapana asubuhi jioni umefika. kama umeme tunao, tunashindwa nini?umeme wa kinyerezi ukianda wabadilishe hizo treni jamani na litajiendesha lenyewe, kwa siku moja watu wanaosafiri huko ni wengi ajabu, watapata hela nyingi sana na shirika litajiendesha lenyewe ili tuache kupanda mabasi.
 
Hili behewa uliloweka ni general ama?! Maana haiingii akilini kukaa masaa 30!!! Tena hadi first class wanaolipa hela ndefu!!
 
Hiyo ni yale wenzetu wa ulaya wamechoka wanakarabati wanatuuzia. Kule kwa ni train inatembea less than three hours katika states au miji mikubwa. Train inakimbia unafikiri inafukuza upepo na kila kitu katika station ni automatic. Anyway safari ni hatua ila wizi Tanzania wa watu wachache unaturudisha nyuma sana. Esikiroo, Richmond, EPA, etc na kuna nyingi kubwa ya hizi under carpets.
 
DSC_4908.JPG jiko la kwenye restaurant ya train
PG4A2797.jpg baadhi ya mabehewa ya daraja la tatu
 
Duh!! Masaa sate? Kwanza si wamesema hiyo Reli wanaitindua wanaweka mpya niaje tena? Hayo makitu mara ya mwisho kupanda ilikua mwaka 92 kutoka Moshi to Tanga.
 
Huyo mwenye suti na tai ndo yule mtoto wa mkulima wa kulialia aliyesemaga BVR ziko poa zitapiga kazi na kumaliza mwezi april 30 au?
 
Kwa wabongo yani baada ya mwezi muonekano wa sit utakuwa kama banda la kuku nipo apa
 
Baada ya wiki moja tu situ zote zitakatwakatwa na viwembe
 
Back
Top Bottom