GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Kwa hiyo huyo mama akifa leo TRA ndo inakuwa imekufa?? Mi nahisi hayo ni majibu ya mzembe mmoja kwenye hicho kiseksheniNdugu wana bodi,
Najua humu ndani ya Jukwaa letu la JF lina wanachama na wapenzi ambao hupitia humu ndani mara kwa mara. Kwa maana hiyo basi , ujumbe unao wekwa humu husomwa na wengi.
Suala ni hivi, watu wa TRA ASCUDA huu ni uzembe wa hali ya juu. Kuna jamaa yangu aliagiza gari na amelipa ushuru kama ilivyokuwa inatatikana na gari tangia Jumatano wiki iliyopita ( 20.03.2013) ilitoka ila mpaka leo hii TRA hawajatoa kadi ya gari. Maelezo aliyoyapata ni kuwa, kuna mama mmoja tu kwenye system yao ya Ascuda ambae anatakiwa aingize data kwenye system , na tangia ijumaa mpaka leo hii hajafika kazini na hana mbadala wake. Kweli huu ni utendaji bora wa kazi kwa mamlaka kubwa kama TRA ambayo inategemewa na uchumi wa nchi ?. TRA tuache kufanya kazi kwa mazoea na kwa utaratibu wa kizamani, kama mtu hayupo wekeni mbadala wake. Mh. Kitilya hebu rekebisheni hili TRA mmekuwa na mfumo mbovu sana.
Kwa hiyo huyo mama akifa leo TRA ndo inakuwa imekufa?? Mi nahisi hayo ni majibu ya mzembe mmoja kwenye hicho kiseksheni
ASCUDA na siasa wapi na wapi!!!
Mkuu hebu jiongeze kwa kuingia mfukoni na kunyoosha mkono. We huoni hapa jamaa wenye kuuza magari kwenye show rooms wanavyoingia na kutoka???
TRA hii ya CCM ni janga la kidunia, wanaona kama mlipa kodi ni mtu mwenye shida wakati inatakiwa kuwa vice versa
Mkuu, sie ndio twatakiwa kuonyesha mfano wakupata haki zetu bila kutoa rushwa. Mtu ametimiza wajibu wake wakulipa kodi huna budi kumuheshimu na ww kutimiza wajibu wetu. Na kila siku wanatoa matangazo ya wananchi kulipa kodi bila kushurutishwa, wao kumbe msemo wao huo ni unafiki mtupu.
Tatizo siyo system ya Asycuda,tatizo wafanyakazi wa TRA wanakula deal na wenye ICDs akina
Kinana muua Tembo wetu,ili magari yalipe storage kubwa.
Siku hizi koment zako ziko tofauti sana na zile za zamani... za siku hizi zinafana na jina lakoMkuu hili ni janga kwa kweli
Mkuu hii TRA ilitakiwa kufanyiwa overhaul siku nyingi sana. Hiyo ASCUDA yenyewe hadi waliposhikiwa bakora ndio wakaanza kutumia. Wao walikuwa wanapenda ule mfumo wa zamani wa mafaili ndio walikuwa wanakula sana.
Sasa hivi kisingizio chao ni huyu mama yuko mmoja tu kwa hiyo njoo saa nane, ukienda saa nane wanakwambia njoo kesho asubuhi hadi wiki inapita. Ukiwatumia mawakala ambao wana mtandao nao kwa ile wanaita FAST TRACK siku mbili tu tayari una kadi ya gari tayari kwa kufuatilia insurance na plate number
Siku hizi koment zako ziko tofauti sana na zile za zamani... za siku hizi zinafana na jina lako
Alaaa, kumbe! Kwa maana hiyo TRA = SIASA? Sasa kama ni hivyo kwa nini mnashangazwa na hayo yaliyotokea?Mpita Njia , TRA purely ni sehemu nyeti ya Serikali ambayo inakusanya mapato ya serikali kwa ajili yaku hudumia shughuli za maendeleo na za kawaida za serikali, huna njia yakuitoa ndani ya serikali . Na serikal ni sehemu ya siasa
Alaaa, kumbe! Kwa maana hiyo TRA = SIASA? Sasa kama ni hivyo kwa nini mnashangazwa na hayo yaliyotokea?
Ingependeza kama ingewekwa kule kwenye mambo ya business
Mkuu tuelimishe wewe sasa ulitaka iende jukwaa lipi ?
Mkuu hili ni janga kwa kweli