Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,075
- 2,316
Nawaomba wabunge mpendekeze tozo ya "wharfage charge" itozwayo kwenye mizigo ipitiayo bandari zetu ifutwe ili kuhamasisha wafanyabiashara wa nchi jirani kupitishia mizigo kwenye bandari yetu ya dar es Salaam. Ukiangalia kwa undani, tozo hii haina maana yoyote kwa sababu sio sehemu ya ukokotoaji wa gharama za bandari. Gharama za bandari ni "handling charges". Tozo hi kwa hivi sasa inatozwa ma TRA ambayo kimsingi haitakiwi kukusanya fedha zozote kutoka kwa wapitishaji wa mizigo ya transit. Inatozwa kwa kiwangi cha 1.25% ya thamanai ya mzigo kama ulivyokadiriwa na TRA lakini ni tozo ambayo haiko kwenye orodha za kodi zinazosimamiwa na TRA. Ni tozo iliyokuwa inatozwa na TPA lakini baada ya kuanza kukusanywa na TRA bado TPA haijalalamika mapato kupungua. Sasa ni wakati bora wa kuiangalia na kujiuliza, je kuna umuhimu wa kuendelea kukusanya tozo hii bila kueleweka ama ni kodi au ni gharama za bandari? Naiona kama tozo ya unyanyasaji tu.