TRA yafunga maduka Iringa

TRA yafunga maduka Iringa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
tra.jpg


Iringa. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefunga maduka ya wafanyabishara wasiotumia mashine za kielektroniki za EFD.

Hatua hiyo imekuja baada ya maofisa wa TRA kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa na kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaodaiwa kutokuwa na mashine za kutolea risiti za EFD.

Akizungumza na gazeti hili leo Jumanne, Julai 25 Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Lampson Tulianje amesema wafanyabishara hao wamekaidi agizo la Serikali la kutakiwa kuwa na mashine kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

“Tumewapa maagizo, tumewahamasisha kwa zaidi ya miezi mitatu lakini bado wamekaidi agizo letu, uamuzi tuliochukua ni kufunga duka na mara atakaponunua tunamfungulia duka lake,”amesema Tulianje.

Tulinje amefafanuaa kuwa lengo la kufikia hatua hiyo ni kuhimiza wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki kwa kutumia mashine hizo ambazo zina uwezo wa kuweka kumbukumbu vizuri za mauzo ya bidhaa zao.

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuacha kushindana na Serikali badala yake kuhakikisha wananunua mashine hizo na kuzitumia kwa kuwa hata gharama wanazotumia zinarudishwa na TRA wakati wa kukadiria kodi zao.

“Rai kwa wafanyabiashara ni vyema wakanunua mashine zitakazosaidia kuweka vizuri kumbukumbiu za mauzo yao na kuisaidia Serikali kukusanya kodi sahihi, zaidi yote mashine hizo zinatolewa bure na TRA kwa kuwa gharama wanazotumia kununulia mashine zitaunganishwa kwenye makadirio ya kodi yao ya mapato,”amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabishara mkoani hapa, Odilo Ngamiraga amesema wafanyabishara hawajagoma kutumia mashine hizo na kwamba tatizo lipo kwa wasambazaji ambao pindi wanapokwenda huambiwa wasubiri.

Chanzo; mwananchi
 
Wangewapa basi mda kidogo sababu ya hao wasambazaji wa hizo mashine aisee
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabishara mkoani hapa, Odilo Ngamiraga amesema wafanyabishara hawajagoma kutumia mashine hizo na kwamba tatizo lipo kwa wasambazaji ambao pindi wanapokwenda huambiwa wasubiri.[/QUOTE]
Hapo kwenye bold ndio ninapo chokaga kabisa; uzembe wa mtu mwingine athari zinaenda kwa mtu asiyehusika; hivi hakunaga sheria ya kuadhibiwa huyu anayemsababishia mtu mwingine matatizo!?
 
Bado kodi ya kichwa tu haijaanza!

sent from my land lover 109 using Jamii forums app
 
Sasa kama machine zipo siwawape tu bure
Ili la kusema ununue kwanza alafu watakatana kwenye kodi kidogo kidogo,uwa hata siwaelewagi au huu ni mradi wa mtu
Kama machine ni mali ya serikali gaweni bure hizo machine.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da mashine mashine wengine capital na efd efd iko juu kuliko mitaji yetu.
 
Wamewaacha MAPAPA wa MAKINIKIA wakitumbua na helikopta, kazi Shinyanga, lunch Hyatt Regency DAR ES SALAAM, then wanarudi Shinyanga, na usiku wanaenda kulala Hyatt!

EBOOO!

@TRA mkoje? Yaani mnanyanyasa WENYE NCHI na kuwaacha MAFISADI-MAKINIKIA wakitumbua na kutugeuza SHAMBA LA BIBI?

Nyieeee! Mungu anawaonaaaa!
 
Back
Top Bottom