Tra na makanjanja wanaokaa nje ya lango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tra na makanjanja wanaokaa nje ya lango

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by haki na usawa, Apr 10, 2012.

 1. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi wafanyakazi wa TRA hamridhiki nini? mbona mna mishahara mizuri mizuri lakini ndo wala rushwa wakubwa
  kwanini dereva au mtu anahitaji TIN number anachukua muda mrefu anaambiwa aje wiki ijayo je ni haki?
  Lakini ukitoa kitu kidogo unashughulikiwa haraka? kama kuprint TIN number bado wanakuandikia katika karatasi ili uendelee na process? kwanini tusio na uwezo wakutoa pesa tusipewe huduma?
  Wanavijana wanakuambia we mzee leta msimbazi tu utapewa TIN number yako sasa hivi?
  Je watu wengine hamjakutana na kadhia hii?
  Je TAKUKURU wako wapi?
  Huduma ya bure kwa pesa mpaka lini?
  Kwanini mnasema HATUPOKEI RUSHWA wakati huduma mnasisitiza pesa?
  Mabango mlioweka milangoni ni nini maana yake kama nyinyi ni waongo na mnakula rushwa?
  Nashauri semeni TIN number inauzwa na si bure wananchi wajui aacheni usanii kuwa ni bure?
  Ni bora mkasema ili mlipwe na mboreshe huduma kuliko kuambiwa njoo wiki ijayo wakati wengine mnawaandikia haraka baada ya kutoa pesa?
  Hivi mnataka mlipwe mamilioni mangapi? mbona mwalim anatoa huduma bila kujali kipato cha mzazi?
  Je mnataka watu wasilipe kodi?
  Mbona mnatangaza watu walipe kodi kwa hiari kumbe nyie moyoni hamtaki hiyari?
  Naomba TAKUKURU waamke kwani TRA nao ni mafisadi papa wasioweza kukamatwa kwa huduma zao mbovu na za rushwa?
  Au nyie TAKUKURU mwazani rushwa ziko mhakamani tu?
  Naomba kusaidiwa ili haki ipatikane kwa watu wote na huduma BURE IWE BURE NA SI VINGINEVYO
   
Loading...