TRANSPORT WOES: Police admit same crisis as military

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,087
TRANSPORT WOES: Police admit same crisis as military

-SUMATRA announcement based on bus owners’ pressure

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

POLICE authorities have echoed their military counterparts in stating that the recent announcement by transport regulators, obliging all security men and women in uniform to henceforth pay requisite fares when using public bus transport, has caught them financially unprepared.

The Director of Finance and Administration in the Tanzania Police Force, Commissioner of Police, Clodwig Mtweve, confirmed to THISDAY yesterday that the declaration by the Surface and Marine Transport Regulatory Authority (SUMATRA) could very well hit them (police) as hard as the Tanzania People�s Defence Forces (TPDF).

The SUMATRA announcement was based on a decision made by members of the Dar es Salaam Commuter Bus Owners Association (DARCOBOA), to scrap the traditional free rides hitherto enjoyed by police and military personnel in uniform, and charge them bus fare like everybody else.

Mtweve said the cash-strapped police force currently does not have any budgeted funds to tackle the looming public transport nightmare for its nationwide staff network.

’’We are not in an adequate enough financial position to meet the costs of transporting our officers to and from work, as well as when they use public transport in the course of their daily official duties,’’ Mtweve stated.

He said the force currently has about 27,000 personnel across the country, with up to 7,000 stationed in Dar es Salaam alone.

’’I don’t think the force can provide its own transport for all police officers in the country, everyday, everywhere and at all times,’’ he said, describing the decision to require uniformed police officers to pay fare when using public transport as a major logistical challenge.

He further noted that the overall effectiveness of police operations may be undermined as a result of this crisis.

Mtweve was speaking in the wake of reports published this week by THISDAY that top TPDF brass and senior officials from the Ministry of Defence and National Service will be meeting in the near future to discuss the problem.

According to incumbent defence minister Dr Hussein Mwinyi, the announcement to start charging bus fares to military personnel in uniform has taken the ministry completely by surprise, since its budget proposals for 2008/09 have already been prepared and approved by Parliament, and did not include any allocation for provision of transport allowances to TPDF personnel

Dr Mwinyi said in an interview with THISDAY earlier this week that the situation as it now stood would require a top-level meeting on how to address the resulting logistical problem of how to transport TPDF troops living outside barracks to and from work.

Some mainly junior-rank TPDF soldiers have told THISDAY that they are currently not given any transport allowances because they previously did not need to pay for public transport.

Since the new system became effective on August 1, there have already been reports of isolated incidents of army men refusing to pay bus fares while commuting within Dar es Salaam. Several daladala conductors have complained of being beaten up by soldiers whom they tried to press to pay up.

In the case of the police, Commissioner Mtweve acknowledged that there is no formal legislation that allows policemen and women to be given free rides on public transport service vehicles.

’’It’s a social dilemma, because bus operators are looking to make a profit yet there is no actual law stating that police officers shall ride passenger buses free of charge,’’ he remarked.

Like Dr Mwinyi, Mtweve said the fact that Parliament has already approved the 2008/09 budget proposals for the Ministry of Home Affairs (under which the police force falls) makes it all the more difficult to solve this particular problem.

It is understood that although it made the announcement, SUMATRA has yet to officially endorse the DARCOBOA decision to start charging bus fares to uniformed police and military personnel.

According to industry sources, SUMATRA has not issued any directive to this effect. ’’It is the bus owners themselves who decided to start charging police and military officers for using public transport services�apparently after realizing that there is no law stopping them,’’ said one reliable source.
 
.......kama Kikwete Anataka Amani Ni Lazima Aagize Huu Waraka Wa Sumatra ..ufutwe..tatizo Kubwa La Tanzania Ni Kuwa Huwezi Kuwaambia Askari Walipe Nauli Wakati Hawapewi Hiyo Posho..pia Marea Nyingine..wanakuwa Wametumwa..na Magari Hayatoshi..

