TRA mko wapi? Selcom imeshirikiana na Azam Play TV kukwepa kodi (VAT) ya zaidi ya Bilioni 181

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
240
267
TAKUKURU, TRA mko wapi? Swala la Luku ni moja tu angalieni Selcom na Azam wanavyoifanyia serikali yetu bila aibu, katika malipo ya vighamuzi kunaukwepaji kodi wa kutisha uchunguzi wa siri ndani ya ofisi za Azam huu hapa

============

Selcom imeshirikiana na Azam Play TV kukusanya, kisha kukwepa kupeleka kodi (VAT) kwenda TRA ya zaidi ya Bilioni 181,44,000.000/=.

Kwa muda wa mwaka mmoja sasa kampuni ya Azam Pay TV (kampuni mtoto ya Azam Media LTD) imekuwa ikiendesha biashara ya kuuza maudhui (Channel) ya AZAM TV bila kulipa hata thumni ya Kodi.

Kwa uchunguzi tuliofanya tumegundua kwamba kampuni ya Azam Play TV ni kampuni mtoto ya Azam Media LTD Iliyosajiliwa Nchini Mauritius

na inafanya biashara hapa nchini bila Kuwakilisha kodi (VAT) inayokusanya TRA, licha ya wananchi kuilipa na VAT.

azam1.png

Tazama Hii Video ya SIRI

Mnamo tarehe 20 June 2015 taarifa za ongezeko la gharama za maudhui (Channels) zilisambaa kwa wateja wake kwamba wameongeza bei ya kila mwezi kutokana na serekali kuongeza Kodi /VAT, na Kuporomoka kwa Shilingi Tanzania, Huu ni Ujumbe mfupi wa simu ya mkononi [SMS]

ulizosambazwa na Kampuni ya Azam Media LTD
“Ndugu mteja, kutokana na serikali kuongeza VAT kwenye malipo ya Mwezi na ongezeko la thamani ya pesa za kigeni, inatubidi tuongeze bei ya vifurushi.

Hivyobasi kuanzia tarehe 1Julai 2015, malipo ya mwezi yatakuwa kama ifuatavyo: Azam Pure itakuwa 12,000,
Azam Plus 20,000, Azam Play 30,000. (nimembatanisha ujumbe wa SMS uliotumwa toka Azam Tv kwenda kwa wateja).

azam6.png

Juu: Ni ujumbe wa SMS uliotumwa kwenda kwa wateja kuwajulisha kwamba kutakuwa na malipo ya VAT kila mwezi tokea Julai 1, 2015)

Kwa uchunguzi wa kiinteligensia tuliofanya tumegundua kwamba kampuni ya Azam Media LTD inafanya utapeli mkubwa hapa nchini kwa njia zifuatazo:-

1. Kampuni ya Azam Media LTD inakampuni mtoto inayoitwa Azam Play TV (APT) ambayo haijasajiliwa hapa nchini Tanzania ila inafanya kazi hapa nchini.

(i) Kampuni ya Azam Media LTD inajishughulisha na kuuza Dishi, Decorder (kisimbuzi) na LNB pekee yake kwa thamani ya Sh 135,000/= pamoja na VAT. Mara moja tu.

(ii) Kitendo cha kuitumia kampuni ya Azam Play TV iliyosajiliwa nchini Mauritius ni kwa ajili ya kukwepa kulipa VAT ya gharama za kila mwezi ambazo ni pesa nyingi kwani hulipwa kila mwezi kwa wastani wa shilingi

28,000 x 12 = 336,000/=

ambapo 18% VAT ni Sh 60,480/= Kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Mapaka sasa Azam Tv wana zaidi ya wateja milioni tatu Tanzania peke yake, kwa hesabu rahisi ni kwamba, (wateja 3,000,000x VAT ya sh60,480 = Bil181,440,000.000/=) Kwa hiyo kwa mwaka jana peke yake. Kwa hiyo wamekusanya Bilioni 181,44,000.000/=

2. Kampuni ya Azam Media LTD ilipandisha gharama za kila mwezi kwa madai kwamba ni kutokana na serikali kuongeza VAT kwenye malipo ya Mwezi. Sasa Jambo la kujiuliza ni -

Je Hizo gharama za VAT kwenye malipo ya mwezi zinapelekwa wapi?

Tulipo fuatilia risiti zinazotolewa na kampuni ya Selcom na Azam Play TV kwa ajili ya malipo ya mwezi, tumegundua kwamba VAT ya 18%

haionyeshwi kwenye risiti kama walivyo dai kwenye ujumbe wao wa SMS. (Nimeambatanisha risiti ya AZAM PLAT TV na Selcom)
Azam2.png

Juu: Ni Risiti (NO.5386..) inayotolewa na kampuni ya Selcom / AZAM PLAY TV (***APT***) KWA AJILI YA MALIPO YA KILA MWEZI. Haionyeshi kulipwa kwa VAT
Azam3.png

Juu: Risiti inayotolewa na AZAM PLAY TV (***APT***) KWA AJILI YA MALIPO YA KILA MWEZI. Haionyeshi kulipwa kwa VAT .
azam4.png

Juu: Ni risiti inayotolewa na kampuni ya AZAM MEDIA LTD kwa ajili ya malipo ya kila mwezi (Miezi mitatu)

Ni wazi kwamba kampuni ya Azam Media LTD ikishirikiana na kampuni ya Azam Play TV hawajawahi kulipa kodi ya ongezeko la thamani kutokana na malipo ya mwezi (VAT) licha ya kuikusanya toka kwa wananchi kila mwezi. (Kama walivyo waambia wananchi kuwa wanaongeza bei ya kulipia kila mwezi kwa sababu wametakiwa walipe kodi VAT)

Tunatoa wito kwa TAKUKURU kuchunguza kampuni hizi na kuiwezesha TRA kukusanya mapato yanayostahili kutoka kampuni ya Azam Media LTD /Azam Play TV.

