TRA yamdai Profesa Tibaijuka Sh500M za ESCROW, apinga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Hatima ya kesi ya Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kupinga kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh500 milioni kutoka katika mgawo wa Sh1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa Akaunti ya Tegeta Escrow, itajulikana Machi 29, wakati Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) itakapotoa uamuzi.

Tarehe hiyo imepangwa na Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbando baada ya kukamilika kwa hatua ya usikilizwaji pande zote mbili kwenye kesi hiyo.

Profesa Tibaijuka alikata rufaa Trab baada ya TRA kumpelekea madai ya malipo ya kodi ya Sh586 milioni kutokana na mgawo wa Sh1.62 bilioni anazodaiwa kupokea kutokana na fedha zilizochotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni ya kufua nishati hiyo ya IPTL kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya ununuzi wa umeme wakati mzozo wao ukiwa mahakamani, lakini zikachotwa kwa njia ambayo ilizua shaka. Rufaa hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa Tibaijuka alipokuwa akitoa ushahidi.

Inadaiwa kuwa Profesa Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.

Kutokana na mgawo huo, Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.

Hata hivyo, alipinga madai hayo na kisha akakata rufaa Trab kupinga hatua ya TRA kumtaka alipe kiasi hicho cha kodi, pamoja na mambo mengine akidai kuwa hajawahi kupokea fedha hizo kutoka kwa Rugemalira.

Katika rufaa hiyo namba 22 ya mwaka 2015, Profesa Tibaijuka anadai kuwa makadirio hayo ya TRA ya malipo ya kodi ni kinyume cha Sheria ya Kodi na hakupaswa kufanya marejesho kwa kuwa hakupokea kipato chochote katika muda huo uliotajwa.

Akiongozwa na wakili wake, Dk Nshalla Rugemeleza wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Profesa Tibaijuka alidai kuwa fedha hizo zilikuwa ni mchango uliotolewa kwa Taasisi ya Joha Trust, kwa ajili ya Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson inayomilikiwa na taasisi hiyo.

Profesa Tibaijuka alidai kuwa yeye si mwanahisa wa taasisi hiyo, bali ni mmoja wa wadhamini na kwamba TRA ilipuuza ushahidi wake kuwa VIP ilitoa mchango kwa Joha Trust na yeye kama mdhamini alizipeleka Joha Trust kupitia Bank M.

Aliongeza kuwa TRA haikuzingatia ukweli kwamba Joha Trust na yeye ni vitu viwili tofauti, huku akisisitiza kwamba fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya Joha.

Hata hivyo, wakili wa TRA, Noah Tito ilipinga madai ya Profesa Tibaijuka akidai kuwa utetezi wake hauna msingi kwani fedha hizo ziliingia kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka na siyo ya Joha Trust.

Chanzo: Mwananchi
 
Hatima ya kesi ya Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kupinga kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh500 milioni kutoka katika mgawo wa Sh1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa Akaunti ya Tegeta Escrow, itajulikana Machi 29, wakati Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) itakapotoa uamuzi.

Tarehe hiyo imepangwa na Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbando baada ya kukamilika kwa hatua ya usikilizwaji pande zote mbili kwenye kesi hiyo.

Profesa Tibaijuka alikata rufaa Trab baada ya TRA kumpelekea madai ya malipo ya kodi ya Sh586 milioni kutokana na mgawo wa Sh1.62 bilioni anazodaiwa kupokea kutokana na fedha zilizochotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni ya kufua nishati hiyo ya IPTL kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya ununuzi wa umeme wakati mzozo wao ukiwa mahakamani, lakini zikachotwa kwa njia ambayo ilizua shaka. Rufaa hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa Tibaijuka alipokuwa akitoa ushahidi.
 
Na kwa ilivyo Tanzania....

Prof Tiba lazima ashinde....afu sasa utasikia anaidai serikali...
 
Kuna wakati mwingine unaona hii dhana ya majipu haian mantiki, why not huyu mama na kina chenge na muhongo wasisitishiwe ubunge wao kwa kuwa ni majipu, wachaguliwe watu wengine wasafi? Hawa wangekuwa wametoka upinzani wangesakamwa ndani ya ubunge mpaka ulimwengu uwajue. Ila kwa kuwa ni ccm na chenge kapewa cheo ndani ta bunge, eti tunatumbua kha.
 
