Naunga mkono sheria nyingi za Kodi ni kandamizi, TRA ni watekelezaji tu wakulaumiwa ni wawakilishi wetu bungeni waliotunga na kupitisha sheria hizo.Pitieni upya sheria za Kodi ziwe rafiki kwa pande zote mbili.TRA wakiamua kusimamia sheria ipaswavyo ni vilio na kusaga meno kwa walipa kodi.Tatizo ni sheria za kodi haziko rafiki. TRA siyo makosa yao. zipitiwe.
Baadhi ya maofisa wa TRA vinara wa Rushwa hutumia Sheria zao binafsi kufunga Account za wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani watengeneza mazingira ya Rushwa au kumkomoa mfanyabiashara kwa wivu chuki endapo atagoma kutoa RushwaTatizo ni sheria za kodi haziko rafiki. TRA siyo makosa yao. zipitiwe.
Ni kweli, tunajua Wabunge na viongozi waandamizi wanapitia humu JF, hasa uzi huu.Naunga mkono sheria nyingi za Kodi ni kandamizi, TRA ni watekelezaji tu wakulaumiwa ni wawakilishi wetu bungeni waliotunga na kupitisha sheria hizo.Pitieni upya sheria za Kodi ziwe rafiki kwa pande zote mbili.TRA wakiamua kusimamia sheria ipaswavyo ni vilio na kusaga meno kwa walipa kodi.
Serikali ilibidi ianzie kwenye umiliki wa mali za wafanyakazi wa tra na polisi wa usalama barabarani,maana hizi ndio sehemu sugu ambazo bado zinapokea rushwa bila wogaWatumishi wengi wa TRA wanamiliki mali majumba kinyume na vipato vya halisi
Sheria zifanyiwe uchunguzi.Serikali akazie humo humo kwani bado wapo wafanyakazi wengi siyo waaminifu wanaendelea kuwasumbua wafanyabiashara TRA inanuka Rushwa na ubadhirifu wa pesa za walipa kodi
Waanze na mali majumba ya watumishi wa TRA kwanza kabla ya kwenda popoteTrillion 2 kwa mwez sio mchezo, acha wafukue makaburi wanaweza pata hata mifupa ikawaongezea kidogo
Biashara yako ikifungwa jua ulikuwa na mapungufu hakuna mtu atakurupuka kuja kukufungia biashara yako wakati hakujui wala hajawahi kukuona. Tuache mazoea tujifunze kulipa kodi kwa maendeleo ya woteTunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.
TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.
TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.
Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.
Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.
UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.
Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.
Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.
Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba
Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.
Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.
Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.
Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.
Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.
USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
YATOKANAYO-UPDATE
====================
Asante sana Waziri Mpango kwa kulifuatilia hili lalamiko na kutoa maagizo ya kutatua kero hii.
View attachment 1652089
Soma mada na uielewe.Biashara yako ikifungwa jua ulikuwa na mapungufu hakuna mtu atakurupuka kuja kukufungia biashara yako wakati hakujui wala hajawahi kukuona. Tuache mazoea tujifunze kulipa kodi kwa maendeleo ya wote
Unadhani wanafanya bila maelekezo?Nashauri; TRA wachunguzwe juu ya uhalali wa kodi zao. Kesi zimekuwa nyingi siku za hivi karibuni.
Umewaza kijinga sana....anaekuajiri akipigwa mikodi atakulipa niniKwa hiyo sasa hivi bora kuajiriwa tu, si ndio?
Walisha toa tamko kiwanja chochote kilicho pimwa hakilipiwi mapato kitauzwa na kufidia deni koo tusubilie mda ufike, trillion 2 sio mchezo kwa mweziWaanze na mali majumba ya watumishi wa TRA kwanza kabla ya kwenda popote
umejibu kijinga pia, vipi km nmeongelea utumishi hapo!?Umewaza kijinga sana....anaekuajiri akipigwa mikodi atakulipa nini
Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
sijamaanisha mzee hiyoUmejuaje ni mzee?
Acha ufala wako wengi wamefungiwa biashara ni walipa kodi wazuri wana Tax Clearence safi lakini vinara wa Rushwa wakifika hutengeneza mazingira ya kufanya ukaguzi juu ya ukaguzi wa awali na usipokuwa makini wanakubambikia VAT ya ajabu ajabu kuwa wakikupa vitisho vya kesi za uhujumu uchumi utakatishaji fedha, Uonevu upo acha kutetea unyanyasaji wa kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetaniBiashara yako ikifungwa jua ulikuwa na mapungufu hakuna mtu atakurupuka kuja kukufungia biashara yako wakati hakujui wala hajawahi kukuona. Tuache mazoea tujifunze kulipa kodi kwa maendeleo ya wote
Hicho si kigezo cha kwenda kupora watu pesa zao kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetaniWalisha toa tamko kiwanja chochote kilicho pimwa hakilipiwi mapato kitauzwa na kufidia deni koo tusubilie mda ufike, trillion 2 sio mchezo kwa mwezi
Sidhani km kuna kitu hakijulikani. Lkn tra wanalaumiwa bure wao wanatekeleza maagizo kutoka juu lkn lawama wanabeba wao..... Umewahi kuona rais anawakemea na kuwachukulia hatua?TRA waundiwe Tume kali ya wataalam hata wa kukodi tokea nje wawahoji wafanyabiashara vizuri kwa umakini mkubwa kubaini udhaifu wa watendaji wa TRA