TRA wanaboa ile mbaya

umeanza lini kumiliki gari? au mwaka gani? hujawahi kuwaona maofisa wa tra na gari zao wanakamata road licence barabarani? na mara nyingine tena sana wanawatumia wale majembe auction mart wanajipanga njia panda ya changombe kama unatokea airpot na ile njia ya kwenda buguruni na sehemu nyingine nyingine nyingi tu . labda kama hupiti hizi barabara za chini. harafu unasema police walikueleza suala la receipt za kufoji sasa kama ulikuwa na receipt halali why uogope kwenda police wakati ingehakikiwa na ingegundulika ni ya halali. na ungeweza kutoa malalamiko yako ya kupotezewa muda. na usingepoteza hela zako kulipa hiyo faini. harafu swali la mwisho hiyo faini waliyokulipisha police iliandikwa nini na ulilipa sh ngapi? otherwise basi wewe ndio utakuwa mmiliki wa kwanza asijua hata sheria ndogo za magari
 
Ni kweli kuchukua sticker ni siku ya pili tangu kulipia, nenda TRA Mwenge utakuta huo utaratibu labda na kwingineko. Polisi hatakiwi kukupiga faini kwa kukosa road licence kwa kuwa utapigwa faini na TRA ukienda kulipa kama siku zimepita otherwise kwa kosa moja utaadhibiwa mara mbili. Pia jukumu la kujua risiti au road licence fake si la Polisi au Majembe bali Ofisa wa kodi ambaye atakuwa assigned kuwepo katika zoezi la ukaguzi.
 

Ubishi mwingine hauna maana.Jamaa hana nia ya kujitangaza kwamba ana gari ni anaelezea usumbufu anaoupata!utaratibu mpya wa TRA ni huo,ukilipa leo unatoa copy ya bank slip unawaachia ile original then unarudi kesho yake kuchukua sticker yako.ukilipia ijumaa ni mpaka J3 ndio unakamatia sticker.matraffic wote wanalijua hili ila kwasababu ya njaa zao kali hupenda kitingisha kibiriti hasa kwa madereva wengi vijana na wamama ma kuwachomoa chochote.
 
kumiliki gari ni ufaharie?ukutangazie un amjua hivi hata akisema ana ari kumi unamfahamu?
 

Mkuu sio Temeke tu hata Samora pia ni hivyo hivyo !
 
As tulivyokubaliana na ndivyo ilivyo kuwa road licence ni issue ya tra . Je huyu ndugu walimwandikia kitu gani hao polisi anaosema wamelipisha faini?
 

Hao Police walikosea kukataa risiti yako kwa kigezo cha risiti za kufoji. Katika ulimwengu wa leo watu wanafoji sana hizo sticker kuliko risiti. Na swali jepesi Ni kwamba, kama wanaweza kufoji risiti watashindwa nini kufoji sticker ambayo ndiyo muhimu kwa garish? Pole sana. Hata hivyo polisi hawakutumia busara ya kawaida tu kwenye kukudai ulipie faini. Ila na wewe kaka umetuangusha kwa kukubali kirahisi na kulipia kitu ambacho naamini hata risiti hukupewa. Ni bora ungekubali usumbufu kidogo wa Kendal polisi lakini ungesaidia kukomesha jambo hili.
 
great thinker hafikirii au kusikiliza maelezo bila kuyafanyia kazi. Tusiwe wavivu wa kufikiri..... Hivi niende tra lets say nilipie road licence tena na faini juu. Harafu natoka hapo naingia barabarani na receipt ninazo eti nakamatwa na polisi na katika maelezo yao eti nakubali kulipa tena????????? Am i a great thinker??????
 
Great thinker, why cant you discuss the root of the problem, instead you keep on discussing the resulting outcomes of the problem?
 

Wewe nae sijui umeajiriwa TRA mwaka huu!!!!!? mbona unarukia suala la polisi na faini na
unaacha main point ya mleta mada juu ya usumbufu wa kupata sticker za road licence na ujinga
mwingine wa kulazimishana kuuziana sticker za fire?TRA na fire wapi na wapi.Acha kutetea ujinga
na udhaifu kubali ukweli ili uiponye TRA yenu kama unaweza ebo!!!!!!!!!
 
Mi nasubiri utawala mpya utakao badilisha uozo wa heruf "T" katika nch hii ya Wadanganyika.
T R A
T anesco
T RL (RAILWAY).
Agghhhh!! Na haka ka TiGO nakafkiria kukafanyia maamuzi.
 

Umenena kaka. Mabadiliko ya maisha ya watanzania yako mikononi mwao. Lazima tubadilishe mienendo ya maisha yetu ya kila siku.
 
.