Hii Tena Inadhihirisha Namna Rais Alivyokosa Mamlaka ...sitegemei Kiongozi Yeyote Tena Wa Sumatra Kudhubutu Kutoa Kauli Kama Hii Bila Kuwasiliana Na Serikali ..ili Ijipange..kauli Hii Ingeweza Kusababisha Uasi Jeshini...kama Si Angalau Wapiganaji Na Maofisa Kuwa Na Subira.....statement Kama Hizi Zinadhoofisha Nguvu Ya Rais Hasa Kipindi Hichi Ambacho Hali Ya Uchumi Imeendelea Kuwa Duni ..ni Kama Kupigulia Msumari Wa Mwisho Kwenye Maisha Magumu Waliyo Nayo Askari Wa Chini Leo,ukizingatia Rais Alikuwa Afisa Wa Jeshi Anatakiwa Kujua Haya...ni Amiri Jeshi Mkuu..ambaye Ana Jukumu La Kuhakikisha Kuwa Vijana Wake.....wanalipwa Nauli Kila Mwezi Au La ..anawapa Wote Nyumba Barracks..............askari Wengi Wanaishi Uraiani Kwa Kuwa Wamekosa Nyumba Kambini......

Kama Hawa Vijana Hawatapatiwa Posho Za Nauli..au Kupatiwa Mabasi Yao ...basi Utawala Wa Kikwete Utakuwa Na Changamoto Sana ...kwa Saababu Tayari Askari Wa Ngazi Za Chini.....wameanza Kunungunika Wazi..kitendo Cha Kudhalilishwa Kila Wanapotaka Kusafiri....na Hasa Kufikia Baadhi Ya Wapiga Debe Wanaowakebehi..kama Kula Kulala..for Which Is Not Fair ..wapiga Debe Wengi Ni Watoto Na Hawajaona Vita So Hawajui Role Ya Askari.....hasa Wanapowaona Wanafyeka Fyeka Makambini..mwao......
 
Lazima kuwepo na Sheria...Social dillema isitegemewe..anytime hali inabadilika..

Maisha Magumu si kwa wanajeshi tu na askar...sote wananchi tuna Hali ngumu.

Hivi Wanafunzi na wanajeshi wapi wanastahili kupanda Bure?....na Vp Madaktari? as long as wanalipwa mshahara wanastahili walipe Nauli.....
 
Lazima kuwepo na Sheria...Social dillema isitegemewe..anytime hali inabadilika..

Maisha Magumu si kwa wanajeshi tu na askar...sote wananchi tuna Hali ngumu.

Hivi Wanafunzi na wanajeshi wapi wanastahili kupanda Bure?....na Vp Madaktari? as long as wanalipwa mshahara wanastahili walipe Nauli.....

Polisi na wanajeshi katika nchi za magharibi wanatakiwa walipe nauli katika mabasi, hivyo sioni kwa nini mapolisi na wanajeshi wetu wasilipe nauli hizo. Maisha magumu, kama alivyosema Chuma hayawaathiri wao peke yao bali Watanzania wote.
 
Issue hapa ambayo tunapaswa kuilewa kabla ya kushinikiza hawa polisi au wanajeshi walipe nauli ni kwamba katika mishahara yao,hakuna kitu kinaitwa posho ya usafiri (transport allowance) na kwakuwa budget imeshapita huwezi kuilipa hiyo posho! sasa nafikiri ni vyema serikali ikaangalia namna ya kulifanyia kazi hili suala wakati ikiendelea kujipanga kuanza kuwalipa posho askari wetu.Usalama wetu na nchi yetu unawategemea sana hawa watu wala si wakati wa kuanza kuwabeza badala yake tunatakiwa tuwapiganie ili waboreshewe maslahi yao na hivyo waweze kufanya kazi yao ngumu kwa moyo wa kujituma na kizalendo.Huu uamuzi uwe deferred wakati serikali ikijipanga.hayo ndiyo maoni yangu
 
Hakuna yeyote anayewabeza polisi au wanajeshi, bali tunasema ukweli kwamba hali ngumu ya maisha haiwaathiri polisi na wanajeshi pekee yao bali Watanzania wote hivyo badala ya kutafuta suluhisho la kuwasaidia wao pekee litafutwe suluhisho la kuwasaidia Watanzania wote. Wanajeshi na polisi wanapendelewa kiasi cha kutosha, kama sikosei wana maduka yao ambayo wananunua bidhaa mbali mbali za muhimu kwa bei poa ukilinganisha na bei halisi ya bidhaa hizo.
 
Lazima kuwepo na Sheria...Social dillema isitegemewe..anytime hali inabadilika..

Maisha Magumu si kwa wanajeshi tu na askar...sote wananchi tuna Hali ngumu.

Hivi Wanafunzi na wanajeshi wapi wanastahili kupanda Bure?....na Vp Madaktari? as long as wanalipwa mshahara wanastahili walipe Nauli.....


