TRA wanaboa ile mbaya

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,212
Yaani hii nchi sijui tulete malaika kutoka mbinguni aje aongoze, yaani kila idara ya serikali utendaji kazi ni wa hovyo hovyo tu. Road license yangu ilikuwa inaisha tar nane mwezi huu. Nimekwenda TRA kulipia tangu tar 8, wakachukua hela yangu wakanambia hawana sticker. Nikaambiwa niifuate tar 12 (jana), ilipofika tar tisa nikapaki gari (bahati nzuri ilikuwa weekend), tar 12 (yaani jana nimekwenda kuulizia sticker naambiwa hazipo, leo tena nimeenda kuulizia wananambia hazipo labda hadi keshokutwa. Nawauliza sasa nifanyeje na gari, wananijibu kwa kiburi kabisa eti nipaki. Na kwa bahati mbaya njiani wakati narudi kwenda home polisi wamenikamata na wamening'ang'ania hadi nimelipa faini. Hapa nilipo nina hasira mbaya. Laiti ningemwona mkurugenzi wa TRA karibu yangu ningeweza hata kumrushia jiwe. Inakera inakera inakera kupita kawaida.
Najuta kuwa Mtanzania mie.
 
Ile imekuwa Taasisi ya kidini sasa hivi.Kuna udini pale na uchaga haujawahi kutokea nchi yeyote.labda kama unashida ya maombi ya kidini wangekusaidia
 
Mkuu pole sana, ukishakipia tembea na copy uliyolipia bank. Si Polisi wala majembe watakaokusumbua, kimsingi wanatakiwa kukamata wanaodaiwa na wewe hudaiwi.
 

Wenzio wanzifoji sana, wanahakiki kama yako iliyoisha ulilipia kihalali vumilia ...
 

Wenzio wanzifoji sana, wanahakiki kama yako iliyoisha ulilipia kihalali vumilia ...

Na road licence in grace period ya siku 30 kabla hawajakutwanga faini ya late renwal.
 


Kwani ulivyolipia haukupewa receipt? kama umelipa kihalali kuna receipt unapaswa upewe,na kama unayo kwa nini wakutoze fine.uwe makini siku nyingine
 
Mkuu pole sana, ukishakipia tembea na copy uliyolipia bank. Si Polisi wala majembe watakaokusumbua, kimsingi wanatakiwa kukamata wanaodaiwa na wewe hudaiwi.
ubungo nilikuwa na copy ya benk, lakini nimeambiwa zipo ambazo ni feki. Na wale polisi nafikiri sijui walikuwa hawajakusanya hela ya kukabidhi kwa bosi wao leo walikuwa hawaelewi kitu. wanasema wanataka kuona stiker na si habari ya stakabadhi. Yaani wameniboa kupita kawaida. Nimejikuta nawatukana matusi ya hovyo hovyo tu. Wangeweza hata kunishitaki maana wameanza kunitishia kwamba ninawaingilia kazi yao. Na wakasema si kosa lao nikawatukane TRA. So frustrated today. Ina maana kesho pia siwezi kuendesha gari langu, maana TRA wanasema hadi keshokutwa ndiyo nitapata stiker.
 
Last edited by a moderator:
Wenzio wanzifoji sana, wanahakiki kama yako iliyoisha ulilipia kihalali vumilia ...

Na road licence in grace period ya siku 30 kabla hawajakutwanga faini ya late renwal.
Niliwaeleza hili police. lakini wao wanasema hiyo grace periodi ni ya TRA na si ya polisi. Wao polisi wanaangalia tarehe inayoishia hiyo Road license. So tedious real.
 
Kwani ulivyolipia haukupewa receipt? kama umelipa kihalali kuna receipt unapaswa upewe,na kama unayo kwa nini wakutoze fine.uwe makini siku nyingine
Hata hiyo receipt nilikuwa nayo you cant imagine, yaani police wameigomea katakata wanasema zipo za kufoji siku hizi, kwa hiyo wenyewe hawaangalii list wanataka stiker yenye seal ya TRA. Yaani nimezozana nao for more than half an hour, wakakomaa eti nipeleke gari polisi. Na sikutaka kuendelea kupoteza muda.
 

usikubali kunyanyaswa, labda kama ulikuwa na kosa jingine, kwanza kukagua road lisence si kazi ya polisi kazi yao kuu ni kuakikisha kuwa gari lina bima na nisalama barabarani, wao wanaingilia majukumu ya TRA kudai kodi, pili kama ulikuwa na risiti na una muda wa mwezi mzima bado mwezi haijaisha na umeonyesha jitiada binafsi, watoa stika ndio wanakwambia zimeisha ufanyaje.
tatu TRA, ndio majizi makubwa ya nchi hii, asilimia kubwa ya kodi imapotea mikononi mwao, ukitaka kulipa kodi harari watapandisha mpaka ukome, ukikubali kugawana nao unalipa mpaka chini ya robo, kiwango harari.
 
Last edited by a moderator:
hwana sticka?hahhaaha kweli hii bongo mbona me leo nimtoka kurenew it did not cost me more than five min?yani ni kitu kimerudufiwa hapohapo mbele yangu.usilaumu police kuna mkakati flani nafikiri serikarlini wa kukisanya kodi ndo maaana unaona wameunganisha na za fire ext,na kama hujui wanasema watu wenge sa hivi wana document fake ndo bongo yetu
 
Pole sana mkuu. Mie wabaya wangu ni wale wapumbavu wa Ardhi makao makuu pale, ngoja ije siku nitaenda kujitoa muhanga niue building yote maana wananitapisha wale mafala aisee. Hili linchi limeoza limeoza limeoza! I hate Tanzania's system!!, i really do!!. Yaani tunaishi ktk nchi kama sio yetu!!!!!!!!!
 

Usilalamike sana, na ndio maana mimi nasema kila siku jamii hii yetu haiwezi kutoa kiongozi tunayemtegemea kututoa hapa tulipo hata siku moja, na sababu ni kwamba hakuna mazingira nchini mwetu ya kutoa huyo kiongozi, na hao watu wa TRA ndio taswira yetu sisi Watz, watu wanamlalamikia tu Bw. Kikwete na CCM lakini ukweli ni kwamba Bw.Kikwete na CCM kwa ujumla ndio sisi, na ushahidi upo wazi kila unapokwenda, kila unapogusa ni watu wa aina hiyo tu, halafu kama hilo halitoshi huyo huyo aliyekufanyia hayo hapo TRA utamkuta humu JF siku nzima anachangia na kulalamikia ufisadi sijui wa Bw. Kikwete au Bw. Lowasa, ukweli ni kwamba hakuna miujiza ni utamaduni tu na hulka ya jamii husika ndio inaleta maendeleo hivyo ingawaje inauma lakini ukweli ni kwamba kwetu hakuna hiyo jamii!


 
Watanzania tuache uongo. Ukishalipia bank . Kinachofuatia ni kupanga foleni wakuprintie road licence yako . Hakuna zaidi . Ni kitu cha dakika chache sana kutegemeana na foleni. Kuna mtu kasema hapo imemchukua dakika tano kupata road licence yake. Wabongo bwana kila mtu anataka ajitangaze ana gari . Labda wewe mwenzetu ni road licence ya ndege
 
Kaka hiyo ni ofisi ya Wapi ya TRA ambayo wamefanya hayo madudu? Ki ukweli ulitakiwa upate sticker yako siku hiyohiyo. Au ulimtuma mtu badala ya kwenda wewe mwenyewe?
 