Umeshindwa kutambua haki yako ya msingi kabisa well ukilipa unapewa risiti meaning that ile risiti ni kithibitisho kwamba umelipa na trafiki yoyote haruhusiwi kukusumbua kwa sababu kodi ya serikali umeshalia...La msingi kama ni feki nani anatakiwa aseme?mnawalea sana hao Polisi sasa wanawasumbua kuna sheria maalum ya magari ambayo ni MotorVehicle Registration and Relicensing Act ambayo inasimamiwa na TRA je Polisi wako hawalitambui hii...Acha Uoga wewe tembea na gari lako...Unapaswa kujua haki zako za msingi na sio kukubali makosa tu...
 
Thanks mkuu kwa kunisaidia. Hawa ndugu zangu hawajui mazingira niliyokuwa nayo jana hadi nikalazimika kumpa polisi kilicho chake. Lakini mimi sijawalalamikia polisi. Nawalalamikia TRA, maana kama TRA wangenipa sticker yangu polisi wangenikamata kwa lipi? Lakini akina kupe wameacha kujadili suala la TRA wanajadili suala la polisi bila kujali nilibanwaje hata nikakubali kulipa.
 
Last edited by a moderator:

Huo utaratibu ndo unatumika sana na TRA mie siku zote sijawahi kwenda kulipia road licence na kupewa siku hiyohiyo, ila kinachofanyika ni kuwa ile form inayotumika kulipia bank ambayo ni ya TRA, pamoja na copy ya malipo uliyofanya bank, unaachiwa hadi siku utakapo enda kuchukua sticker yako. Ni ukweli usiofichika pale TRA wanasumbua sana kwa mtu anaejipeleka kulipa kodi hilo mie nilishaliona siku nyingi.

Kuhusu Police kumkomalia inawezekana kabisa yeye baada ya kusumbuliwa TRA aliposimamishwa na traffic police hakuwa na kauli ya kiungwana nao wakaamua kumkomesha; Tukumbuke police nao ni watu na wanasikiliza kama utajieleza vizuri bila nyodo ila ukijidai much know utawakoma hao ndo police wetu.

Huyu ndugu yetu hivi kweli aliona ugumu gani kupeleka gari police halafu akaiacha huko akisubiri hiyo sticker, na kama alitoa pesa kwa ajili ya faini, hiyo risti ya serikali iliandikwa kosa gani? au labda alikutwa na makosa mengine?
 
Huyu ndugu anachoelezea si kweli hakuna kusubiri kupata sticker ni kama alivyosema mchangiaji hapo juu
huyu bwana naona hajui taratibu sio kweli kabisa anatafuta umaarufu tu. Hizo ni story za vijiweni huko aache mambo yake ya kitoto.
 
Ngoja nirudi nikaangalia kosa waliloandika kwenye list ya faini maana jana nilikuwa na hasira kupita maelezo. Kuhusu kupeleka gari polisi lilikuwa ni suala gumu sana, humo kwenye gari nilikuwa na mizigo ninayoipeleka nyumbani halafu nipo na familia. Ndiyo maana nasema watu waacha kujadili faini niliyolipa, wajadili source ya tatizo ambayo ni TRA. Maana huko kwenye faini naamini yule polisi alikuwa na njaa zake tu. Maana alikuwa anakomalia mambo ya kijinga kabisa. Wala siwafichi polisi walionikamata ni wale wa Ukonga Banana. Nasikitika tu kwamba sikumpiga picha labda ningeiweka hapa ili mmujue kabisa polisi aliyeniharibia siku yangu ya jana.
 
Huyu ndugu anachoelezea si kweli hakuna kusubiri kupata sticker ni kama alivyosema mchangiaji hapo juu
huyu bwana naona hajui taratibu sio kweli kabisa anatafuta umaarufu tu. Hizo ni story za vijiweni huko aache mambo yake ya kitoto.
ha ha ha, wee jamaa una matatizo sana, mimi nitafute umaarufu kwako, unanifahamu? Au nakufahamu wewe? Wee vipi mkuu... soma post yangu namba 17 utaelewa, au soma post za wengine wanaotoa ushuhuda wa kuambiwa waje siku ya pili kuchukua sticker. Sasa sisi tumeambiwa tuende kesho na tulilipia tangu wiki iliyopita. Na wale maofisa wa TRA Temeke wametuambia bila hata jicho la soni kwamba tukapaki magari. Watu wa daladala nusura warushe ngumi. Wewe kama hujui nyamaza kimya. si lazima sana uandike. Na ukiona una sababu ya kuandika basi nenda katafute ushahidi ndipo uje kubishia hapa.
 

Kwa maelezo hayo kaka inabidi nikupe pole tu sina zaidi, ila TRA wanakera si kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…