TRA yakamata mifuko 400 ya sukari ya magendo

Majs

Senior Member
Dec 21, 2012
190
500
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata mifuko 400 ya sukari iliyokuwa ikisafirishwa kwa magendo.

Taarifa ya mamlaka hiyo imesema mifuko hiyo ya sukari ya kilo 50 kila mmoja imekamatwa usiku wa kuamkia jana, Agosti 26 ikiwa imepakiwa kwenye magari mawili aina ya Mitsubishi Fuso.

TRA imesema hatua hiyo ni mwendelezo wa kampeni yake ya kukamata magendo, kazi inayofanywa na kikosi chake maalumu cha Fast kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama.

Mamlaka hiyo imesema mzigo huo na watuhumiwa wa magendo wanaodaiwa kuwa ni sugu wamekamatwa eneo la Bagamoyo mkoani Pwani.

Taarifa imesema magari hayo ya mizigo yanashikiliwa katika ghala maalumu la TRA kwa hatua za kisheria, ikiwemo kuyataifisha.

Imeelezwa mzigo huo ni wa hatari kwa kuwa hauna vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

TRA imewaomba wananchi kutoa taarifa za vitendo kama hivyo ili kukomesha dhuluma kwa nchi na uwezekano wa afya zao kudhurika.

CHANZO: Mwananchi
 
Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,157
2,000

sukari wachukue na gari wachukue, duu, hii kweli Tanzania
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,734

Wafirisiwe tu ili wapate akili
 
mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
3,936
2,000
Wabomoleshe iyo sukari kama walivyowabomolesha wale vifaranga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom