Traffic lights kona ya vingunguti

julisa

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
209
49
Ktk kona ya vingunguti barabara ya nyerere zimefungwa taa za kuongozea magari ambazo zinasababisha foleni tu. sijui hawa wajenzi wanajifunzia wapi pyuuu!
 
Hata mimi nimezishangaa sana hizo taa. Haya ni matatizo ya kutoa majibu ya haraka bila kufanya utafiti wa kina. Binafsi sioni mantiki ya hizo traffic lights kwani wakati hazikuwepo hakukuwa na tatizo lolote.
 
bado sijaziona mi nakaa vingunguti kidarajani sijapita muda kule nimeposti sabb mungu akinipa ruksa ya kuvuta hii hewa yake mpaka 20!5 mi ndo ntakuwa diwani kule
 
bado sijaziona mi nakaa vingunguti kidarajani sijapita muda kule nimeposti sabb mungu akinipa ruksa ya kuvuta hii hewa yake mpaka 20!5 mi ndo ntakuwa diwani kule

Hahahaha u just seized the opportunity kutangaza nia
 
Nimesita kuanzisha uzi mpya lakini mod akiona inafaa ruksa.
Hapo vingunguti kwa sasa pamegeuzwa kijiwe cha genge la askari wala rushwa na hasa kwa jamaa wa bodaboda yaani ukipita hapo bila kukutwa na kosa lolote basi wewe ni malaika.
Leo nimeshuhudia pikipiki zaidi ya ishirini zikiruhusiwa kuondoka moja baada ya nyingine baada ya kutoa rushwa kwa polisi na kwa bahati nzuri nilifanikiwa kumuuliza mmojawapo akaniambia yeye amekamatwa kwa kosa la kutovaa koti zito bila kujali joto lote hili!
Badala ya kuelimishwa amepigwa faini elfu 30 na ndipo alipojiongeza na kutoa elfu 5 kama rushwa ili awahi kibaruani.
Hivi hawa askari wameruhusiwa na nani kujazana hapo Vingunguti na kuwakamua watu pesa zao? Je kuna ugumu gani kuwatia hatiani hao askari?
Hivi hawa askari wanajua kuwa wao sio wazalishaji na hivyo mishahara yao inategemea uzalishaji wa viwandani ili walipwe?
Ni hizo bunduki wanazotishia nazo watu lakini nina imani watu hawapendi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom