TRA Tanga, nihurumieni jamani

Acha uoga.
Kama huna we tulia tuliii.
Endelea kufanya biashara yako.
mpaka waje wenyewe.waone na mjadiliane.
Wakiifunga saloon basi.
kwanza kodi kutoa ni huruma tu ya wananchi.
serikali nayo ipambane na hali yake
Iwe na vyanzo vyake vya kujiingizia mapato.
 
50,000? Kama hio ndio imekufanya ujje kufungua uzi wa malalamiko funga tu biashara.
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
Ongea na mwenyekiti wa mtaa akuandikie barua kuwa umefunga biashara yako hadi pale utakapowalisha tena kuwa umefungua. Wataluuliza kwa nini, waambie umeamua ukasome CBE kwanza
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
andika barua ya aidha kupungizwa kodi au kushindwa/kufunga biashara kutokana na changamoto mbali mbali, utaeleweka.
 
Kuna watu wawili wanaweza kukuelewa na kukusaidia!
1. Afisa elimu wa kodi yuko hapo ofisini.
2. Meneja wa mkoa!
Ni waelewa mno, nenda kwa meneja moja kwa moja umweleze haya uliyosema!
 
Kwani ukifunga biashara ukaanza kuuza vitumbua watakuja kukuuliza...watakupatia wapi...
Watakuja kukukamata tu watakuja kuona malimbikizo makubwa ya kodi, ukija kufungua biashara nyingne utaendelea kutumia ile TIN No, mwisho wa siku utakuja kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Anacho takiwa kufanya ni kutuma barua TRA ya kufunga biashara
 
Wananchi wazidi kulipa kodi tumalize SGR kabisa na Stiegler's Gorge.
shughuli itakuwa badoo sana kaka kuna vile viwanda vya cherehani vinatakiwa viwe vinachakata na kutengeneza malighafi zao pamoja na kuzalisha kwahiyoo afunge tuu akafunguee mtaa mwinginee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…