HATA HIVYO KODI NI KUBWA MNO.! ZAIDI YA 30%! MJADALA JUU YA KUSHUSHWA KODI UNAHITAJIKA.! MADINI YOTE,! GESI YOTE,! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA,! MLIMA KILIMANJARO! NK BADO WATANZANIA WANATOZWA KODI KUBWA KWA LENGO LA KUKIDHI BAJETI YA NCHI.! NAOMBA NIELEWEKE, "SITETEI MGAO WA ESCROW". ILA KODI IMEZIDI!
 
Haweze kushinda , hela iliingizwa kwenye account yake yani personal account na sio kwenye account ya shule kwanini? arafu msaada ulikuwa wanini ili mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali akakague .
 
Mkuu
HATA HIVYO KODI NI KUBWA MNO.! ZAIDI YA 30%! MJADALA JUU YA KUSHUSHWA KODI UNAHITAJIKA.! MADINI YOTE,! GESI YOTE,! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA,! MLIMA KILIMANJARO! NK BADO WATANZANIA WANATOZWA KODI KUBWA KWA LENGO LA KUKIDHI BAJETI YA NCHI.! NAOMBA NIELEWEKE, "SITETEI MGAO WA ESCROW". ILA KODI IMEZIDI!

Hata mimi nimeshangaa sana, yaani wanakata kodi inayo karibia nusu ya mapato!
 
Mbona Wale Wengine Hatuwasikii Wakidaiwa Hiyo KODI!!!?? Au Kuna Wanaotakiwa Kulipa Na Wengine Hapana!!!! Maana Wako Wengi Na Wale Walichukua Kupitia STANBIC BANK, Hadi Leo WAMEFICHWA Tu!!!
 
Kuna wakati mwingine unaona hii dhana ya majipu haian mantiki, why not huyu mama na kina chenge na muhongo wasisitishiwe ubunge wao kwa kuwa ni majipu, wachaguliwe watu wengine wasafi? Hawa wangekuwa wametoka upinzani wangesakamwa ndani ya ubunge mpaka ulimwengu uwajue. Ila kwa kuwa ni ccm na chenge kapewa cheo ndani ta bunge, eti tunatumbua kha.

MODS nashauri unitafutie heading ya hii mada uiweke kama uzi mpya watu wajadili:

Mkuu mimi naunga mkono hoja yako. Lakini wakati mwingine nauliza hawa ndg zetu wapinzani wanaogopa nini kuibua mambo kama haya bungeni? ili serikali iwawajibishe watendaji wabovu inahitaji wapinzani imara na wasiokuwa waoga kuibua hoja hatakama zinagusa maslahi ya watawala.

Wana JF mtakumbuka kipindi wapinzani walipoibua hoja ya ESCROW hata wanachama wa chama tawala waliungana bila kujali chama waliangalia maslahi ya nchi.

Ilifika mahali Yule mama Speaker aliyekuwa akitetea chama chake na kuficha udhaifu wa serikali akathubutu kusema. "Hebu we fulani kaa chini kwanza tumsikilize Mh.Halima mdee na Mh.Tundu Lissu huwa na waamini sana hawa wamebobea kwenye mambo haya ya sheria.eenhe Mh.Lissu tuandikeje hapa......." tena aliyeambiwa akae chini ni mbunge wa chama chake tawala. Tutamkumbuka sana"Tumbili" Yuko wapi Mh.aliyekuwa wa ubungo siku hizi kibamba? Naona siku hizi kimyaa...!

