TRA yamwita Mbowe mahakamani kisa hakutumia mashine ya EFD Club ya Bilcanas

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
20170302_042800.jpg

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyodai kuwa imeshindwa kuwapata kwa kutumia hati za wito za Mahakama, Freeman Mbowe, mkewe Dk Lilian Mtei na aliyekuwa Meneja wa Klabu ya Bilicanas, Steven Mligo kujibu mashtaka yanayowakabili, jana ilisaidiwa namna ya kuwafikia watu hao.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, ilitoa barua ya wito wa kuwataka wahudhurie mahakamani Machi 21, baada ya kufikia uamuzi wa kutoa wito huo kupitia magazeti.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mkewe, Dk Mtei ni wakurugenzi wa Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd.

Wawili hao pamoja na Mligo, Katika kesi hiyo namba 402 ya mwaka 2016, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kushindwa kutumia mashine za kielektroniki (EFD) kutoa risiti kinyume na kifungu cha 86 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015.

Mashtaka mengine ni kuipotosha mamlaka kwa kutoa nyaraka za uongo kinyume na kifungu cha 84 na kushindwa kutekeleza masharti ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi kinyume na kifungu cha 82 cha sheria hiyo. Wanadaiwa kutenda makosa hayo Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa tangu kesi hiyo ilipofunguliwa mwishoni mwa mwaka jana, imeshatajwa mara nne bila washtakiwa kufika mahakamani.

Wakili wa TRA, Marcel Busegano aliieleza Mahakama kuwa wamejaribu kuwapelekea washtakiwa hati za wito wa kufika mahakamani mara nne lakini wameshindwa kuwapata.

Alidai Meneja wa TRA Mkoa wa Ilala alijaribu kumpigia simu ya mkononi Mbowe lakini hakumpata na, hata walipokwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anakofanya kazi mkewe, Dk Mtei pia hawakumpata.

Kutokana na hali hiyo, TRA iliiomba Mahakama iamuru watumie tangazo gazetini kuwaita washtakiwa mahakamani na iwapo korti itakubali ombi hilo, tangazo litolewe kabla ya tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Shauri hilo linalosikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo litatajwa Machi 21.

Kutokanana na ombi hilo, tangazo hilo linapaswa kutangazwa gazetini kabla ya tarehe hiyo.



========

Bila shaka naona hizi siasa hadi kwenye vyombo vya serikali na hili halijaanza Leo:

Nakumbuka kanda ya ziwa mmiliki wa Imalaseko yalishamkuta baada ya kushabikia upinzani TRA walivamia na kumfilisi.

Na wengine wengi ukiwa upinzani ukiisema vibaya chama tawala na serikali basi jamaa wanatumwa.

Kwa hali ya kawaida na kulingana na sheria za nchi Bilcanas inamilikiwa na Mbowe hotels ni kampuni kwanini wasiishitaki kampuni badala ya mtu?

Kampuni ni legal person na inataratibu zake kwanini afuatwe mmiliki badala ya kampuni?

Mbona kwa Dangote walifuata taratibu za kuwawajibisha na hawakumshitaki Dangote kama mmiliki wa campuni?
 
Viongozi wetu wanafikiri tatizo ni Mbowe.Ukweli tatizo ni maisha magumu ya Wananchi.Wakijitahidi kuboresha maisha na kutekeleza ahadi za uchaguzi Mbowe na wapinzani kwa ujumla hawatapata wafuasi.Lakini kama maisha yakiendelea kuwa magumu kama sasa watamkamata Mbowe mmoja wataibuka Mbowe Elfu.
 
Ha ha ha, nategemea kuona hata clouds, eatv, nyama choma, na club zote dsm wakiitwa, sababu hata wao walikuwa hawatumii EFD wakati wakikata receipt zao

Pili, Billcanas inamilikiwa na mbowe hotels, inatakiwa iitwe mbowe hotels kujibu hizo tuhuma, kisheria kampuni Ni mtu, (legal person) inashitaki, shitakiwa , kuzaliwa kukua na hats kufa, Limited liability companies owners wanakuwa separated na kampuni mpaka hapo mahakama itakapo amua Ku lift corporate veil (hii nayo inataratibu zake tens ndefu tuu) ndio owner anaweza kufika mahakamani kujibubtuhuma za kampuni...

Hili limenishangaza hata kwa kesi za max melo na mmiliki mwenzake wa jii forums, walivyotunga Companies Act walidhani ni ya mapambo, hawawezi kujisomea?

Chuki na visasi havitakusaidia kifanya nchi iendelee, serikali ingejitungia sera ya No retaliation kwa ajili ya wananchi wake, ikikosolewa isiweke vinyongo chuki na visasi hii nchi ni yetu sote
 
Back
Top Bottom