TRA huu ni zaidi ya unyanyasaji!

TRA huu ni zaidi ya unyanyasaji!

white wizard

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2011
Posts
8,618
Reaction score
13,890
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadiria kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka ni 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mimi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!
 
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadilia kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka na 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!

kakuona zuzu.....
 
ndio maana wale wa PAP, walisema mtaji ni elf 50 wakapotezea ile $.

hii nchi, ujanja ujanja sn.
 
kodi ya ardhi inakusanywa kwa tabu sana ndio iyo ya kupangishia jengo itawezekana ?.
 
Sasa kama wewe ni mfanyakazi tayari umeshafyekwa kodi, tena ya kihalali haipungui hata senti. Sasa tena ulipie na kodi kwenye pango si ndiyo double payment hiyo?

Just thinking aloud na hizo sera zao.
 
kakuona zuzu.....

mkuu, sio kwamba kamuona zuzu. hiyo kodi inaitwa stamp duty. ni kodi ambayo wananchi wengi hawana uelewa nayo. ni 1% ya monthly rental price.
 
Hiyo kodi kama ungelipa ungekua mjinga wa mwaka 2014/2015.

Hakuna kitu kama hicho kama walihitaji hiyo kodi ungewapa mkataba wakafatilia wenyewe hio kodi tena bila ya kukuathiri wewe na mwenye nyumba.

Nchi hii wengi tunashindwa kuelewa haki zetu ni zipi kwakua hawaweki wazi wanatupa zile za kutunyanganya chetu tuu.

Juzi niliwasikia Tra wanasema eti wamefuta kodi za forodha kwakua mashine ziweze kutumika lakini cha ajabu mpaka kesho ukiingiza mzigo unalipishwa kodi hizo za forodha kama kawaida.

Kila mwenye nafasi anakula kwa kamba yake
 
Mambo mengi sana yanapangwa kwenye vikao vyoa, wanakubaliana wenyewe lakini wananchi hawapewi elimu yoyote, unakuja kuambiwa tu utekeleze.
 
mkuu, sio kwamba kamuona zuzu. hiyo kodi inaitwa stamp duty. ni kodi ambayo wananchi wengi hawana uelewa nayo. ni 1% ya monthly rental price.

Mkuu hivi ni 10% au 1% kwani kuna mfanyakazi wa tra nimemuuliza kuhusu kiwango hicho akasema ni asilimia 1, ya stamp duty na sio asilimia kumi, asilimia kumi ni withholding tax?? Sasa kipi sahihi?? Hata kama ni asilimia moja, sitakiwi kulipa mimi.
 
Ndio utatatibu wanaotumia mkuu, no way you can escape that.

Mbona kuna biashara ya wife amefuatilia TIN namba wilaya ya mkuranga amekadiliwa kodi tu hayo mengine hamna? Kama suala la mkataba? Ina maana TRA, Nayo imekuwa kama halmashuri kila sehemu ina ushuru wake? Kitu ambacho ctaki kuamini kama ni kweli.
 
Mkuu hivi ni 10% au 1% kwani kuna mfanyakazi wa tra nimemuuliza kuhusu kiwango hicho akasema ni asilimia 1, ya stamp duty na sio asilimia kumi, asilimia kumi ni withholding tax?? Sasa kipi sahihi?? Hata kama ni asilimia moja, sitakiwi kulipa mimi.

Ni 1% ya kodi ya mwezi. kwa kua mkataba ni wa mwaka, ndo maana wanazidisha tena kwa 12. ni kweli kuna utata kwenye nani alipe. kwa makampuni mara nyingi kampuni ndo hulipa kukepwa usumbufu wa tra. ukikutwa hujalipa penalty ni 200% ya amount uliyotakiwa kulipa. Sasa kwa kua stamp duty amount ni ndogo, na penalty ni kubwa sana, makampuni huamua kulipa wao wenyewe. ukimtegemea mwenye nyumba utalipa penalties sana tu
 
Hapo ni sawa,
kodi za majengo zinaangukia katika kipengele cha "Withholding Tax". Hii ni aina ya kodi ambayo hukatwa from "the source". Kwenye fungu hili hata kodi kutokana na mishahara-PAYE zinaangukia humu.