Kuna mambo ambayo kwa mtu mwenye akili timamu ukiyafikiria yanauma sana.
1.Eti mtu anajulikana wazi anatuhuma zaidi ya moja
i.Rada
ii.Ndege aina ya jet ya Rais wa awamu ya tatu
ii.Richmond
iv.Sakata la kukutwa na fedha nyingi huko bank-uswis
v.Kudharau watanzania wote na kusema pesa yote hiyo aliyonayo huko nje ni "vijisent tu".wakati watu wanashinda na njaa wanakula mlo mmoja tu ugali haragwe jioni
vi.ESCROW
Vii.Kuwadharau watanzani tena hadharani kusema kuwa yeye ni "nyoka wa makengeza"
vii.Kuigomea kamati ya maadili kumhoji kwa kuweka pingamizi kwa tuhuma za wazi kama mtumishi wa umma kupokea pesa nyingi vile bila kuzitolea maelezo wala taarifa.

Leo mtu huyu ni ndiye pekee anayefaa kukaa mbele ya Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuliongoza kama mwenyekiti.Aidha amepitishwa na chama chake kuwa yeye ni msafi hivyo alikidhi vigezo na kupita kura za maoni wale aliyokuwa nao akawashinda ndiyo sio wasafi. Wapinzani wako kimya

2.Mwingine akiwa kama mjumbe wa Bodi ya mamlaka ya bandari, mshauri na msaidizi wa maswala ya sheria na kutajwa kuwa amebobea sana kwa maswala ya kisheria,ameshindwa kuishauri bodi na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya pesa ,kiasi cha kumuudhi RAIS wetu mpendwa na mchapakazi kuivunja bodi hiyo na kuagiza office ya IGP na TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina juu ya wajumbe hao wakiongozwa na Prof.Msambijungle

Japo hatuja taarifiwa uchunguzi huo umefikia wapi,na inakuwaje uchunguzi unafanyika na wengine wameachwa na nyazifa zao kubwa sijui watahojiwaje? mgongano wa kisheria wajuzi wa mambo haya waje kutuelimisha ma "layman" Wapinzani wapo kimya.

Mimi najua pamoja na shughuli nyingine za maendeleo kazi ya wa pinzani ni pamoja na kuikosoa serikali pale inapofanya mambo double standard,Kuikosoa serikali sio kosa kosa ni kutukana,hawa watu wanatuhuma kunahaja gani nchi kuongozwa na watuhumiwa? inamaana kwenye chama chetu tawala hakuna watu wasafi mpaka mpate shida ya kusafisha?

Mbona wapo watu wazuri na wasafi sana huko kwenye chama tawala mmewatelekeza? KWANINI MSAFISHE HAO WATU WACHACHE WENYE TUHUMA NA KULAZIMISHA WANANCH TUWAKUBALI KUWA NI WASAFI WAKATI MAMBO YOTE WALIYOYATENDA YALIRUSHWA MCHANA KWEUPE KWENYE MEDIA? Waliotuhumiwa tuhuma ya escrow wapo wengi na baadhi wamerudishwa serikalini na kupewa nyadhifa kubwa tu. Kama mlikosea bunge linaendelea mwezi appril serikali jirekebisheni na pia wapinzani chukueni hatua.
 
Duh, huyu bibi ana roho ngumu kweli!!! Pesa ilipita kwenye account binafsi halafu anadai haikulipwa kwake?
 
ILI RAIS MAGUFULI ADHIHIRISHE KUWA SI MNAFIKI BASI ANAPASWA:-

-Kuwafutia CHENGE,TIBAIJUKA NA NGELEJA UONGOZI WALIO NAO.

Hayo ndio Majipu anayopaswa kuyatumbua na sio kuwasakama watu wadogo na wapinzani tu.
 
HATA HIVYO KODI NI KUBWA MNO.! ZAIDI YA 30%! MJADALA JUU YA KUSHUSHWA KODI UNAHITAJIKA.! MADINI YOTE,! GESI YOTE,! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA,! MLIMA KILIMANJARO! NK BADO WATANZANIA WANATOZWA KODI KUBWA KWA LENGO LA KUKIDHI BAJETI YA NCHI.! NAOMBA NIELEWEKE, "SITETEI MGAO WA ESCROW". ILA KODI IMEZIDI!
Kwa kweli ni kodi kubwa sana. Tena pamoja na kodi hizo zinazotozwa kwa lazima, lakini bado wananchi wanaambiwa tena wakati mwingine kwa kulazimishwa watoe pesa eti kuchangia maendeleo.
 
Back
Top Bottom