Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) imepanga kutumia Dola 110.45 milioni za Marekani kujenga gati na matangi ya kuhifadhia mafuta ghafi yatakayokuwa yakisafirisha na bomba la mafuta la kutoka Uganda.
Fedha hizo zitatokana na vyanzo vya ndani ya mapato vya TPA na zitatumika kwa miaka mitatu tofauti huku kila mwaka ikitumia Dola 30 milioni za Marekani.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Mipango ya TPA,Alfred Matuntelo ametoa taarifa hiyo leo wakati wa mkutano wa maandalizi ya awali ya kupokea mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda uliofanyika jijini Tanga.
Akizungumza katika mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mkuu waMkoa wa Tanga,Martine Shigela na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) amesema ujenzi huo unatarajiwa kuendeshwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Source: Mwananchi