Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amewataka wafanyabiashara wa kati maarufu kama mawinga kuhakikisha wanazingatia sheria za kodi na kujitokeza kulipa kodi kwa wakati.
Akizungumza Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam, Kamishna Mwenda ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Elimu ya Kodi kwa Biashara za Mtandaoni. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wawakilishi kutoka TCRA, BASATA, pamoja na Umoja wa Wafanyabiashara wa Kariakoo.
Kamishna Mwenda amesema kuwa biashara za mtandaoni zimeendelea kukua kwa kasi nchini, jambo linalofanya kuwa muhimu kwa wafanyabiashara wote hususan mawinga na wale wanaouza kwa kutumia mitandao kuelewa umuhimu wa kodi kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa.
"Nimesikia wengine wanasema sisi mawinga, mawinga, winga si kamisheni, biashara ya winga ni huduma. Ukifanya biashara la milioni moja na ukaiuza milioni moja na laki moja, hautatozwa laki moja, ila utatusaidia huyo wa milioni moja ni nani ili atozwe kwa milioni hiyo moja”, amesema Mwenda.
Aidha, ameeleza kuwa kampeni hii inalenga kuelimisha na kuwahamasisha wafanyabiashara wote kujiunga rasmi na TRA na kulipa kodi kwa njia sahihi. Alisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za malipo, hasa katika kipindi hiki ambacho biashara za mtandaoni zinaongezeka kwa kasi kubwa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amewataka wafanyabiashara wa kati maarufu kama mawinga kuhakikisha wanazingatia sheria za kodi na kujitokeza kulipa kodi kwa wakati.
Akizungumza Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam, Kamishna Mwenda ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Elimu ya Kodi kwa Biashara za Mtandaoni. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wawakilishi kutoka TCRA, BASATA, pamoja na Umoja wa Wafanyabiashara wa Kariakoo.
Kamishna Mwenda amesema kuwa biashara za mtandaoni zimeendelea kukua kwa kasi nchini, jambo linalofanya kuwa muhimu kwa wafanyabiashara wote hususan mawinga na wale wanaouza kwa kutumia mitandao kuelewa umuhimu wa kodi kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa.
"Nimesikia wengine wanasema sisi mawinga, mawinga, winga si kamisheni, biashara ya winga ni huduma. Ukifanya biashara la milioni moja na ukaiuza milioni moja na laki moja, hautatozwa laki moja, ila utatusaidia huyo wa milioni moja ni nani ili atozwe kwa milioni hiyo moja”, amesema Mwenda.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amewataka Wafanyabiashara wa kati maarufu kama "Mawinga" kuhakikisha wanazingatia sheria za kodi na kujitokeza kulipa kodi kwa wakati.
Kauli hiyo ameitoa leo August 9, wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TCRA, BASATA na Umoja wa Wafanyabiashara wa Kariakoo katika uzinduzi wa Kampeni ya Elimu ya Kodi kwa Biashara za Mtandaoni uliofanyika jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kamishna Mwenda amesema kuwa biashara za mtandaoni zinazidi kukua nchini, hivyo ni muhimu kwa Wafanyabiashara wote hasa mawinga, kuelewa umuhimu wa kodi kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa.
"Ni lazima wafanyabiashara wa kati wajue kuwa kulipa kodi sio adhabu, bali ni wajibu wa kila Mtanzania anayefanya biashara kuunga mkono jitihada za maendeleo ya nchi," amesema Kamishna Mwenda.
Aidha, amesema Kampeni hiyo ni hatua muhimu ya kuelimisha na kuwahamasisha wafanyabiashara wote kujiunga rasmi na TRA na kufanya malipo ya kodi kwa njia zinazofaa, hususan katika zama hizi za biashara za mtandao zinazoongezeka kwa kasi.