kuna watu wanadhani jf ni sehemu ya kutafuta umaarufu . kwa mtu anayejua magari au aliyewahi kutumwa au kumiliki gari hakuna kitu kama hicho anachotuelzea huyu ndugu. labda kama naye amehadithiwa hiyo hadithi vijiweni. ukishalipa bank then unarudi ndani unakusanya docoument zako kusubiri wa print hiyo road licence . pia hakuna mtu atakayekubali kulipa fine wakati tayari unayo receipt ya bank kuonyesha umeshalipia na ina namba ya gari pia kama alivyoelezwa hapo juu kazi ya kukamata road licence sio ya police . then kama wamekukamata na wakakulipisha fine kwenye hiyo fine waliandika kosa gani coz wote tunafahamu kuwa kazi road licence ni ya tra . so police hawana faini hiyo......... labda kama uliazima gari au hukuwa na driving license so sio rahisi kujua sheria za barabarani . na pia ukiona police au traffic unachanganyikiwa . so kwa ushauri watu wa jf tusichukulie hii sehemu ni ya kudanganya watu . uongo mwingine uishie vijiweni .hili ni jukwaa la wasomi au ma great thinker yaani ni zaidi ya wasomi . kajipange tena au kama kitu hukijui kuuliza si ujinga
 
Wewe upo wapi ndugu? Kama upo Dar es salaam basi nenda TRA ya Temeke hata kesho asubuhi uulizie kama hizo road licence zipo? Na zinatoka kwa utaratibu gani? Wanaharaka tu ya kukupa form ukalipie lakini ukishalipia wanachukua kopi ya receipt yako halafu wanakupangia tar ya kwenda kuchukua. Kitu kizuri ni kwamba kwa kulipia ni hapo hapo kwenye benk ya exim hata huendi mbali kokote. Ingekuwa nakwenda kulipia mbali labda mngesema nilishindwa kurudi na list benk, sasa nimelipia hapohapo na nikarudisha list hapo hapo ndipo wakanipangia tar. Kwanini tuandikie mate ndugu? Hivi mimi nina akili gani ya kijinga nikubali kulipishwa faini na polisi ilihali ninajua kwamba ninaweza kuichukua tu?

Na ni vizuri ujue kwamba hii si mara yangu ya kwanza kulipia hiyo road licence TRA wala sina sababu ya kujitangaza kama nina gari. Itanisaidia nini wakati sikujui wewe wala mtu mwingine yeyote wa humu JF. Mimi nijitangaze kwa wasionijua ili kiwe nini? Kama wewe ni mfanyakazi wa TRA basi ujue wazi kwamba mnatukera kupita kiasi. Na nyie ndiyo mnachangia sana kuzorotesha maendeleo ya nchi hii.
 
Wewe uko wapi ndugu? Kama upo dar basi soma post yangu namba 17. Mkuu ulishawahi kuwaona TRA wamepanga foleni barabarani wanakamata magari yasiyo na road licence? Mbona ni wazi kwamba polisi ndiyo huwa wanakamata? Walichokataa ni zile list kwamba zinaeweza kufojiwa, kwa hiyo hiyo si kazi yao kutafuta evidence ya kwamba nina list harali.
 
Kaka hiyo ni ofisi ya Wapi ya TRA ambayo wamefanya hayo madudu? Ki ukweli ulitakiwa upate sticker yako siku hiyohiyo. Au ulimtuma mtu badala ya kwenda wewe mwenyewe?
Temeke. Wanasema mtandao upo slow. kwa hiyo wana list ndefu ya watu ambao wanahitaji kuprintiwa hizo sticker, na hadi kufikia leo walikuwa wanatoa sticker zilizolipiwa hadi tar nne, sisi wa kuanzia tar tano tumeambiwa tuende kesho kutwa. Sasa nashangaa kuna watu humu wanaleta ubishi tu wakati mimi ndiyo nimekumbana na dhahama hiyo.
 
jeneneke, habari ya document fake ndiyo niliyokuwa naambiwa na mimi na polisi. Kila nilipojaribu kueleza kwamba nimelipia hawajakubali kabisa kwa madai kwamba wengi wana hizo lisit ambazo ni za kufoji. Kwa hiyo polisi wanataka kuona ile stika yenye seal ya TRA.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…