..tukikosa usalama hata haya tunayoyapigania tutayakosa...in first place nimesema kuwa rais hana control wala vyombo vyake havina control[usalama]...nchi yeyote systemised ..mtu hawezi kukurupuka tu na kusema askari walipe nauli bila kufanya intersectorial collabo...kujua kwanini hawalipi....wangejadiliana wangejua hawalipi kwa sababu ...mshahara wao hauna hicho kipengele....wangewasiliana na hazina hata kabla ya budget ili kifungu cha nauli kiwepo......mnajua tunao askari wa vyombo vyote kama 100,000 assume kila mmoja inaamuliwa alipwe tsh 50,000 za usafiri..inamaana itabidi budget iongezeke kwa BILIONI 5 KILA MWEZI..au BILIONI 60 kwa MWAKA.....je HIZO PESA ZIPO?????......wakati pesa za operation nyingine still hazitoshi??????

NCHI NYINGINE HAWALIPI NAULI ...MNAJUA KWA NINI..KWA SABABU ASKARI WAO WOOTE WAPO BARRACKS....so akiamua kupanda public transport kwenda kumsalimia nduguye that is different ....kwa kuwa barracks za wenzetu zimejitosheleza hadi ENTERTAINMENT ZA HALI YA JUU ZIPO...nenda hapo kenyya tu uone barracks zao....

MNAJUWA miaka KAMA 10 ILIYOPITA ILIKUWA HIVI HIVI UPANDE WA CHAKULA...ASKARI WOTE WANASTAHILI KUPEWA CHAKULA....RATION ...IKAJAKUONEKANA KUWA ASKARI ASILIMIA KUBWA WAMEKOSA NYUMBA BARRACKS ...SERIKALI ILIYOPITA ILITAFAKARI NA KUAMUA KUWALIPA ASKARI POSHO ZA RATION KWA KUWA WANAISHI NJE YA KAMBI .....

haya MAMBO SI YA KUKURUPUKA...TUTAHARIBU@!!!!!!!!!!!
 
PM, polisi na wanajeshi ninaozungumzia mimi wanaishi kwenye nyumba zao hawaishi Barracks. Hivyo sioni sababu yoyote ya kuwa na sera maalum za upendeleo kwa wanajeshi wakati matatizo yanayowakumba wanajeshi ndiyo hayo hayo yanayowakumba wananchi wa kawaida. Wapewe mishahara mikubwa wapewe transport allowances lakini kwenye mabasi walipe kama Mtanzania mwingine yeyote yule.

Kama rasilimali zetu zingekuwa zinainufaisha Tanzania, kupunguza matumizi ya anasa kama magari ya kifahari na safari za JK za majuu zisizokwisha na lundo la maofisa katika safari hizo na kupambana na mafisadi wanaokupua mabilioni ya walipa kodi basi labda tungeweza kabisa kuwalipa Watanzania wote mishahara mizuri inayoendana na hali halisi ya gharama za maisha.
 
PM, polisi na wanajeshi ninaozungumzia mimi wanaishi kwenye nyumba zao hawaishi Barracks. ..............

..polisi na askari wanaomiliki nyumba ni idadi ndogo kama ni sample size ..haitoshi kutoa confidence ya kuamini kuwakilisha askari wengi..

labda kwa kifupi watu hawajui hii ya askari kusamehewa nauli ilikujaje...

this was or is a presidential decree..iliyotolewa na rais mwinyi ..kipindi kile alikuwa anakabiliwa na hali ngumu....na askari waliomba kuongezewa mishahara na posho..na walikuwa wakidai malimbikizo.....zaidi ya hapo serikali haikuwa na pesa na hata huduma zao nyingine ie mabasi yao ,malori ,magari ya maafisa...ie ungeweza kukutana na kanali wa jeshi kwenye daladal...hii ilisababisha usalama kuwa mdogo ..na waliokuwa wakuu ERNEST KIARO na TUMAINIEL KIWELU walimshauri rais achukue hatua za dharura ...

alichukuwa hatua zifuatazo..

1.KWANZA ALITANGAZA KUWA ASKARI WOTE WASILIPE NAULI KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI..na wakati ule wananchi walielewa ..kuna wakati wanajeshi waliweza kupanda gari kwenda mikoani bure..pamoja na kuwa walikuwa wameruhusiwa town trip tu!

