TRA iwabane wachimba madini wadogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA iwabane wachimba madini wadogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kingadvisor, Dec 30, 2011.

 1. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachimbaji wengi wadogo miaka nenda rudi wawe wachimba Tanzanite mererani au dhahabu popote wamekuwa hawalipi kodi kwa kisingizio kuwa hawapati kitu wakati pembeni wanatamba wanapata mabilioni.Kutolipa kodi kwao ndiko kunaifanya serikali itafute wageni wafanye uchimbaji mkubwa kwenye hayo maeneo ya wachimbaji wadogo ili serikali ipate chochote.

  Wachimaji toka nje wakubwa wakishaanza kuchimba ndipo siri zinaanza kufichuka wachimbaji wadogo wanaanza kulalama kuwa wageni wanabeba mabilioni ya madini na kuacha wazawa hoi.Lakini kabla walikuwa wanajifanya hapo wanapochimba wanahangaika tu hamna kitu.

  Dawa ni machimbo ya wachimbaji wadogo yakianza tu TRA ihamishie makao makuu hapo na wawambie kama hamtalipa kodi tunaenda ishauri serikali iwaondoe aje mwekezaji atakayelipa kodi.wawaambie kwanza mnapoteza muda tu kwenye hayo machimbo kama hampati kitu fungeni virago mkafanye shughuli zingine.

  Sehemu kubwa kwenye machimbo waliko wawekezaji kulikuwa na weusi kibao wazawa wa nchi hii wanachimba miaka nenda rudi lakini uzalendo wa kulipa kodi hawana huku wakiwa wakali kwenye kudai huduma za jamii wapelekewe na serikali kwa kodi zinazokusanywa sehemu nyingine.

  Kama tunataka maendeleo wachimba madini wanaoitwa wadogo wabanwe nao kuna mabilioni kule wanapata wakisema hawapati tafuta FFU jaribu kuwatimua uone vita yake ya kukataa kutoka ndipo utajua serikali inavyoibiwa kodi na hao maruhuni wanaojiita wachimbaji wadogo.

  kingadvisor@yahoo.com
   
 2. papason

  papason JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mkuu huu uzi wako haujakaa vizuri kidogo yaan unajua hawa wachimbaji wakubwa wanaoondoka na mamia ya tani za dhahabu yetu wasamehewe kodi na serikali (tena faida yote ya dhahabu yetu wanapeleka kwao na kutuachia mashimo na mahandaki) alafu mchimbaji mdogo anaye ganga ka gram kamoja au tuwili ( Tena kafaida kadogo anakopata atajenga ka nyumba au kununua bodaboda au hata ka hiace ambako katawasaida wa TZ wenzake) abanwe vilivyo ili alipe kodi?
  Mimi nadhani kwanza serikali ingeanza kuwabana wachimbaji wakubwa kama Barrick, GGM, Resolute N.K ili waanza kulipa kodi zote wazopaswa kulipa kabla ya ku harass huyu small scale miner ambaye kimsingi ndiye huwa anakuwa mgunduzi wa mgodi na badaye huyu large scale miner anakuja kufukuza akisaidiwa na serikali
   
 3. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Aisee!!!
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  TRA inashindwa kuwabana wakina Barrick itawaweza wajimbaji wadogo? Mbona unachekesha kijana TRA ipi unayoizungumzia ile ya Kikwete legelege
   
 5. c

  comte JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 80
  Papason,
  mtoa mada yuko sahihih kabisa kila azalishae lazima alipe kodi na mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe, achana na wageni. Hivi hizo nyumba , hiace na toyo ni zetu wote ?
   
Loading...