Trafiki Dodoma waanza kutafuta pesa za Xmass kihuni

Nov 13, 2016
9
4
Wakati tunaelekea Krismasi, kuna matrafiki wameanza kuwanyanyasa raia isivyo halali. Naongelea mfano wa leo leo. Taarifa iliyonifikia inasema hivi:

"Trafiki kituo cha Msembeta Dodoma wameamua kuvua uniform na kujificha vichakani wakiwa na kamera zao binafsi kuvizia magari kilometa mbili kabla ya kituo cha msembeta shule ya msingi. Wanatoza faini ya TZS 30,000 kwa kila mtu anayeonekana kuzidisha mwendokasi. Hakuna alama yoyote ya barabarani kuhusu speed limit. Baada ya kubanwa na madereva werevu, wakajibu kwamba wanatumia sheria ya makazi kutoza faini. Wanasema kibao kinapaswa kuwepo sema tu TANROADS wamechelewa kukiweka. Maderevea wanaokomaa wanaachiwa, wanaolegea wanakamuliwa. Njiani ni kero tupu."

Mh Mwigulu na wenzako fuatilieni ujambazi huu...
 
Sehemu zingine wanajificha kwenye magari au wanavalia kimasai huku wanapiga tochi ukijichanganya 30 inakutoka
 
Duh, msimu huu wa sikukuu mapato kutokana na makosa ya barabarani yataongezeka mara dufu!
 
Kimsingi, Mwigulu inabidi atoe ufafanuzi wa haya:
1. Ni sahihi Askari kujificha vichakani, kwenye nyumba za watu, na hata nyuma ya magari
mengine?
2. Ni sahihi kutoza faini dereva wakati hakuna alama ya speed limit?
3. Je hili suala la sharia ya makazi halihitaji alama ya speed limit?
4. Ni sahihi kupiga tochi na kurusha picha kwenye simu ya askari mwingine aliye mbele?
5. Je uvumi kuwa askari akitoza faini ya 30,000, anapewa 5,000 ni wa kweli?

Mji wa Kayanga Wilayani Karagwe uko km 6 toka mji wa Omurushaka Karagwe. Jana tukiwa na waandishi wa habari kutoka DSM, tulikamatwa katikati ya Omurushaka na Kayanga. Tulichoambiwa ni kuwa kutoka Kayanga mpaka Omurushaka speed limit ni 50. Tulipouliza kibao kiko wapi, tukaambiwa hakipo lakini "tunatakiwa kujua".

Huu ni uonevu na kuichonganisha serikali na wananchi wake.
Mahali popote kama kuna eneo lefu lenye speed limit, inatakiwa waweke vibao kila baada ya umbali Fulani kuwakumbusha madereva kuwa bado wamo ndani ya speed limit. Madereva wote si lazima wawe wenyeji wa eneo.
 
Back
Top Bottom