HITIMISHO;


Kwa makadirio, Kati ya tarehe 01Julai2015 mpaka tarehe 01Julai2016 Wamewatoza watanzania na wamelimbikiza VAT ya zaidi ya Bilioni 181,44,000.000/=.

Tunataka AZAM MEDIA LTD Wailipe TRA pesa zetu.
 

Attachments

  • Selcom imeshirikiana na Azam Play TV ya Mauritius kukwepa kodi.pdf
    2.5 MB · Views: 237
  • Selcom imeshirikiana na Azam Play TV ya Mauritius kukwepa kodi (1).pdf
    318.5 KB · Views: 141
Mkuu nakuombea kwa Mungu akupe ulinzi unaostahiki..sina shaka ktk hii issue lazima kuna vigogo wa TRA wanaopitia mlango wa uwani kuchukua rushwa ili kuilinda Azam sasa mnapotokea wazalendo kama nyie wanahamaki na wanaweza fanya chochote kulinda kula yao.TAKUKURU mmemsikia ni wakati wenu sasa kuyafanyia kazi haya mambo.
 
Bakhresa hawezi kuwa zuzu kiasi hicho.....mkakati wa kuwafanya matajiri wa nchi hii wanyanyasike na kuishi kama mashetani hautafanikiwa.....bakhresa ni world class businessman ....hawezi kukosea vitu vidogo tena katika mfumo wa malipo wa kidigitali

Siasa za kudhalilisha wazalendo naona mnazifanya sasa baada ya kuishiwa hoja na kusikia wananchi wakilalamika ugumu wa maisha
 
TAKUKURU, TRA mko wapi? Swala la Luku ni moja tu angalieni Selcom na Azam wanavyoifanyia serikali yetu bila aibu, katika malipo ya vighamuzi kunaukwepaji kodi wa kutisha uchunguzi wa siri ndani ya ofisi za Azam huu hapa

============

Selcom imeshirikiana na Azam Play TV kukusanya, kisha kukwepa kupeleka kodi (VAT) kwenda TRA ya zaidi ya Bilioni 181,440,000.000/=.
mkuu unauhakika na hicho ulichokiandika kwenye red hapo? naona tatizo la hesabu hapa.
 
You hinted us a very NICE source where Govnt can start investigation...!!
But kuweka sawa kabisa MATHS, kuna sehemu ndogo umekosea, but ur on point, ila hesabu umekosea kidogo:


Wateja: 3,000,000

VAT : 1: Kwa wateja wa Azam pure 12,000 ni wangapi then kila mmoja kwa mwaka ni 12,000 × 12 × IDADI YA WATEJA WA AZAM PURE × 18% VAT kwa mwaka..

2: 20,000 × 12 × IDADI YA WATEJA WA AZAM PLUS × 18% VAT kwa mwaka..!!

3: 30,000 × 12 × idadi ya wateja wa AZAM PLAY × 18% VAT kwa mwaka...!!

So, Total VAT, kiusahihi kabisa na iliyo halali kwa mwaka mzima... ni jumla ya VAT

1 + 2 + 3... hapo juu.. kwani Hao wateja 3,000,000 ni wateja wa vifurushi vyote 3 vya Azam pure, plus na play...!!

So, VAT, total hapo juu ukijua tu idadi wa wateja wa kila kifurushi UTAPATA HESABU SAHIHI, though again itakuwa na correction kidogo kidogo, mfano, kuna wateja wanaongezeka kila mwezi hivyo VAT kupanda, pia kuna wateja wachache kutoka, VAT kupungua kidogo... BUT YOU COME UP with very nice source, VAT ya SERIKALI LAZIMA ILIPWE...!! Hapo haraka haraka niki estimate kuna VAT over tshs. 100 Bil... serikali itapata, i can spot that haraka sana... but 181.4 Bil haiko sawa sana kimahesabu..!! but VAT is within that range..!!

Good job, tumsaidie Mh. Rais wetu mpendwa kufichua wakwepa kodi..!! Naamini vyombo vinavyohusika vitafanyia kazi hii hoja..!!

Tuipende nchi yetu jamani, hatuna nchi nyingine ni hii tu, wote tuisaidie serikali..

Nice day..!!
 
Bakhresa hawezi kuwa zuzu kiasi hicho.....mkakatkuwafanya kuwafanya matajiri wa nchi hii wanyanyasike na kuishi kama mashetani hautafanikiwa.....bakhresa ni world class businessman ....hawezi kukosea vitu vidogo tena katika mfumo wa malipo wa kidigitali

Siasa za kudhalilisha wazalendo naona mnazifanya sasa baada ya kuishiwa hoja na kusikia wananchi wakilalamika ugumu wa maisha

Mwenzako amekuja na udhibitisho Kwa kile anachokituhumu wewe unakuja Na blaha blaha tu huna unachokijua.

Sitashangaa baadae ukiingiza maswala ya Imani kwenye hizi tuhuma.
 
mkuu upo vzr, m sina utaalam wa kodi ila nmechunguza nmegundua ni kweli wanatupiga, maana hata ukinunua kwa sim, bado hakuna vat, TRA mkuje huku plz....
 
Back
Top Bottom