TRA: Wanaofanya biashara mitandaoni kuanza kutozwa kodi

TRA: Wanaofanya biashara mitandaoni kuanza kutozwa kodi

kuna siku tutatakiwa ukiamka tuu... unalipa kabisa kodi alafu ukirudi jioni unapiga hesabu kama hujafanya chochote cha kuzalisha unatunziwa hela yako (tax withholding sijui inaitwa)
 
kuna siku tutatakiwa ukiamka tuu... unalipa kabisa kodi alafu ukirudi jioni unapiga hesabu kama hujafanya chochote cha kuzalisha unatunziwa hela yako (tax withholding sijui inaitwa)
YERIKO NYERERE UMESHAONWA NA VITABU VYAKO
 
Jumia, Kupatana, Be Forward wote wana leseni wanazilipia vile vile wanalipa kodi ya mapato TRA, tena TRA wanataka walipie mitandao yao, hii sasa siyo double taxation ni triple taxation.
Sio kama natangaza biashara hapana ila nimeweka tu kutoa uhalisia..!! Angalia mtu kama huyu ata anakuambia anakuletea ulipo unafikiri huyu TRA isijue kinachoendelea nini?
 
Serikali imesema wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mapato Tanzania TRA ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanya biashara wengine wote.

"Watu wote wanaofanya biashara mitandaoni ni lazima wajiandikishe ili wapate namba ya mlipakodi (TIN), kama wamekidhi vigezo. TRA tumeanza kuwafuata wanaofanya biashara mitandaoni ili walipe kodi, hivyo niwatake wajitokeze waje wajiandikishe."- Kamishna Mkuu TRA, Charles Kichere.

Wanaofanya biashara mitandaoni kuanza kutozwa kodi

My Take:

1. Chungu kinazidi kupungua, baada ya wamachinga wa barabarani zamu ya wamachinga wa mitandaoni wanaouza simu used, keki, nguo, sandals mitandaoni.

2. Tumesahau viwanda?

Waziri wa Fedha: Nchi inapita kwenye kipindi kigumu, wafadhili wamepunguza misaada
Itabidi wale wafanyabiashara wadogo wa mitandaoni wakaombe vitambulisho vya mkulu waweke nakala mtandaoni wanakouzia bidhaa zao.
 
Jumia, Kupatana, Be Forward wote wana leseni wanazilipia vile vile wanalipa kodi ya mapato TRA, tena TRA wanataka walipie mitandao yao, hii sasa siyo double taxation ni triple taxation.
Hoja nzuri.
 
Nnavyojua mm na kwa uzoefu ni kuwa ukiagiza kitu mathalan toka alibaba ama ebay kinapokelewa posta ama dhl ama ups pale wanakukokotolea gharama ambayo unatakiwa ulipe kama kodi. Baada ya hapo ukiiweka bidhaa hewani kama ZoomTanzania ama kupatana inabidi umalizane tena na TRA? Embu wenye ujuzi mtuelimishe zaidi…
 
kuna siku tutatakiwa ukiamka tuu... unalipa kabisa kodi alafu ukirudi jioni unapiga hesabu kama hujafanya chochote cha kuzalisha unatunziwa hela yako (tax withholding sijui inaitwa)
Daaah we jamaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
MTAJENGA SGR na STG GEORGE KWA MENO
HALAFU SIFA KWA MHAMIAJI WA 1960's KUTOKA RWANDA
 
Serikali imesema wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mapato Tanzania TRA ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanya biashara wengine wote.

"Watu wote wanaofanya biashara mitandaoni ni lazima wajiandikishe ili wapate namba ya mlipakodi (TIN), kama wamekidhi vigezo. TRA tumeanza kuwafuata wanaofanya biashara mitandaoni ili walipe kodi, hivyo niwatake wajitokeze waje wajiandikishe."- Kamishna Mkuu TRA, Charles Kichere.

------------
Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere leo asubuhi alipokuwa akizungumza kupitia Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza mapato.

Kamishna Kichere amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji kuhusu uwepo wa watanzania wachache wanaolipa kodi (zaidi ya milioni 2) wakati jumla ya Watanzania wapo takribani milioni 55.

Akizungumzia mkakati wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi, kamishna huyo amesema wameanza kuwafikia watu wanaofanya biashara mitandaoni ambao wamekidhi vigezo vya kutakiwa kulipa kodi, wawe wanalipa kodi kama wafanyabiashara wengine.

