Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 70,480
- 167,336
Wakuu habari za Jumapili,
Nimeona nipaze sauti yangu kwa hili linalosumbua akili yangu kwa siku ya nne.
Naogopa kuja kutumia neno (NILIJUA) ajali zitakapo tokea, katika hili wahenga walisema majuto ni mjukuu nami sitaki nije kujuta au roho kunisuta.
Wengi mliofika Arusha kuanzia septemba 2015 na kutumia barabara ya Arusha. Moshi, mmejionea utanuzi wa barabara hii kutoka barabara moja kwenda barabara mbili kwa uelekeo mmoja.
Barabara hii imeanza kukamili kwa urefu wa karibu kilomita 4 kutoka Tengeru hadi daraja kubwa la nduruma. Ni wiki sasa barabara mbili kila upande zimeruhusiwa kutumika.
Kinachonisukuma kutoa tahadhari kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni matumizi mabovu ya barabara hii yatokanayo na ugeni (USHAMBA) wa watumiaji wa barabara WALIO WENGI.
Nimeshuhudia madereva wengi wakishindwa kuitumia barabara ipasavyo kwa mfano;
a) Magari madogo ya abiria (hiace) wamekuwa wakishusha abiria upande wa kulia katikati ya barabara badala ya kushoto vili po vituo hivyo kuleta usumbufu na kuhatarisha maisha ya abiria na magari.
a) Baadhi ya madereva hawajui kabisa kutumia hizi barabara, badala ya kupitia hizi barabara mbili za kushoto, wanapitia upande wa kulia yaani upande wa barabara mbili zinazoelekea upande alikotoka yeye.
Hivyo ninalishauri jeshi la polisi watoe elimu au maelekezo ya namna bora ya kutumia barabara hii ili kuepusha ajali ambazo zimenza kujitokeza zinazosababishwa na kutokujua kutumia barabara hii ya njia mbili.