Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,097
Ni swali la mjadala. Kwamba; Mitandao ya Kijamii ni RAFIKI au ADUI wa Vyombo vya Habari vikongwe i.e Televisheni, Redio na Magazeti?
Tunakumbuka jinsi tulivyokuwa tukifuatilia ratiba za televisheni na redio, bila kusahau story na habari kutoka magazetini. Katuni zile, makala za kusisimua, michezo ya kuigiza, taarifa za habari, muziki na kadhalika.
Maisha yalikuwa matamu sana aisee.. Hiyo ni kuanzia mwaka 2005 kurudi nyuma. Kabla ya ujio wa hii Mitandao ya Kijamii ambayo imeshika kasi kweli.
Leo hii mambo yamebadilika! Tangu zije Blogs, Facebook, Youtube, Twitter, Instagram mambo yamekuwa ni moto. Kwa ufupi, Intaneti imekuja kuleta mabadiliko ambayo huenda yakawa yameongeza au kupunguza uhondo ule.
Siku hizi kila kitu kinapatikana mtandaoni: Ukitaka habari unapata, muziki unapata, udaku unapata, mpenzi unapata (tena fasta), kazi unapata, elimu unapata... Na vyote hivi unavipata chap chap..
Kwa bahati mbaya, hizi zote mbili zina hasara zake pia.
Kwa mfano, Vyombo vya Habari vya zamani taarifa zilikuwa zinachelewa sana. Yaani habari inaweza kutokea saa hizi, ukaipata kwenye tv, redio au gazeti baadae sana au hata kesho yake.
Au, unaweza kukuta taarifa unavyoijua na inavyokuja kuripotiwa ni tofauti. Mambo yanafichwa fichwa kwa maslahi flani. Na hakuna mjadala kwenye habari. Ni kusoma, kusikiliza au kutazama, basi!
Haya, huku kwenye Mitandao (New Media) nako;
Hasara ya kwanza ni matango pori. Aisee ni rahisi sana kupewa habari za uongo huku kwa sababu taarifa nyingi zinaripotiwa bila kuthibitishwa kwanza. So kujua ya kweli na uongo sometimes ni mtihani.
Sio hivyo tu, mitandaoni kila mtu ni mjuaji. Kila mtu ni Mwandishi. Athari ya hii ni kama hiyo hapo juu; kusambaza 'fake news' au kutapeliana nje nje. Ndio maana Mamlaka zikaona zianzishe Sheria ya Mtandao ili angalau ku-control.
Hasara nyingine huku ni matumizi. Kwa sasa, sio kila mtu anaweza kutumia vizuri nyenzo za kufikia habari. Inahitaji uelewa mkubwa ili kuweza kutumia simu, kompyuta au vifaa vingine kama hivyo. Bibi yangu Nangondo kule Ugweno umpe smatifoni atumie anaanzia wapi?!
Kwa mantiki hiyo sasa, kusema kwamba New Media / Traditional Media ni marafiki au maadui inategemea...
1. Uadui utaonekana kwa vile intaneti imekuja kutoa changamoto kwa hawa jamaa wa zamani. Nani asubiri gazeti la kesho wakati habari nzima anaipata punde inapotokea?
2. Uadui utatokea ikiwa vyombo vya zamani vitashindwa kujiongeza na kutafuta nafasi kwenye ulimwengu wa kisasa. Kwani TV, Redio, Gazeti limekatazwa kujisajili mtandaoni na kufanya kazi zake?
3. Uadui utakuja pale vyombo vya zamani vitakaposhindwa kulinda uaminifu wake kwa wateja wake. Leo hii, mtandaoni iandikwe habari kwa juu juu, au uongo, halafu vyenyewe vikashindwa kwenda kutafiti na kuja na habari ya ukweli kwa kina.
4. Uadui utakuja pale ambapo vyombo vya zamani vitajenga uadui na New Media badala ya kujenga urafiki na kusaidiana.
5. Uadui hautaepukika endapo vyombo vikongwe havitosimamia weledi na kutumia taarifa za mtandaoni kama 'news tip' katika kufanya kazi zake.
Kwa ufupi, mimi binafsi namiss sana uhondo wa zamani lakini sijutii utamu wa sasa. Na kwa bahati nzuri, vyote vipo na vinaweza kufanya kazi kwa pamoja (co-exist).
Hayo ni yangu. Kama kuna mwenye hoja tofauti na hizo, namkaribisha kwenye mjadala.