2.PILI kwa hali ngumu waliyokuwa nayo maofisa ...aliongea na serikali ya korea ikakubali kuwapa mkopo wa magari commiissioned officers wote waliopenda[ingawa walikuwa wanabeza hyundai ni mbovu].....walikuwa wanachagua hyundai saloon or picup....hadi leo mnaziona ...pia kampuni ya MITSUBISHI ilikubali mpango huo na kuwakopesha..[nina imani hata muungwana atakuwa nalo moja kati ya hayo]

3.TATU askari wote wenye kuanzia sermajor hadi staff sergent ..walipewa mikopo ya pikipiki..[waliotaka]...za kikorea .[sangyung]....wakala alikuwa muhindi mmoja nazi wa simba..

4.NNE askari woote waliobakia walikopehwa baiskeli.....

HATUA HIZI KWA KIASI KIKUBWA ZILIPOOZA MAMBO NA KUFANYA MZEE MWINYI AMALIZE NGWE YAKE SALAMA...!..ILIKUWA HATUA MUHIMU KUCHUKUA KWA WAKATI ULE!!!

ikimbukwe kuwa chanzo cha yote haya ni serikali kushindwa kuwaweka vijana BARRACKS kwani askari waliopo barracks nchini hata hawafiki asilimia 40%...na utaratibu duniani askari wanakaa barracks..kama ukishindwa kuwaweka inabidi uwasafirishe....au uwawezeshe walipe..na pia lazima uwape RATION allowance kwa sababu wakiwa barracks wanapata chakula....thats why mkapa naye aliamua kuanza kuwalipa askari wote wanaoishi nje ya makambi pesa ya chakula au wale wa makambini waliooa..

NCHI ZOTE ZA KISTAARABU MNAZOOONA ASKARI WANALIPA MJUWE KUWA SERIKALI IMEWAPA WOTE MAKAZI BARRACKS ...kwa hiyo wanapokuwa nje ya hapo huhesabika wapo kwenye matembezi binafsi...kama ni ya kikazi zinamudu kuwapa mabasi au magari..ambayo hiyo hata hapa inafanyika kwa sasa ......
 

..polisi na askari wanaomiliki nyumba ni idadi ndogo kama ni sample size ..haitoshi kutoa confidence ya kuamini kuwakilisha askari wengi..

labda kwa kifupi watu hawajui hii ya askari kusamehewa nauli ilikujaje...

this was or is a presidential decree..iliyotolewa na rais mwinyi ..kipindi kile alikuwa anakabiliwa na hali ngumu....na askari waliomba kuongezewa mishahara na posho..na walikuwa wakidai malimbikizo.....zaidi ya hapo serikali haikuwa na pesa na hata huduma zao nyingine ie mabasi yao ,malori ,magari ya maafisa...ie ungeweza kukutana na kanali wa jeshi kwenye daladal...hii ilisababisha usalama kuwa mdogo ..na waliokuwa wakuu ERNEST KIARO na TUMAINIEL KIWELU walimshauri rais achukue hatua za dharura ...

alichukuwa hatua zifuatazo..

1.KWANZA ALITANGAZA KUWA ASKARI WOTE WASILIPE NAULI KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI..na wakati ule wananchi walielewa ..kuna wakati wanajeshi waliweza kupanda gari kwenda mikoani bure..pamoja na kuwa walikuwa wameruhusiwa town trip tu!

2.PILI kwa hali ngumu waliyokuwa nayo maofisa ...aliongea na serikali ya korea ikakubali kuwapa mkopo wa magari commiissioned officers wote waliopenda[ingawa walikuwa wanabeza hyundai ni mbovu].....walikuwa wanachagua hyundai saloon or picup....hadi leo mnaziona ...pia kampuni ya MITSUBISHI ilikubali mpango huo na kuwakopesha..[nina imani hata muungwana atakuwa nalo moja kati ya hayo]

3.TATU askari wote wenye kuanzia sermajor hadi staff sergent ..walipewa mikopo ya pikipiki..[waliotaka]...za kikorea .[sangyung]....wakala alikuwa muhindi mmoja nazi wa simba..

4.NNE askari woote waliobakia walikopehwa baiskeli.....

