Tozo ya kulipia Sh. 100/- ili kupata taarifa zako toka NIDA ni biashara ya kihuni isiyo na makubaliano!

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,734
Reaction score
1,150
Ibara ya 8 -,(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi kwa wananchi wake.

Kwa kuzingatia hili hapo juu katika kustawisha wananchi wake, serikali imeona umuhimu wa kuwatambua wananchi wake kwa utambulisho wa kupitia kitambulicho cha utaifa (national identity).

Zoezi hili limeratibiwa na NIDA na limeibua upungufu mkubwa sana kiutendaji kutokana na kukosa ufanisi, ambao wa kulaumiwa ni serikali.

Pamoja na Bunge kutenga bajeti ya kukamilisha zoezi la kusajili vitambulisho hivi, bado Watanzania wengi hawana vitambulisho hivi, pamoja na kuwa bajeti yake ilipangwa.

Hii ni kiashiria kingine cha harufu ya ufisadi kwenye zoezi zima.

Leo badala ya kuzungumzia vitambulisho, Watanzania wana hangaika kutafuta namba za vitambulisho vyao toka NIDA, vitambulisho ambavyo utaratibu wake na structure yake hautofautiana na vitambulisho vya mpiga kura.

Ikiwa zoezi la upatikanaji vitambulisho vya mpiga kura lilifanyika na watu kuondoka na vitambulisho vyao, hili la vitambulisho vya Taifa lilipata ukakasi gani.

Wapo Watanzania wengi hawana vitambulisho hivi kutokana na ukiritimba ulio sababishwa na NIDA, lakini kwanini sasa serikali kabla haijafikiria kutekeleza zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, lisinge kuwa na haraka kuhakikisha ugawaji wa vitambulisho hivi unapatiwa uvumbuzi wa haraka kuliko kuwashughulisha wananchi kuhangaikia namba za vitambulisho vyao ilihali hawana vitambulisho hivi.

Hii ni sawa na kumuuzia mfugaji kamba ya kumfungia mbuzi, ukimuaminisha mbuzi atazaliwa muda si mrefu.

Kwa kuzuia udhaifu wa zoezi zima la usajili usionekane, serikali kupitia NIDA kwa ushirika wa TCRA imeanzisha biashara ya tozo mpya ya 100/- kusaka namba za kitambulisho cha utaifa, kitambulisho ambacho bado kipo kwenye mikono yao,kwa kuanzisha zoezi la usajili mpya wa laini za simu kwa alama za vidole.

Imeelekezwa na serikali ukitaka kupata Namba ya kitambulisho chako cha utaifa piga namba *152*00# hapo utakutana na maelekezo jinsi ya kupata namba yako toka NIDA kwa gharama ya 100/- kupitia mpesa, tigopesa na makampuni mengine ya simu yenye huduma kama hiyo.

Lakini ndani ya sekunde zisizo 20s utapata majibu ya makato ya fedha 100/- yakiambatana na ujumbe wa aina mbili, ujumbe wa risiti ya serikali ya muamala ulioufanya na ujumbe unao kutaarifu kuwa taarifa zako hazipatikani.

Huu ni uhuni usiokubalika kwa walipa kodi kuwatoza tozo wakati kodi yao ndiyo iliyo tumika kuratibu zoezi zima, hii ni biashara mpya isiyo rasmi na hatujui ni sheria ipi iliyopitishwa na bunge kuruhusu yanayo fanyika sasa.

Hebu fikiri kwa kina;

Watanzania mathalani milioni 1 wanamiliki laini za simu labda kwa kampuni ya vodacom,ukiwatoza 100/- maanake ni kwamba;

Watu 1,000,000 * 100/- = 100,000,000/-

Hizi zinaingia kwenye mfuko wa serikali, lakini hatuambiwi zinawekwa kwenye fungu gani kwa mujibu wa sheria ya makusanyo.

Serikali itueleze ni kwanini imeamua kutuletea biashara isiyo rasmi ya kupata taarifa zisizo andaliwa wakati ikitutoza fedha, tukisema huu ni uhuni au ufisadi tutakuwa tumekosea!!!

Serikali iache kutuumiza wananchi kununua huduma zisizo julikana kwa mgongo wa kusajili laini ikiwa utaratibu wa vitambulisho haujakidhi malengo.