Ameeleza kuwa, wafanyabishara ambao thamani ya biashara zao ni zaidi ya shilingi milioni nne wanatakiwa kufika TRA wajiandikishe ili wapate Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) waanze kulipa kodi.

Ametahdharisha kuwa, tabia ya wafanyabiashara kulipa kodi inaweza kuwasababisha matatizo ikiwamo malimbikizo ya kodi ambayo yanaweza kupelekea biashara zao kufungwa, hivyo ni vyema wakalipa stahiki hizo kwa wakati.

Mbali na kuwafikia wanaofanya biashara kwenye miatandao, Kamishna Kichere amesema kwamba wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi, ili wafahamu umuhimu wa kulipa kodi na waone kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo bila kusubiri kushurutishwa.

Wanaofanya biashara mitandaoni kuanza kutozwa kodi

My Take:

1. Chungu kinazidi kupungua, baada ya wamachinga wa barabarani zamu ya wamachinga wa mitandaoni wanaouza simu used, keki, nguo, sandals mitandaoni.

2. Tumesahau viwanda?

Waziri wa Fedha: Nchi inapita kwenye kipindi kigumu, wafadhili wamepunguza misaada
hatupo mbali sana..naona kila mtu anakaribia kufikiwa na bwana pepsi...nafikiri hizi kauli za "chadema hao" au "wanatumiwa na mabeberu" au "kazi yao kupinga kila kitu" zote tutaacha kuzisema na tutaimba wimbo mmoja juu...yumkini kiitikio kikawa "******** out"...time will tell
 
Sijajua watatumia vigezo gani lakini hawa jamaa wanaofanya biashara mtandaoni wengine wanamaduka maeneo ya sinza na kariakoo ambayo tayari yanalipiwa kodi so kule huwa wanafanya kama matangazo tu!!Labda wana aproach nzuri ya kuwapata hao wafanyabiashara wa mtandao!!Ngoja tuone itakavyokuwa ingawa hawa jamaa wenye biashara mtandaoni wanapata faida nyingi kwa gharama ndogo ya bando ambayo itamsaidia kuweka tangazo lake mtandaoni
 
Sio kama natangaza biashara hapana ila nimeweka tu kutoa uhalisia..!! Angalia mtu kama huyu ata anakuambia anakuletea ulipo unafikiri huyu TRA isijue kinachoendelea nini?

Mimi ni mzoefu wa biashara za mitandaoni, ukute aliyeweka tangazo au picha hizo hana mtaji hana hata kijiko cha kuuza ni mali kauli tu, anategemea umpigie simu yeye aweke cha juu akachukue dukani kwa mhindi kariakoo, au anategemea kamisheni.

Binafsi nilinunua TV yangu online, nilipomwambia aniletee akasema nitume nauli, nikamwambia situmi hadi nitakapoiona, basi akanielekeza duka lilipo kariakoo, nilipoenda nikanunua dukani kwa bei ya chini zaidi, jamaa akanieleza ukweli kuwa yeye ni dalali tu nikampoza kwa 20.

Ndiyo maana nasema kama serikali imeshindwa kuwaajiri vijana iwaache wajiajiri, hawa vijana wakiwemo wa mitandaoni hawana mitaji kama wanavyofikiria, kuzidi kuwakamua ni kuua maisha yao.
 
Serikali imeshindwa kuandaa watu ili waweze kupata kodi kwao na badala yake sasa ni kutafutana ubaya tu.

Serikali zote duniani zinazoongozwa na watu wenye akili huwatengenezea wananchi wao mazingira mazuri ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kuwaandalia utaratibu wa kupata mikopo kwa riba ndogo na ndipo serikali hutoza kodi ndogo.

Lkn kwa mkakati huu wa akina Kichere wa kutaka tu kukamua ng'ombe bila kumlisha sidhani kama utafaulu. Pale makusanyo yao yalipofikia hayatavuka hapo sana sana yatapungua tu kwa sababu serikali yenyewe imekuwa mzigo kwa matumizi mabovu ya kodi kama kununulia wabunge na madiwani.
 
sasa sisi tulio na mtaji usiozidi laki mbili tukatwe na kodi pia? na wakati huohuo hizo bidhaa ulizonunua zimeshakatwa kodi...? asalaaalee
 
Hahaha watanzania tunavituko sana, eti hata wale waliounga mkono juhudi za rais nao wanalalamikia kodi huku kwenye mutandao. Kweli mchana inzi usiku mbu.
 
Back
Top Bottom