HATUA HIZI KWA KIASI KIKUBWA ZILIPOOZA MAMBO NA KUFANYA MZEE MWINYI AMALIZE NGWE YAKE SALAMA...!..ILIKUWA HATUA MUHIMU KUCHUKUA KWA WAKATI ULE!!!

ikimbukwe kuwa chanzo cha yote haya ni serikali kushindwa kuwaweka vijana BARRACKS kwani askari waliopo barracks nchini hata hawafiki asilimia 40%...na utaratibu duniani askari wanakaa barracks..kama ukishindwa kuwaweka inabidi uwasafirishe....au uwawezeshe walipe..na pia lazima uwape RATION allowance kwa sababu wakiwa barracks wanapata chakula....thats why mkapa naye aliamua kuanza kuwalipa askari wote wanaoishi nje ya makambi pesa ya chakula au wale wa makambini waliooa..

NCHI ZOTE ZA KISTAARABU MNAZOOONA ASKARI WANALIPA MJUWE KUWA SERIKALI IMEWAPA WOTE MAKAZI BARRACKS ...kwa hiyo wanapokuwa nje ya hapo huhesabika wapo kwenye matembezi binafsi...kama ni ya kikazi zinamudu kuwapa mabasi au magari..ambayo hiyo hata hapa inafanyika kwa sasa ......

Ninajua ninachokizungumza kwamba hao polisi na wanajeshi hawakai Barracks na hulipa nauli ya usafiri kila watumiapo public transport kwenda makazini au kununua mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Watawala wengi wa Afrika wanakikisha wanajeshi na polisi wanakuwa na maisha mazuri sana ili wasilete ukorofi dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani. Ndiyo maana wengi huwa na sera tofaut za kuhakikisha wanajeshi wanaishi kama vile wapo katika nchi tofauti wakati wananchi wa kawaida wanaumia na hali ngumu ya maisha. Mfano hai ni juzi tu katika nchi ya Zimbawe ambapo wanajeshi na kama sikosei polisi wa nchi hiyo walitamka hadharani kwamba kama dikteta Mugabe asipochaguliwa basi wataipindua nchi.

Sote tunajua jinsi Mugabe alivyouangusha uchumi wa Zimbabwe na kufikia kiasi mkate unanunuliwa kwa Z$ 20 billion. Hakuna kazi, hakuna chakula, wananchi wanaishi maisha ya dhiki kubwa lakini bado wanajeshi na mapolisi wa nchi hiyo walitaka Mugabe aendelee 'kuiongoza' nchi hiyo kwa mshangao wa Wazimbabwe walio wengi na Waafrika na hata dunia nzima. Hii ni kwa sababu Mugabe alihakikisha wanaishi katika maisha ambayo yana tofauti kubwa na wananchi wa kawaida. Kwa sababu hiyo basi ndiyo nikasema si vibaya kuwa na sera maalum za kuwasaidia wanajeshi lakini si za kupanda mabasi bure, wapewe allowances, watafutiwe mabasi maalum ya jeshi na polisi ili kuwasaidia katika usafiri. Na siyo kutaka kuwabebesha wenye mabasi binafsi mzigo usiowahusu.

Pia Tanzania si nchi maskini tuna rasilimali kibao ambazo kama tungesaini mikataba ambayo siyo ya kifisadi na pia kupambana na kuwafilisi mafisadi waliokupua mabilioni ya pesa basi polisi, wanajeshi na Watanzania wote wanaweza kabisa kulipwa mishahara na marupurupu ambayo yatawawezesha kulipa nauli za usafiri bila hata matatizo yoyote.

Tumeona kwamba katika mwaka mmoja tu wa 2005/2006 mafisadi wamekupua kati ya shilingi bilioni 288 bilioni na trilioni, sasa hebu fikiria kama uchunguzi huo ungefanyika kuanzia mwaka 1998 ambapo Ballali alianza kazi rasmi BoT kama Gavana. Chukua gharama kubwa za uendeshaji wa serikali magari ya kifahari ambayo yanatumia mafuta kwa kiwango cha juu kabisa na magari hayo kama sikosei mara ya mwisho tuliambiwa serikali inayo magari hayo 1,000 kama siyo zaidi.

