Tozo kwenye soko na ahadi ya kampeni kuwasaidia wafanyabiashara wadogo

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Serikali yetu iliahidi kuwasaidia wafanyabiahsara wadogo wadogo kufanya biashara kwa urahisi bila bugudha na kuwasaidia kukuza kipato. Katika soko la Bomang'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Halmashauri ya Hai inawatoza wafanyabiashara kodi ya eneo wanalotumia kuuzia bidhaa zao sh 15,000 kwa mwezi. Wote waliokuwa wanauza mboga, nyanya na vitunguu chini wamefukuzwa na kuwaruhusu wanaouza mtumba.

Sawa kiafya ni vizuri ila kiwango hicho cha tozo ni kikubwa kwa mwezi (wanaombwa ya miezi 3) ukizingatia kwamba bado kuna ushuru wa kila siku na soko hilo wanaoingia hapo walio wengi huuza hapo siku ya soko ambayo ni Jumatano na Ijumaa, wengi ni wale wenye biashara ndogo ndogo wanalalamika kuwa halmashauri ya mji inawatoza hela kubwa maana hawaji kila siku.

Soko la kwa Sadala waliandamana na kufunga barabara kwa sababu hiyo. Hata kama ni vyanzo vya mapato kwanini hatujasikia kwenye madini kunaguswa na ndio kwenye pesa nyingi?

Ningeiomba serikali kuu isaidie kuangalia swala hili walau kwa mwezi wawatoze sh 5,000 na ushuru walipe hili litawasaidia wanyonge kuuza chochote kile. Kwa sasa ukiwa mnyonge huwezi kwenda kuuza sokoni pale lazima uwe na sh 45,000 ndipo upate meza, kama huna kaa nje hangaika kivyako.

Wanyonge wasinyanyaswe na kutopewa maeneo ya kufanyia biashara kisa serikali inahitaji mapato, kwa mtazamo wangu matajiri wananufaika zaidi ya wanyonge. JPM anasema anawatetea na kuwasaidia wanyonge hapa ni kinyume na maneno yake.

Tukumbuke ahadi za serikali kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 
Back
Top Bottom