Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imethibitisha kuwa nyasi bandia za klabu ya Simba zilizopo bandarini zitapigwa mnada endapo Simba watashindwa kulipa kodi wanayodaiwa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema Simba pia wananafasi ya kuzipata nyasi hizo endapo watalipa kabla ya tarehe ya mnada.
Kwa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange amesema “Ni kweli nyasi hizo zimezuiliwa na sababu ya kushindwa kulipia ushuru TRA pamoja na kuomba msamaha serikalini walikataa kufuta ushuru huo.”
Kwa upande wake Kampuni ya ya Udalali ya Majembe (Majembe Auction) wamesema kuwa watazipiga mnada endapo Simba watashindwa kulipa ushuru hadi kufikia tarehe ya mnada.
"Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga *mnada* nyasi bandia za SIMBA SPORTS CLUB na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia *kodi*.
Mnada utafanyika Eneo la Nyuma ya "The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar", barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa *LW9*.
Maoni ya mwandishi:
Kama hili litatokea leo basi ni simanzi si kwa Simba tu bali familia nzima ya soka nchini.
Kabla ya kuutupia lawama uongozi wa Simba SC kwa kushindwa kutafuta njia mbadala za kutafuta fedha za kulipa kodi za nyasi hizi? Serikali kwa wizara yenye dhamana ya michezo na shirikisho la soka nchini iliwapasa kuwasaidia Simba SC katika hili hata kwa mkopo au dhamana fulani katika ile sera ya kuendeleza michezo nchini.
Tukirudi kwa uongozi wa Simba kama mlifikia kukwama kiasi hiki , si mngepitisha bakuli kwa wanachama wenu na wadau wa soka nchini ?! Hili suala lisiwe la aibu maana hizi timu ni za wanachama hivyo wana dhamana na timu yao.
Lakini pia huu ni uwekezaji mkubwa kwa Simba SC katika suala la miundo mbinu hivyo lilipaswa kupewa kipaumbele kuliko jambo lolote ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hii kuthubutu kumiliki uwanja wake . Hizo milioni 800 za kutafutia ubingwa si mngewekeza huku???? Daaah