Ndiyo, tradecarview.com ni wa kweli.
Unachotakiwa kujua ni kwamba, wao si wauzaji wa magari, tradecarview ni kama watangazaji tu, wao wanatoa huduma ya kutangaza magari yanayouzwa na wauzaji wa magari. Ni watu wengi tu wanaonunua magari hapo (mara nyingi mnadani unapata kitu kwa bei rahisi kidogo!).
Kama walivyosema wadau hapo juu, unaweza kupata gari bei chini lakini kuwa mwangalifu sana! fuatilia reputation ya hiyo kampuni, imekuwwepo tradecarview kwa muda gani, hawa tradecarview mara nyingi ni waangalifu wakipata malalamiko kuhusu kampuni wanaifungia kutangaza, mpaka mwizi huyo ajipange upya aingie na jina lingine.
Pia jitahidi kufuatilia details zote za gari, mara nyingi wezi hawa wanakuwa na picha tu za hayo magari, ukimuomba details kama deragistration au picha zaidi na service record anakuwa hana, usijiridhishe mapema, ulizia hata kwa watu wengine kama walishaagiza na hiyo kampuni, kampuni zingine ni za ukweli lakini wanaweza kukutumia gari ambayo hukuichagua, au MBOVU!!!!
YOTE KATI YA YOTE, UKITAKA KITU NAFUU UKUBALI KUTAKE RISK.