Tuamke, hiki ni kizazi cha kuhoji, tutahoji mpaka dakika ya mwisho.
 
sammosses Umeona hiyo Tsh 100 unesahau nauli ya mtu anatoka mwakitolyo nauli ni sh 6000 kwenda na kurudi 12000 na bado anaambiwa njoo wiki ijayo akija tena anaambiwa njoo jumatatu..hili ni janga kubwa kwa watu wa vijijini hasa hao wanyonge. wangeiga mfano jirani zetu kenya hii habari ya vitambulisho waliisha isahau..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu walichojifunza kupitia kwa January Makamba (I am not a fan of his just because he is over ambitious, but he listens) those are the traits of a good leader.

Baada ya kutoa deadline ya mifuko ya plastic kupitia malalamiko ya wadau aliona mapungufu ya wizara na kujikita kwanza wao kujipanga upya, kuhakikisha kuna mifuko mbadala etc na maandalizi sahihi ya kutekeleza azma yao.

Hawa jamaa pamoja na kwamba kila leo watu wanalalamikia operation za NIDA ndio tatizo watu kupata ID na kujisajili swala ambalo hata kwenye taarifa ya habari unaona watu walivyojaa nje ya ofisi za NIDA wakilalama wanavyozungushwa.

Badala ya serikari kutaka kujua operation strategy yao kuona wamejipanga vipi na kama kweli wana capacity ya kutoa huduma kwa idadi ya wateja waliopo hadi deadline date serikari if not watenge tarehe sahihi . Serikari yenyewe imekazana kuwalaumu wananchi as if wana choice.

Hawa wakurugenzi wa mashirika ya serikari sijui wanaokotewa wapi unaona jitu halina uwezo halafu linapewa nafasi kubwa.
 
Umeona hiyo Tsh 100 unesahau nauli ya mtu anatoka mwakitolyo nauli ni sh 6000 kwenda na kurudi 12000 na bado anaambiwa njoo wiki ijayo akija tena anaambiwa njoo jumatatu..hili ni janga kubwa kwa watu wa vijijini hasa hao wanyonge.. wangeiga mfano jirani zetu kenya hii habari ya vitambulisho waliisha isahau..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni tatizo na uonevu kwa wananchi
 
Wakati zoezi linaanza vyeti vya kuzaliwa havikuhitajika, lakini leo unaambiwa lazima uwe na cheti. Kupata cheti lazima ulipie gharama si chini ya 15000/-,ina maana hata kuzaliwa kwako Tanzania lazima ulipie.

Ukiangalia chanzo cha mnyumbuliko wa mapato ya serikali kwa kigezo cha kitambulisho cha utaifa kinazidi hata ile kodi ya kichwa iliyo futwa na MZEE Mkapa.

Serikali imefanya huduma za kijamii kuwa chanzo cha mapato, pamoja na utitiri wote wa kodi. Sijui tunaponea wapi Watanzania
 
100 tu? Ishakuwa kesi?

You guys just say "ANYTHING THAT GIVES CREDIT TO JPM MTALALA NACHO MBELE"
 
Hata wakoloni walijenga reli na vingine lakini walitunyonya, hatuoni matunda ya uhuru ikiwa tuna kandamizwa kila kukicha, iko wapi impact ya vitambulisho vya ujasiriamali!!!

Hizi ni deal za watu kama ilivyokuwa speed governor.
 
Unakandamizwa kivipi? Enlighten me?

Kuhusu ID za ujasiriamali eti hazina impact kwako au?

Cool down open your mind!

There is nothing ever good made without negative effects, as long as these good outrank bad effects we go with it.

Vitambulisho vya ujasiriamali vimesaidia wafanya biashara wadogo wadogo kujikwamua, while wakubwa wakibanwa na makodi, yeti wakubwa wameamua kugawa mzigo kwa vijana wawauzie kwa mgongo wa vitambulisho vya ujasiriamali.

Na mkuu nijibu unakandamizwa kivipi na 100 ya NIDA?
 
Unashangaa pita daraja la nyerere,buku 2 unaiacha getini.

Kumbuka road licence nalipia pia.

Tunasubiria na kwenye fly ova watuwekee fee pia.