Yaani mlipa hela (Mpangaji au Mwajiri) anamkata kabisa kodi mlipwa hela (Mwenyenyumba au Mfanyakazi) na kuipeleka TRA.

Ukitaka wewe ulipe rent kisha Mwenyenyumba ndio akalipe kodi, vipi waajiri nao wakitaka wawalipe mishahara mizima mizima wafanyakazi wao kisha wao wafanyakazi ndio wakalipe kodi wenyewe?
 
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadiria kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka ni 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mimi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!

MkuU KaSome sHerIa kwaNza ndo Uje haPa kUlaLaMika. maLipo Ya pango yanaYozidi shilingi 500,000 hupigwa kodi kwa asilimia kumi na ukusanyaji wake huwa katika mfumo wa withholding. Sheria ya kodi ya mapato inasema wewe mpangaji ndo utakuwa withholding agent wa mpangishaji waKo iki mAaniSha kwaMba UnaTaKiwa kUkAta Asilimia KuMi ya MaLipo kAbla uJamlipa MpaNgisHaji waKo nA kuPeleKa T.R.A as witholding tax. Hapo afisa wa T.R.A yuko sahihi sema ni wewe kama taxpayer unatakiwa uwe na elimu ya kodi au tafuta consultant awe anasimamia mambo yako yote yahusiaNaYo nA koDi.
 
Tatizo sio kutokuwa na elimu ya kodi, kinacholeta utata ni kwanini sio kwa kila mfanyabiashara? Mke wangu amefuatilia TIN, mkuranga na amepata hayo mambo ya kulipia mkataba wala hata hakukutana nalo!! Na hata jana kazini na sehemu mbalimbali nimejaribu kuulizia kila mtu anashangaa!! Kuwa labla kama mfumo huu umeanza mwaka huu, na wao wengine mwaka jana wameomba tin na hakuna kitu kama hicho!!!
 
Hapo ni sawa,
kodi za majengo zinaangukia katika kipengele cha "Withholding Tax". Hii ni aina ya kodi ambayo hukatwa from "the source". Kwenye fungu hili hata kodi kutokana na mishahara-PAYE zinaangukia humu.

Yaani mlipa hela (Mpangaji au Mwajiri) anamkata kabisa kodi mlipwa hela (Mwenyenyumba au Mfanyakazi) na kuipeleka TRA.

Ukitaka wewe ulipe rent kisha Mwenyenyumba ndio akalipe kodi, vipi waajiri nao wakitaka wawalipe mishahara mizima mizima wafanyakazi wao kisha wao wafanyakazi ndio wakalipe kodi wenyewe?

Hapa mkuu nawe umechanganya!! Mi sizungumzii Property tax.Kwani hii hukusanywa na halmashauri husika, japo kwa dar jukumu alikabidhiwa TRA, alichemka.hilo suala lako la PAYE hilo lipo ki sheria, sasa hili la mikataba ya pango inawezekana liko kisheria sasa inakuwaje uniambie mimi kuwa kodi ya mwenye nyumba mnikate mimi eti wao huwa hawakubali!! Hivyo nilipe mimi then nika negotiate naye akikubali kuni refund powa akikataa basi!!! Huoni kuwa kuna tatizo hapo??? Then mnategemea kuongeza tax base kwa mwendo huu!!! Jiulize kwanini TRA walichemka kukusanya hiyo property tax???? Wakawa wanaacha magorofa ya kariakoo wanakimbilia vijumba vya mbagala?? Na inakuwaje mtu akachukue TIN namba wilaya ya mkulanga asikutane na kodi hiyo?! Ndio vitu vinavyotakiwa kujibiwa.
 
mkuu, sio kwamba kamuona zuzu. hiyo kodi inaitwa stamp duty. ni kodi ambayo wananchi wengi hawana uelewa nayo. ni 1% ya monthly rental price.