Serikali ianzishe mashirika ya umma ya usafiri na kuwaruhusu wanajeshi na polisi kupanda mabasi hayo bila kulipa, lakini kuwashinikiza wafanya biashara binafsi wenye mabasi hayo kuwabeba polisi na wanajeshi bila kulipa ni uonevu wa hali ya juu, kwa sababu wao hawahusiki kwa namna moja au nyingine na matatizo ya usafiri yanayowakabili polisi na wanajeshi bali yamesababishwa na sera na utawala mbovu wa serikali iliyo madarakani.
 
ninajua Ninachokizungumza Kwamba Hao Polisi Na Wanajeshi Hawakai Barracks Na Hulipa Nauli Ya Usafiri Kila Watumiapo Public Transport Kwenda Makazini Au Kununua Mahitaji Yao Muhimu Ya Kila Siku.
.


...nafikiri Mpango Endelevu Hapo Ni Kuanza Au Kuendeleza Mipango Kabambe Wa Kujenga Barracks....mkapa Alianza ...baadhi..na Uwt Asilimia Kubwa Sasa Watakuwa Na Nyumba Sehemu Yao....juzi Hapa Nssf Imekubali Kuwajengea Polisi Barracks Kilwa Rd,na Pemba..kwa Makubaliano Ya Kibiashara....bila Kusolve Tatizo La Makazi ...tatizo La Askari Kulalamikia Usafiri ...litakuwa Linajirudia Rudia...

....nadhani Tathmini Ya Mahitaji Ya Nyumba Inahitajika Kufanyika .....majeshi Yenyewe Yaendelea Kuingia Ubia Na Mabenki Na Mashirika Mengine Kwa Udhamini Wa Serikali ..ili Wajengewe Makazi Ya Kutosha.......

...pia Utaratibu Wa Kujenga Makazi [estates]....na Kuyauza Kwa Gharama Nafuu Za Mkopo Kwa Watanzania Hasa Watumishi Wa Umma,askari Nu Muhimu..kwani Mfanyakazi Akishakuwa Na Uhakika Wa Kukopeshwa Nyumba Atakayoishi Uzeeni..basi Hata Tamaa Ya Kukwapua Ili Akajijengee Kwenye Viwanja Visivyopimwa Inapungua....
 
Mimi naunga mkono ombi hili la Wanafunzi na kuongeza kwamba polisi na wanajeshi nao watafutiwe usafiri wao badala ya kuwashinikiza wenye mabasi binafsi wawasafirishe bure.

Wanafunzi waomba usafiri wao

na Lilian Mbowe SAUT na Nasra Abdallah
Tanzania Daima~Sauti ya watu

KUTOKANA na mzozo unaoendelea kati ya makondakta na wanafunzi baada ya kuruhusiwa kulipa sh 100 na kukaa ndani ya daladala, wanafunzi sasa wameiomba serikali kuwatafutia usafiri wao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Katibu Mkuu wa Chama cha wanafunzi (TASSA), Augustino Matefu, alisema tangu kutangazwa kwa hatua ya kuruhusiwa kukaa, tatizo la usafiri kwao limezidi kuongezeka badala ya kupungua.

Alisema ni vema sasa serikali ikaangalia utaratibu wa kuwa na usafiri kwa wanafunzi ambapo amedai watakuwa tayari kuchangia hata ununuaji wa vipuri ilimradi waondokane na adha hiyo.

Alisema kitendo cha wao kuruhusiwa kukaa kwenye viti, kumechangia kuachwa vituoni na makondakta na hivyo wengine kushindwa kufika shule kwa wakati muafaka na wengine kushindwa kabisa kwenda shule.

Aidha, aliishauri serikali iwasiliane na wahisani mbalimbali kama inavyofanya katika masuala mengine, ili waweze kupata usafiri.

"Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta wahisani kupambana na ugonjwa wa ukimwi, lakini pia wajue tatizo la ukimwi kwenye shule za sekondari halitapungua kama bado wanafunzi watakuwa wakinyanyasika kwenye usafiri," alisema.

Akizungumzia kikao kilichofanyika mwanzoni mwa wiki iliyopita, kilichoshirikisha SUMSTRA na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Matefu alisema uamuzi wa wanafunzi kulipa nauli ya sh 100 na kukaa kwenye viti , ulifanyika kwa shinikizo.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Sumatra, David Mzirai, alipozungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kuhusiana na malalamiko hayo alisema kiasi cha sh 100 kinacholipwa sasa na wanafunzi ni cha mpito na kusisitiza kwamba kuanzia Julai mwakani wanafunzi hao watapaswa kulipa nusu nauli ya mtu mzima kama sheria inavyoonyesha.
 
Back
Top Bottom