Kuna jambo gani la muhim daraja la nyerere ambalo ni tofauti na madaraja mengine kama la mkapa pale rufiji,kilombero,ama kule malagarasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa kwa nini Police hawaiwakamati NIDA kwa uhujumu uchumi. Hawa NIDA ndiyo wahujumu uchumi maana wanadhulumi wananchi masikini sammosses
 
Hata wakoloni walijenga reli na vingine lakini walitunyonya, hatuoni matunda ya uhuru ikiwa tuna kandamizwa kila kukicha, iko wapi impact ya vitambulisho vya ujasiriamali!!!

Hizi ni deal za watu kama ilivyokuwa speed governor.

Matunda ya Uhuru!

- Maisha Mazuri.
Yanapatikana ukiwa na chanzo cha kipato au tuseme ajira. Serikali inaandaa mazingira ya ajira kupitia sera zake.

Ikiwa sera ya vitambulisho imelenga kusaidia tabaka dogo kujipatia kipato ila kuinua maisha yao tunasemaje hapa? Japokuwa tabaka kubwa linaathiriwa.

Kuhusu miradi mikubwa ya ujenzi haina faida katika kumuinua watanzania? Sidhani kama ni wote tutafaidi ajira za miradi hiyo japokuwa inaweza kutengeneza mapato yatakayo saidia kuinua sekta nyingine.

Japokuwa approach ya miradi mikubwa haikuwa nzuri yaani kuwazawadia makampuni ya kigeni hivyo fedha kwenda nje badala ya makampuni ya ndani kuongeza mzunguko wa pesa na kuinua kiwango cha maisha, hapa nakuwa mkweli sijafurahishwa.

Matunda mengine ni yapi twende kwa kina?
 
Unakandamizwa kivipi? Enlighten me?

Kuhusu ID za ujasiriamali eti hazina impact kwako au?

Cool down open your mind!

There is nothing ever good made without negative effects, as long as these good outrank bad effects we go with it.

Vitambulisho vya ujasiriamali vimesaidia wafanya biashara wadogo wadogo kujikwamua, while wakubwa wakibanwa na makodi, yeti wakubwa wameamua kugawa mzigo kwa vijana wawauzie kwa mgongo wa vitambulisho vya ujasiriamali.

Na mkuu nijibu unakandamizwa kivipi na 100 ya NIDA?
Hizi tozo kila kukicha siyo ukandamizaji!!?,ukienda halmashauri wanakuambia ingia kwenye simu, piga *152*00#,unazungumzia 100/- hiyo 100/-*5 bila taarifa si wizi huo!!?

nieleze vitambulisho hivi vimesaidiaje wajasiliamali!!?
 
100 tu? Ishakuwa kesi?

You guys just say "ANYTHING THAT GIVES CREDIT TO JPM MTALALA NACHO MBELE"
Lazima iwe kesi kwasababu hakuna justification ya tozo hiyo!

Fikiria Mwananchi aliyejiandikisha tangu July hadi leo hajapata hiyo namba, kosa ni la nani?

Kuna sababu gani ya kumtoza hiyo Tsh.100 anapoulizia taarifa zake?

Kwa hali ya kawaida hapo nani anatakiwa kulipia usumbufu wa mwenzake kati ya huyo Mwananchi na NIDA ni nani anamsumbua mwenzake?

Tukiendelea kudharau vitu vidogo vidogo kama hivi kwa kutojali madhara yake mbeleni ni kuiendekeza serikali na huu uonevu mdogo ndio huzaa uonevu mkubwa

Ukiangalia zoezi linavyoendelea kwa sasa wakurugenzi na wasemaji wa haya mashirika mawili NIDA na TCRA wamegeuka kuwalaumu wananchi kwamba wamejichelewesha wenyewe kwamba zoezi lilianza zamani sana

Lakini ukiangalia uhalisia tangu zoezi lianze foleni hazijawahi kuisha kwenye vituo vya NIDA kwa baadhi ya maeneo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujivunia kukusanya kingi lakini tuna nyang'anya mpaka shilingi ya mwisho!!! Uko wapi ustawi wa wananchi kwa operation zima moto kama hizi.

Watanzania wanazaliwa na kukuwa kila siku kwanini zoezi lisiwe endelevu.

Tuache kuchezeana
 
Ibara ya 8 -,(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi kwa wananchi wake.

Kwa kuzingatia hili hapo juu katika kustawisha wananchi wake, serikali imeona umuhimu wa kuwatambua wananchi wake kwa utambulisho wa kupitia kitambulicho cha utaifa (national identity).

