nxon
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,162
- 407
Juzi nilienda karikoo kujumua bidhaa zangu za biashara yangu mkoani, nilipata risiti za mashine baadhi na za mikono.
Nikachukua kirikuu kwa ajili ya kunisogezea mizigo yangu jangwani ambapo tunapakiza kwenye mafuso ya mikoani. Vile tunatoka TRA wakatusimamisha ili kukagua risiti, cha kushangaza wao wanataka za mashine tu, hawataki za kuandika na mkono, nilioata usumbufu mkubwa sana mpaka kuniachia.
1.Kuna maduka ya jumla kariakoo hawana mashine kabisa wao wanatoa risiti za kuandika na mkono hao ndio wapo wengi zaidi ya salimia 70℅.
2. Kuna maduka machache ya jumla wao wanatoa risiti za mashine ila hawaandiiki kiasi chote cha thamanibya mzigo, mfano mzigo umelipia tsh 1500000/- wao watatoa risiti ya tsh 250000/- tena kwa shida, ukiwalazimisha wakuandikie kiasi chote hawataki wapo radhi urudishe mzigo waliokuuzia na wakurudishie pesa yako ukose mzigo.
Sasa najiuliza
1)Je TRA hawajui kuwa kuna maduka mengi kariakoo hawana mashine za EFD?
2) Ina maana kodi wanayokata ni kubwa sana mpaka inafikia mfanyabiashara yupo radhi asiikuuzie bidhaa kama ukidai risiti halali ya EFD?
Ushauri kwa TRA:
1)Wafanye ukaguzi kwnye maduka yote kariakoo kuhakikisha kuwa wananunua mashine za EFD. mfano walipita huku kwetu Morogoro mwezi uliopita walifunga maduka yaliyokidhi vigezo vya kununua mashine ya EFD mpaka watakapo nunua mashine ndo yafunguliwe.
2) Warekebishe kiasi cha kodi wanazotoza 18℅ ya pesa iliouzwa ili kuepusha ukwepaji kodi kwa maana unawabana wafanyabiashara, tena kwa kuwashirikisha wafanyabiashara wenyewe.