Hapana siyo stamp duty bali hiyo kodi inaitwa Withholding tax ambayo kimsing mlipaji anatakiwa amkate yule anayemlipa yaani 10%.Hii inamaana kwamba kama kodi ya pango ilikuwa ni 1,200,000.00 basi inatakiwa amlipe mwenye nyumba 1,080,000.00 halafu 120,000.00 uwape TRA.Kama nchi hii itakusanya kodi ipasavyo ni vigumu mwananchi wa kawaida kuendelea unless utoe Rushwa hebu fikiria una kampuni yako kodi zilizopo ni kama zifuatazo,

1. City service Levy ambayo ni 0.3% ya turnover yako kwa mwaka bila kujali unapata faida kiasi gani au hasara? Hii ni kodi mbaya sana kama makampuni yote yangekuwa yanalipa sawasawa basi mengi yangefilisika.Makampuni mengi hayalipi hapa nchini.
2. Withholding Tax kama ambayo jamaa analalamika.
3. VAT
4. Corparate Tax 30% ya Net Profit.
5. Bado wewe kama Mkurugenzi ulipe PAYE (individua Income).
6. Kama unaagiza bidhaa zako kutoka nje basi utakumbana na Import Duty, VAT na Excise Duty.
7. Bado hujawalipia wafanyakazi NSSF, PPF, etc.
8. Property Tax kama unamiliki majengo.
9. Leseni za magari kama unamiliki magari tena siku hizi TRA wasivyojua kujali wateja hawatoi hata stika ya kubandikia Road License.
10. Bado kuna Parking fees ambazo wanachaji siku hizi hadi kwenye nyumba za watu.
11. Bado hujalipia Fire extinguisher bila hata kukagua gari na kukupa mtungi wa fire.
12. Bado ulipie stika ya week ya nenda na usalama.
13. Ziko nyingi Mno kama stamp duty, etc.
14. Bado hujakutana na foleni kubwa Dar es Salaam ambayo inapoteza mafuta mengi na muda wa kufanya kazi.

NDIO MAANA UKITAKA KUENDELEA KIBIASHARA LAZIMA UKWEPE KODI KWA ASILIMIA FULANI.MAKAMPUNI MENGI SANA NCHINI NA HATA DUNIANI YANAKWEPA KODI WANACHOZIDIANA NI VIWANGO VYA KUKWEPA KODI VINGINEVYO YASINGEKUWEPO.HAPA NDIO LILE FUNGU LINALOSEMA MPE MUNGU VILIVYO VYAKE MUNGU NA MPE KAISARI VILIVYO VYAKE KAISARI LINAPOAPPLY.
 
MkuU KaSome sHerIa kwaNza ndo Uje haPa kUlaLaMika. maLipo Ya pango yanaYozidi shilingi 500,000 hupigwa kodi kwa asilimia kumi na ukusanyaji wake huwa katika mfumo wa withholding. Sheria ya kodi ya mapato inasema wewe mpangaji ndo utakuwa withholding agent wa mpangishaji waKo iki mAaniSha kwaMba UnaTaKiwa kUkAta Asilimia KuMi ya MaLipo kAbla uJamlipa MpaNgisHaji waKo nA kuPeleKa T.R.A as witholding tax. Hapo afisa wa T.R.A yuko sahihi sema ni wewe kama taxpayer unatakiwa uwe na elimu ya kodi au tafuta consultant awe anasimamia mambo yako yote yahusiaNaYo nA koDi.

kuna utata kidogo juu ya hii kodi, halmashauri za wilaya zimekuwa zinadai kuwa ndio zenye wajibu wa kukusanya wakati huohuo tra nao wanaidai, sasa hebu tufafanulie niwakati gani nalipa halmashauri na wakati gani npa tra?
 
Back
Top Bottom