Zoezi hili limeratibiwa na NIDA na limeibua upungufu mkubwa sana kiutendaji kutokana na kukosa ufanisi, ambao wa kulaumiwa ni serikali.

Pamoja na Bunge kutenga bajeti ya kukamilisha zoezi la kusajili vitambulisho hivi, bado Watanzania wengi hawana vitambulisho hivi, pamoja na kuwa bajeti yake ilipangwa.

Hii ni kiashiria kingine cha harufu ya ufisadi kwenye zoezi zima.

Leo badala ya kuzungumzia vitambulisho, Watanzania wana hangaika kutafuta namba za vitambulisho vyao toka NIDA, vitambulisho ambavyo utaratibu wake na structure yake hautofautiana na vitambulisho vya mpiga kura.

Ikiwa zoezi la upatikanaji vitambulisho vya mpiga kura lilifanyika na watu kuondoka na vitambulisho vyao, hili la vitambulisho vya Taifa lilipata ukakasi gani.

Wapo Watanzania wengi hawana vitambulisho hivi kutokana na ukiritimba ulio sababishwa na NIDA, lakini kwanini sasa serikali kabla haijafikiria kutekeleza zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, lisinge kuwa na haraka kuhakikisha ugawaji wa vitambulisho hivi unapatiwa uvumbuzi wa haraka kuliko kuwashughulisha wananchi kuhangaikia namba za vitambulisho vyao ilihali hawana vitambulisho hivi.

Hii ni sawa na kumuuzia mfugaji kamba ya kumfungia mbuzi, ukimuaminisha mbuzi atazaliwa muda si mrefu.

Kwa kuzuia udhaifu wa zoezi zima la usajili usionekane, serikali kupitia NIDA kwa ushirika wa TCRA imeanzisha biashara ya tozo mpya ya 100/- kusaka namba za kitambulisho cha utaifa, kitambulisho ambacho bado kipo kwenye mikono yao,kwa kuanzisha zoezi la usajili mpya wa laini za simu kwa alama za vidole.

Imeelekezwa na serikali ukitaka kupata Namba ya kitambulisho chako cha utaifa piga namba *152*00# hapo utakutana na maelekezo jinsi ya kupata namba yako toka NIDA kwa gharama ya 100/- kupitia mpesa, tigopesa na makampuni mengine ya simu yenye huduma kama hiyo.

Lakini ndani ya sekunde zisizo 20s utapata majibu ya makato ya fedha 100/- yakiambatana na ujumbe wa aina mbili, ujumbe wa risiti ya serikali ya muamala ulioufanya na ujumbe unao kutaarifu kuwa taarifa zako hazipatikani.

Huu ni uhuni usiokubalika kwa walipa kodi kuwatoza tozo wakati kodi yao ndiyo iliyo tumika kuratibu zoezi zima, hii ni biashara mpya isiyo rasmi na hatujui ni sheria ipi iliyopitishwa na bunge kuruhusu yanayo fanyika sasa.

Hebu fikiri kwa kina;

Watanzania mathalani milioni 1 wanamiliki laini za simu labda kwa kampuni ya vodacom,ukiwatoza 100/- maanake ni kwamba;

Watu 1,000,000 * 100/- = 100,000,000/-

Hizi zinaingia kwenye mfuko wa serikali, lakini hatuambiwi zinawekwa kwenye fungu gani kwa mujibu wa sheria ya makusanyo.

Serikali itueleze ni kwanini imeamua kutuletea biashara isiyo rasmi ya kupata taarifa zisizo andaliwa wakati ikitutoza fedha, tukisema huu ni uhuni au ufisadi tutakuwa tumekosea!!!

Serikali iache kutuumiza wananchi kununua huduma zisizo julikana kwa mgongo wa kusajili laini ikiwa utaratibu wa vitambulisho haujakidhi malengo.

Tuamke, hiki ni kizazi cha kuhoji, tutahoji mpaka dakika ya mwisho.

Lines za simu tunaambiwa zahitaji namba za NIDA. Hii Ina maana kibongo bongo wageni hata waliopo hata ki halali nchini hawaruhusiwi kuwa na lines za Tanzania?

Zoezi hili lina ukakasi mwingi.

Bora hata hizo siku 20 za nyongeza waziondoe tu wafunge hizi lines kama walivyokuwa wamepanga.
 
Exactly
 
Back
Top Bottom