TRA kodi ya mapato kwa bajaji ni hatari Lindi

TRA kodi ya mapato kwa bajaji ni hatari Lindi

RUT

Senior Member
Joined
Feb 6, 2013
Posts
144
Reaction score
28
Hivi sheria ya kodi ya mapato kwa pikipiki za miguu mitatu(Bajaji) zinasemaje?

Mimi ninavyofahamu ni kwamba hizi pikipiki zimefutiwa kodi lakini kwa usumbufu, unyanyasaji unaoendekea hapa Lindi Manispaa kwa Boda boda kukamatwa na kutozwa pesa kiasi cha Tsh 150,000 pamoja na pesa ya wakamataji tsh 50000 na kama fedha hiyo ikupatikana basi pikipiki ikilala TRA.

Unalipa kiasi cha Tsh 15000 kwa Siku kwa ajili ya gharama za eneo la kuweka bajaji hapo ktk ofisi za umma.

KWA HIYO JUMLA YA PESA TSH 215000 kwa Siku moja na hii pesa itaendelea kukua kadri ya pikipiki itakavyokuwa ilala TRA.

Kwa hali hii naomba WANABODI Munisaidie nifahamu ukweli wa hii hali au huu ni mwendelezo wa unyanyasaji wa TRA lindi.

Naomba watetezi munisaidiye na vijana wa bodaboda hapa lindi Manispaa.

Naomba mchango wenu.


Chanzo; mimi mwenyewe.
 
pambaneni jiungeni umoja ni nguvu,hawa jamaa tukiwalegezea watatuua.
 
Soon hata sadaka makanisani watataka kodi.nchi aina pesa jamaa kamkopesha odinga akitegemea kuwa nae atapiga bao la mkono kama yeye


Swissme
 
Soon hata sadaka makanisani watataka kodi.nchi aina pesa jamaa kamkopesha odinga akitegemea kuwa nae atapiga bao la mkono kama yeye

Tayari Wamesha anza kufanya upembuzi yakinifu!! where to start and how!
 
Ni hatari sana hii serikali, nchi ina dereva aliepoteana kiuongoz,,, hayo yanayofanywa Lindi ni hivo hivo Wamefanya Tunduma Songwe,, inaumiza mnoo... Imenitoka kama laki tano ivi kwa bajaj mbili,,, hoja sio kufanya kosa 2020,, Mbona wananyang'anya haki za wapiga kura hata wasipo pigiwa?? Daaaah huyu Ngosha sijui twaenda wap!!
 
Tayari Wamesha anza kufanya upembuzi yakinifu!! where to start and how!


Tetetrtertet eti where to start and how to take money from church.hahaha tutawapiga albadir nyingine



Swissme
 
Inaonekana Serikali kwa kukosa vyanzo vya mapato, wameamua kuingiza kodi katika vyombo hivyo yani Bajaji.
 
Guys hivi Shokapu Moya 1 ya Bajaji (Dukani) itakuwa bei gani ? Kulingana na eneo ulilopo.
 
Back
Top Bottom