Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Ksk,Hata ukijificha vipi na uongo mwingi, kila mtu anajuwa wewe ni nani. Ila ungekuwa mkweli ungeonyesha pande zote za shillingi. Upande mzuri na upande mbaya. Ni kweli mapinduzi ya Zanzibar au mapinduzi ya nchi yoyote yana mazuri na mabaya. Mabaya ni yale ya watu wengi kupoteza uhai. Kama ingewezekana ingekuwa jambo jema mapinduzi kutokea bila vifo kwa upande wowote. Kwa upande mwingine mapinduzi huleta uhuru kwa wale ambao hutawaliwa kwa maguvu, kama vile sultani alivyokuwa anatawala Zanzibar na kuwafanya weusi kuwa watumwa nyumbani kwao.
Ila sihangai mleta maada kuangalia hili kwa upande mmoja. Huyu ni kinara wa malalamiko mengi ambapo huwa anatetea uarabu, mara uislamu, mara Nyerere kawasahau waleta uhuru halisia na mambo chungu mbovu. Sasa hapa kaja kwa kujificha ili tusimbaini ni nani.
Lam...Negative perception, mpk inashangaza… atleast ungenarrate hta gettysburg address ya Abraham Lyncoln
Pro...Mzee Mohamed yale yalikuwa mapinduzi maana serikali ya Shamte iling'olewa....kuna wanaoita ule ulikuwa 'uvamizi' kutoka Tanganyika wakishirikiana na kina Hanga...hii historia ina utata mwingi na watawala hawataki kuiweka wazi.
Jiwe...Hivi kuna watu bado wanafuatiria huu upupu wa huyu mzee ambaye mawazo yake zote yapo kwa bwana zake waaarabu..kwa mgongo wa dini.
Huyu mzee wa kupuuzwa kama wapuuzi wengine wanayopaswa kupuuzwa.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe...
''Wanafuatilia,'' si ''Wanafuatiria.''
''Waarabu,'' si ''waaarabu,'' na unaanza na herufi kubwa, ''Waarabu.''
Nukta zinakuwa tatu, ''...''
Uniwie radhi lakini ni vyema hapa tukachukua fursa kama hizi kufunzana lugha za kistaarabu katika kuandika.
Ukishaandika ipitie kazi yako uangalie makosa ili ufanye masahihisho.
Tukitoka hapa tunaweza tukaingia katika adabu za uandishi ikiwa utapenda nikufundishe.
Uarabu au Uafrika wake unahusiana vipi na mada hii?!Hivi huyu Mzee Ni muarabu?
Mcq...Hivi huyu Mzee Ni muarabu?
Chinch...Mzee tunashukuru kwa Historia, je hao rafiki wa baba yako waliouawa waliuawa kwa sababu gani wakati wao walikuwa ni ASP? au walikuwa na asili ya kiarabu au chotara?