mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,073
Bandari ni lango kuu la mapato ya mengi yenye tija kwa maendeleo ya Tanzania ya leo na kesho..Umakini na udhati ktk kuitumia vema bandari yetu kuboresha mapato ya ndani una tija kubwa kitaifa sasa na baadae sababu ya umuhimu wa kijiografia ktk kuwahudumia nchi majirani na kujihudumia wenyewe kibiashara .
Kwa masikitiko makubwa uwazi wa hujuma za ukwepaji kodi kupitia udanganyifu wa thamani halisi,mapana ya mzigo,ubora wa mizigo,ujazo wa mizigo,ujanja ujanja,ulaghai wa nyaraka na matumizi mabaya ya fulsa za kibiashara vitaendelea kuitesa nchi yetu ikiwa hatua mahsusi hazitachukuliwa kudhibiti mianya mingi inayotumiwa na wafanyabiashara ama wafanyakazi wa wafanyabiashara na kulitia hasara kubwa taifa.
Mfano,Haiingii akilini kuipa fulsa ya kuendesha bandari kavu/Kuwa na kampuni ya uwakala wa forodha kampuni/mfanyabiashara mkubwa au Kikundi cha makampuni chenye/mwenye tuhuma za kukwepa kodi ya mabilioni kupitia ulaghai wa kutoa mizigo bandarini/kulipia kodi kama vile mizigo au bidhaa zilizopaswa kusafirishwa kwenda nje ya Tanzania lakini kwa makusudi zikauzwa ndani ya nchi hivyo kuikosesha serikali mapato makubwa ya kodi ya uagizaji,Ongezeko la thamani,n.k
Udhaifu wa kimkakati wa kuzuia waagizaji wakubwa kumiriki bandari kavu na kampuni za uwakala wa forodha /utoaji mizigo bandarini,kampuni za usafirishaji wa bidhaa kwenda nchi jirani.Uagizaji huo umekuwa ukihusisha bidhaa timilifu,ghafi,marighafi na bidhaa mtambuka toka nchi za nje kuja Tanzania.