Trafiki waagizwa kukamata na kutoza faini magari kumi kila siku

mkurya org.

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
1,571
1,694
Ni usalama barabarani yaani Trafic wameagizwa kuyakamata angalau magari kumi kila siku na kuyatoza faini

Chanzo: Jambo leo
 
Kama gari yako iko safi na unafuata sheria za usalama barabarani hata gari 20 hazipati hizo faiin
Tuwe makini ili wakose
 
Labda wanakusanya hela ya madawati ili wampelekee mkuu wa mkoa, duuuh watanzania kwa kweli tumekuwa wabunifu
 
Nadhani kila eneo wamepangiwa idadi yao nadhani hiyo kumi ni Dar labda. Hapa kuna hatari ya kubambikiziana makosa askari asipofikisha hayo makosa kumi. Ki utaratibu ni kwamba sheria ikianza kusimamiwa vizuri watu huwa wanabadili tabia na kuacha kufanya makosa, je hizo faini 10 watazipata wapi?
Mbaya sana serikali ikiamua kutumia makosa ya wananchi wake kama chanzo cha mapato.
 
BANDARI NYEUPEEEE....BEIRA YAELEMEWA NA SHEHENA.
TAFUTENI TATIZO!!!
...atauwaaaa...let ppls relax...
n.b/
law of influx needed, shusheni viwango mpate meli nyingi,au pandisheni mkose hata kidogo...
Kama la sukari hatujaliona na kulifumbua hilo la bandari tutaanzia wapi ngoja twende vivi hivi hadi kieleweke ila mapato yapatikane hata kwa kuuza tairi za magari yanayoingilia njia za DART
 
Nadhani kila eneo wamepangiwa idadi yao nadhani hiyo kumi ni Dar labda. Hapa kuna hatari ya kubambikiziana makosa askari asipofikisha hayo makosa kumi. Ki utaratibu ni kwamba sheria ikianza kusimamiwa vizuri watu huwa wanabadili tabia na kuacha kufanya makosa, je hizo faini 10 watazipata wapi?
Mbaya sana serikali ikiamua kutumia makosa ya wananchi wake kama chanzo cha mapato.
Wanalazimisha, kuna sehemu wanakaa na tochi lkn hakuna alama yoyote ya barabarani inayoonyesha speed limit ukiwauliza wanakwambia haya ni makazi ya watu.

Sasa dereva anaendesha gari kufuata alama za barabarani au kufuata makazi ya watu?
 
sijawahi sikia nchi yeyote duniani inalazimisha watu wafanye makosa ili walipe faini, basi kama ndiyo hivyo trafic wote wapelekwe pale CBE ili wasomee masuala ya kodi then wapelekwe TRA na kazi ya kuongoza shughuli za usalama barabarani wapewe TRA...."kama ni kweli"........ngachoka.....
 
Maskini wa Mungu weee, nilikua na rafiki yangu wa kike Trafiki, nilikutana nae huko mikoani wakati naenda Musoma 2013, yuko Mkoa Fulani hapo tukajenga mazoea mwaka jana alikua miongoni mwa askari ambao walikuja kujiandaa na gwaride la Uhuru kabla ya kuahirishwa, nilipata muda wa kuongea nae hapa Dar na baadhi ya mambo aliyoyaeleza ambayo kwake ni magumu ilikua ni pamoja na hilo la kuwekewa idadi ya "Mabao" ya kupeleka kwa Boss. Alisema Baadhi ya Mikoa kama Mwanza si chini ya magari matano kwa kila askari kwa siku na kwa upande wake yeye alipangiwa at least magari matatu kwa siku mana ni mkoani na ni highway... anakwambia hakuna kazi ngumu kama hio na usipopeleka jamaa wanakutukana kama mtoto.

Nikajiuliza, hii sasa ni kazi au ni adhabu, namtafutia Chuo aje kusoma aachane na huo wizi wa nje nje
 
Back
Top Bottom